Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, March 1, 2013

MADIWANI CCM WACHAPANA NGUMI



JESHI la Polisi wilayani Kwimba mkoani Mwanza, linawashikilia madiwani wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kosa kuchapana ngumi wakati wa kikao cha baraza la madiwani jana. Madiwani hao na kata zao kwenye mabano ni Shija Malando (Hungumalwa)na Tabu Maganga (Mhande). Tukio hilo, ambalo lilionekana kuwashangaza madiwani na viongozi wa Halmashauri ya Kwimba, lilitokea jana saa 5 asubuhi na kusababisha shughuli zote kusimama kwa muda. Kutokana na kuchapana ngumi ovyo ovyo, madiwani waliumizana vibaya sehemu za usoni. Akidhibitisha kukamatwa kwa madiwani hao, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kwimba (OCD),Dk. Enock Rukiyaa alisema mpaka jana mchana viongozi walikuwa wanaendelea kushikiliwa kwa vile kupigana ni kosa.

Alisema kwa mujibu wa maelezo ya awali, madiwani hao wamekuwa na ugomvi wa muda mrefu kutokana na mambo yao binafsi. “Tumepata maelezo yao ya awali, inaonekana wamekuwa na ugomvi wao binafsi kwa muda mrefu… lakini inaonekana wamekuwa wakiwindana mno,”alisema OCD Dk.Rukiyaa. Alisema anasikitishwa kuona viongozi ambao ni wawakilishi wa wananchi, wanaamu kupigana baadala ya kutetea matatizo ya wapiga kura wao. Akizungumzia suala la dhamana, OCD Rukiyaa alisema bado wanaendelea kuwahoji kwa kina zaidi ili wafikishwe mahakamani kujibu kosa linalowakabili. “Hapa suala la dhama kwa sasa halipo,haiwezekani waheshimiwa hawa wapigane mbele ya hadhara mchama kweupe, kisha tukaharakisha kutoa dhamana…bado tutaendelea kuwashikilia na kuwachukua maelezo zaidi,kitendo walichokifanya ni cha ajabu kabisa”,alisema OCD Dk Enock.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba, Abbas Mwijuki alisema amesikitishwa na kitendo hicho na amepanga kukutana na OCD ili kujua ni hatua gani zaidi zitachukuliwa dhidi ya madiwani hao. Alisema wakati madiwani hao wanapigana, alikuwa hajaingia ukumbini na alipata taarifa za tukio hilo wakiwa tayari wamefikishwa kituoni. Kuhusu hatua ambazo CCM,itachukua baada ya madiwani hao kuonyesha utovu wa nidhamu,Mwijuki alisema kuna mambo mawili ambayo yanatarajiwa kufanyika. Alisema kama madiwani hao, litafikishwa mahakamani chama hakiwezi kuchukua hatua zozote za kisheria na kinidhamu.

Pili endapo suala hilo, litashindikana kupelekwa mahakamani basi chama kinatarajia kuwaita na kuwahoji madiwani haraka iwezekakanvyo kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo kupitia kamati husika, zikiwamo za Kamati ya Maadili na Kamati ya Siasa ili iwe fundisho kwa wengine. Juhudi za MTANZANIA kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Zephania Masangu hakufanikiwa kutokana na simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.


Source: Maduhu J. (March 1, 2013) Madiwani CCM wachapana ngumi. Mwanza. Retrieved from Mtanznaia

No comments: