Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, December 3, 2014

UKAWA: Tumefanikisha wizi Escrow kujulikana

Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha
Wananchi (CUF),Magdalena Sakaya
.

Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umesema kuwa ndiyo uliofanikisha kwa kiasi kikubwa umma wa Watanzania kufahamu wizi wa wa fedha za umma zaidi ya Sh. bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na waliopokea mgawo. Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya (pichani), katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana ya chama hicho (JUVICUF). Alisema wabunge wa Ukawa walipigana usiku na mchana na wale waliokuwa wakisambaza ujumbe wa uongo ili kujaribu kuzima umma usifahamu ufisadi uliofanywa na viongozi wa dini pamoja na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Dodoma tulikuwa hatulali, hatunywi, kuna kikundi cha watu kiliibuka kuzima jitihada zetu za kuufahamisha umma tulipambana nacho hadi mwishowe tukawashinda,” alisema Sakaya.

“Ufisadi huu umechangia matatizo mengi katika nchi yetu yakiwamo wananchi kuswekwa ndani kwa kushindwa kuchangia maabara, wengine kuyakimbia makazi yao, wanafunzi kukosa mikopo, kinamama wajawazito kukosa huduma muhimu, walimu kushindwa kumaliziwa madeni yao na vijana kukosa mikopo,” alisema. Aidha, aliwataka vijana wanaotaka kuingia katika uongozi kuwa na nia ya dhati ya kuliletea taifa maendeleo kwa kupambana na ufisadi uliokithiri huku akiwasistiza kuwahamasisha Watanzania kuikataa Katiba inayopendekezwa. Sakaya alisema wao ndiyo waliokuwa wa kwanza kupendekeza katiba itakayowanufaisha wananchi, lakini cha kushangaza iliyosambazwa ni ya kikundi cha watu fulani kinachofanya kampeni ipitishwe. Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Getrude Ndibalema, amewataka vijana kuwa nguvu ya maendeleo kwa kushiriki katika kuleta mabadiliko.
 

Nipashe

No comments: