Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, March 24, 2013

MAANDAMANO MBEYA, IRINGA, ARUSHA, RUVUMA, NJOMBE YAZUIWA



Serikali imezuia maandamano yote yalyokuwa yafanyike tarehe 25.3.2013 katika Mkoa wa Mbeya na Arusha yalikuwa yanaratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama Cha Mapinduzi (CCM). CHADEMA waliomba kufanya maandamano katika mkoa wa Mbeya kuishinikiza Serikali iwawajibishe Waziri wa Elimu na Naibu wake wajiuzulu kufuatia matokeo mabaya ya Kidato cha Nne 2012. Maandamano ya CHADEMA yalipangwa kuhusisha wanachama kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma. Kwa upande wake, Chama Cha Mapinduzi kilipanga kufanya maandamano yake Mkoani Arusha kupinga kusudio la CHADEMA kuandamana wakieleza kwamba wana imani na Tume malum ya Waziri Mkuu inayochunguza tatizo la kufanya vibaya wanafunzi wa Kidato cha Nne 2012.

Serikali imesitisha maandamano hayo kutokana na ukweli kwamba tarehe 25.3.2013 ni siku muhimu kwa Watanzania tutakapompokea Rais mpya wa China, Xi Jinping ambaye atakuwa na ziara ya siku mbili nchini. Kwa kuwa, Tume Maalum iliyoundwa na Waziri Mkuu inaendelea na uchunguzi wa suala la kushuka wka ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne 2012 si vyema vyama vya siasa CCM na CHADEMA vikaingilia mchakato huo wa uchunguzi. Serikali inatoa wito kwa wananchi kutoshiriki maandamano hayo badala yake wajitokeze kwa waingi kutoa mawazo kwenye Tume ya Waziri Mkuu.

ASSAH MWAMBENE

MKURUGENZI IDARA YA HABARI (MAELEZO)

No comments: