PRESS
BRIEFING;
CHAMA CHA
DEMOKRASIA NA MAENDELEO -CHADEMA
YANAYOJIRI
NJOMBE - BVR
1. Ikiwa
zoezi la uandikishaji limeanza leo tarehe 23 Feb na likitarajiwa kuzinduliwa
rasmi kesho tarehe 24 Feb na Waziri Mkuu Pinda, Naibu Katibu wa CHADEMA upande
wa Tanganyika ameanza Operesheni R2R BVR ambapo asubuhi mpaka mchana alikuwa
katika Mji wa Makambako akipitia mitaani pamoja na msafara wa viongozi wa chama
hicho ngazi mbalimbali kuhamasisha wananchi kujiandikisha.
Aidha,
Operesheni hiyo imehusisha kukagua utaratibu wa uboreshaji kwa kutumia BVR
kwenye vituo mbalimbali ambapo imebainika kwamba udhaifu uliokuwepo wakati wa
majaribio na mwingine mpya umebainika katika sehemu kubwa ya vituo
vilivyotembelewa.
Baada ya
kubaini udhaifu huo Mnyika na timu ya maafisa wa CHADEMA iliyoweka kambi katika
mkoa wa Njombe ikihusisha wataalamu wa TEHAMA (ICT) wamekutana na Mkurugenzi wa
NEC Mallaba na kueleza kuhusu udhaifu huo.
Mfano
katika kituo cha Malombwe mpaka saa 6 mchana mashine zilikuwa hazifanyi kazi.
Hali kama hiyo imejitokeza katika kituo kituo cha Liamkena ambapo uandikishaji
ni taratibu kwa kiwango mpaka saa 4 waliandikishwa watu watano tu.
2. Aidha,
pamekuwepo na tatizo la watu wenye mikono yenye vidole sugu kutokana na kufanya
kazi ngumu mashine kugoma kuwatambua na hivyo kukataliwa kujiandikisha.
Hali kama
hiyo imejitokeza mfano katika kituo cha Sigfrid, Malombwe na vituo mbalimbali.
Kufuatia hali hiyo ambapo Operesheni R2R BVR iliamua kutembelea vituo zaidi na
kubaini kwamba vipo ambapo mashine hazikuwa zikifanya kazi kabisa mathalani
Lumumba.
Kwa ujumla
katika vituo vingi ukiondoa matatizo ya mashine upo pia udhaifu wa
waandikishaji na waendeshaji wa vifaa vya BVR (Kit Operators) ambao wanashindwa
kutumia mashine hizo na walipohojiwa baadhi walikiri kwamba wamepewa mafunzo
siku moja kabla ya kuanza uandikishaji huku wakiwa hawajawahi kutumia kompyuta
wala kuwa na ujuzi wa ICT.
Wapo
waandikishaji ambao walionyesha kutokuwa na ufahamu wa upigaji picha na hivyo
kufanya zoezi kwenda taratibu na pia kupiga picha zinazoonekana vibaya.
Kasi ndogo
ya uandikishaji huku siku zikiwa saba na kwa kituo inaashiria bayana kwamba
wapo wananchi ambapo mwishowe watakosa fursa ya kujiandikisha.
Operesheni
R2R BVR imebaini mpaka sasa kuwa pamoja na kutumia alama za vidole mfumo
umeacha mianya mpiga kura kujiandikisha zaidi ya mara moja katika vituo tofauti
tofauti kwa kuwa hakuna mawasiliano ya kimfumo kati ya kituo kimoja na kingine.
Mfumo
unategemea kwamba taarifa zikitumwa kanzidata kuu (central databank) ya tume
ndiyo itakayochambua wakati ambapo hakutakuwa na mawakala katika hatua hiyo
kuthibitisha uondoaji wa wapiga kura waliojiandikisha zaidi ya mara moja kwa
kuzingatia kwamba katika kipindi cha uhakiki wa daftari la awali napo hakuna
mwingiliano baina ya daftari la eneo kwa eneo wakati wa ukaguzi.
Aidha,
CHADEMA imeweka mawakala katika vituo vyote lakini wanapata vikwazo vya namna
vya kudhibiti uchakachuaji katika hatua ya usafirishaji wa takwimu ambapo
mifumo miwili inatumika kwa wakati mmoja; wa kutumia simu na ule wa kuhamisha
kwa kutumia kifaa cha kuhifadhi taarifa (flash drive) bila uhakiki wa mawakala.
Operesheni
R2R BVR katika mazingira hayo haitaishia tu kuwa na mawakala kwenye vituo bali
kukagua mfumo mzima.
4. Naibu
Katibu Mkuu Mnyika ametaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika uzinduzi wa BVR
Makambako tarehe 24 Feb aeleze namna Serikali ilivyoiwezesha tume kushughulikia
udhaifu huo kwa kuzingatia kwamba mabilioni yametumika kwenye zabuni ambayo
imeleta vifaa vibofu hali inahitaji uchunguzi kufanyika kubaini iwapo hali hiyo
imetokana na ufisadi au imefanywa makusudi kuachia mianya ya uchakachuaji
katika uchaguzi.
Mara baada
ufuatiliaji huo jioni ya leo patafanyika Mkutano wa uzinduzi wa Operesheni R2R
BVR jukwaani katika Jimbo la Njombe Kusini na kesho kutwa tarehe 25 Operesheni
R2R inahamia wilaya ya Wang'ing'ombe kwenda kuhamasisha wananchi kujiandaa
kujiandikisha.
Tumaini
Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano -CHADEMA
No comments:
Post a Comment