Kwa marafiki na wapenzi wangu wote
tulio shirikiana kwenye kampeni zangu, Liberatus Mwang’ombe, za ubunge 2015
jimbo la Mbarali;
Kwanza kabisa naomba samahani kwa
kuchelewa kuwashukuru wote mlio tumia muda wenu, mali zenu, na nguvu zenu
kwenye kampeni hizi. Nawashukuru kwa
kunipa support ya kifedha, mawazo, vyombo, ushirikiano usio na kikomo; na
kuniamini.
Natambua wazi tumepita kwenye kampeni
ambazo ni ngumu na zenye changamoto nyingi, lakini hata siku moja hamkuweza
kuniacha. Tulilia pamoja, tulicheka pamoja na tulifurahi pamoja na tuli
huzunika pamoja. Kuna siku zilipita bila
hata kupata chakula cha mchana; lakini, kwa sababu lengo letu lilikuwa ni moja,
hatukuteteleka. Mwisho wa siku
tumemaliza kampeni salama kwa uwezo wa mwenyezi Mungu.
Kwa umoja wetu tumeweza kuionyesha
Mbarali, Tanzania na dunia kuwa tukiungana na kuamua kufanya kitu hakuna wa
kutuzuia. Tumefanikiwa kwa kuweza
kufikia kata zote 20; na kufanikiwa kupata madiwani 8 kutoka 2 tulio kuwa nao
2010. Kwa pamoja tulishirikiana kwa
nguvu zote na maarifa yote.
Hadi tunamaliza uchaguzi matokeo
yalikuwa kama ifuatavyo:
Haroon Mulla (CCM) 45,352
Liberatus Mwang'ombe (CHADEMA) 36,603
Modestus Kirufi (ACT) 20,606
Gamdust Hajji (CUF) 382
Getruda Pwilla (NCCR) 120
Nurdin (UPDP) 114
Siumii
kunyang'anywa ushindi Mbarali. Naumia navyo ona wakina mama, vijana na wazee wa
Mbarali walio jitolea kwa moyo moja bila kulipwa kufanikisha kampeni zetu
wanavyo toa machozi na kuja nyumbani wakiniuliza haki yao ipo wapi. Tunaishi
kwenye nchi ambayo hata ukipiga Kura; huna hakika kama itahesabiwa, na hata
kama ikihesabiwa; huna hakika kama itaenda kwa yule uliye mpigia.
Tumemaliza
kampeni na uchaguzi; najua inaumiza sana, lakini ni wakati wa kurudi kwenye
maisha yetu ya kawadi na kuondoa makandokando na tofauti zilizo jitokeza
kipindi cha kampeni. Sisi wote ni wamoja
na naamini hakuna ambaye aliingia kwenye kampeni kwa maslai binafsi; wote
tulikuwa tunapigania maslai ya Mbarali na Tanzania yetu.
Assanteni
sana kwa ushirikiano, umoja na mapenzi mliyo yaonyesha kipindi cha kampeni na
sasa. Nisinge fikia hapa bila ya nyinyi, kwani ili niwe mimi ni lazima nyinyi
muwepo; vinginevyo “I’m nothing”.
MUNGU IBARIKI
MBARALI, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Liberatus
Laurent Mwang’ombe
BAGASA2015
UJASIRI WA
KUAMUA/UJASIRI WA KUTHUBUTU
No comments:
Post a Comment