Najua kama umekua karibu na media katika siku za
karibuni, stori kuhusu uongozi wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
kutangaza mpango wa kutaka bunge lisiwe linaonekana live kwenye TV utakua
umeisikia. Ni maoni mengi ya Watanzania yametolewa huku
asilimia kubwa ikionekana kupinga huo mpango ambao lengo lake ni kukwepa
kuonekana kwa wabunge wanaovunja kanuni kwa kuropoka na kufanya vurugu.
Kwenye hii post ni maoni maalum ya mbunge wa Kawe
Halima Mdee ambae namkariri akianza kwa kusema “mmhh… kwanza ni hoja ya kipuuzi
sana na muhimu ikaeleweka kwamba bunge ni moja kati ya mihimili mitatu ya dola,
kinachoonekana kutaka kufanyika ni muhimili mwingine wa dola kutokutaka umma
ujue ukweli kwa kutumia watumishi wa bunge kwa mantiki ya katibu wa bunge kwa
sababu yeye ndio ametoa hilo tamko ili kuzuia Watanzania wasipate taarifa
ambazo tokea bunge limeanza kurushwa live wamekua wakizipata tofauti na ambavyo
walikua wanapewa hizo taarifa katika mazingira ambayo sio ya wazi”
Kwenye sentensi nyingine Mh Mdee amesema “nasema
hivyo kwa sababu kupitia bunge Watanzania wamejua mikataba mibovu ya madini,
wamejua EPA, wamejua Richmond, Buzwagi, wamejua jinsi gani fedha zinavyotengwa
kwa ajili ya bajeti zimekua zikitumika vibaya sana kupitia CAG report ambazo
zimekua zinajadiliwa live, Serikali imeona inaumbuka na ikaamua sasa kupitia
katibu wa bunge na kina Lukuvi, tunataja majina ya watu sababu tuna uhakika na
tunachokisema na juzi imeumbuka, sasa wanatafuta statergy ya kuficha”
“Kama mlikua mnafatilia bunge la juzi mmeona kwamba
wameweka sheria kusema kwamba mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG taarifa
yake akiisoma haitajadiliwa hadi mwaka tena mwingine upite waende tena kuedit
na kuleta majibu ya uongo, kwa hiyo kuna mrundikano wa vitu vingi ambavyo
Serikali inaona mambo yakiendelea hivi inawezekana 2015 wakifika watakua
wamechoka, sasa wanazuiaje? kwa kuleta vitu vya ajabu ajabu… kwa hiyo waache
wananchi wajue nini kinachoendelea, kuna kanuni za bunge kama Mbunge anakiuka
kanuni” – Halima Mdee
Source: Audiface J. Blog (February 17, 2013). umesikia alicho kisema Halima Mdee... Retrieved from Audiface J. Blog
No comments:
Post a Comment