KAMATI ya Ulinzi na Usalama
Mkoa wa Mbeya limepiga marufuku maandamano yoyote kufanyika Mkoani hapa yenye
lengo la kushinikiza Raisi Kikwete kumfukuza kazi Waziri wa Elimu kutokana na
matokeo mabaya ya kidato cha nne. Maandamano hayo yalipangwa
kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) Machi 25, Mwaka huu,
ambayo yamepangwa kuhusisha Mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini na kufanyika
Jijini Mbeya kwa lengo hilo. Akitoa taarifa ya Kamati
hiyo kwenye Mkutano wa ushauri wa Mkoa (RCC),Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk.
Norman Sigalla amesema kamati hiyo ilikaaa Machi 19, mwaka huu na kuamua kuwa
hakuna mantiki ya kufanyika kwa maandamano hayo. Amesema sababu iliyoonekana
ni kwamba tayari tume imeshaundwa kuchunguza madai hayo hivyo hamna sababu ya
watu kuandamana kushinikiza waziri kujiuzulu ili hali kamati itakuja na majibu
juu ya kile kilichosababisha matokeo kuwa mabaya.
Sigalla amesema kamati ya
Ulinzi na Usalama imeona kuwa kuendelea kufanya maandamano soyo ufumbuzi wa
matatizo bali yataathiri shughuli za kujitafutia kipato kwa wananchi wa kawaida
pamoja na usalama wa mali. Ameongeza kuwa usalama wa
Wananchi wa Mkoa wa Mbeya utaathirika kutokana na wanaotarajiwa kufanya
maandamano hayo wamehamasishwa kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma ambako kutajaza
idadi kubwa ya watu. Amesema kamati pia inaamini
kuwa maandamano ya aina hiyo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani hivyo
kamati inapiga marufuku maandamano ya aina yoyote kufanyika Mkoani Mbeya na
kuongeza kuwa yapelekwe maeneo mengine.
Aidha ametoa rai kwa
vikundi vya kisiasa, kijamii na vikundi vya dini kuweka mbele maslahi ya
wananchi kwa kuhimiza kujitafutia vipato kutokana na fursa za maendeleo
zilizopo. Hata hivyo Mwenyekiti huyo
wa kamati ya Ulinzi na Usalamaya Mkoa ameviagiza vyombo vyote vya Ulinzi na
usalama kuendelea kuhakikisha kwamba Mkoa wa Mbeya unaendelea kuwa tulivu na
amani ambayo itawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kujiongezea kipato
bila bugudha yoyote. Maandamano hayo yamepangwa
kufanyika Machi 25, Mwaka huu kufuatia Mkutano wa Hadhara uliofanyika hivi
karibuni wa Chadema katika Viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe Ilomba
Jijini Mbeya Februari 28, Mwaka huu, ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho taifa
Freeman Mbowe aliagiza kufanyika kwa maandamano hayo kwa namna yoyote ile.
Pia katika kuhakikisha
dhana hiyo inatimia Mwenyekiti huyo pia alichangisha zaidi ya Shilingi Milioni
Tatu ambazo alidai kuwa zitasaidia wakati wa maandamano katika kununulia maji
ya kunawa baada ya kupigwa na mabomu pia kununulia dawa za huduma ya kwanza kwa
watakaoathirika na maandamano hayo.
Source: Mbeya Yetu (March 2013). Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mbeya imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa na CHADEMA tarehe 25 Machi, 2013. Retrieved from Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment