Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, December 15, 2014

CCM kwachafuka,mchawi anatafutwa

Leo hapa Lumumba hakukaliki.Hakusemeki jema. Hasira zimetanda. Nyaraka kalikali zinapita kutoka huku kwenda kule. Ofisi zetu hapa leo zinakuwa chungu.Kisa,UKAWA kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM kama Monduli. Makada wanalaumiana,vikao visivyoisha.Lakini,ni vikao kwa kukalishwa na si kukaa.Kukalishwa na kusimangwa. Kukemewa. Kushambuliwa.

Inasemwa hapa kuwa lengo la CCM halijatimia.Iitakiwa CCM ishinde kwa asilimia 90. Hadi sasa,hali ni tete.Mikoa yetu tuliyokuwa tunaitegemea imetuangusha. Majimbo yetu yaliyokuwa imara,yamesambaratika. Wabunge wetu wanaojitutumua Bungeni kama majembe ya chama, hawajasaidia kupatikana asilimia 90. Mambo ni shaghalabaghala. Mchafukoge!

Kambi za Urais na Escrow zinatajwa kama sababu kuu. Ziara za Katibu Mkuu wa chama nazo zinapondwa kwa kukosa matunda ya maana. Hakuna pa kushika,hakuna wa kumtupia lawama za moja kwa moja. Lakini,wakuu wanamtafuta wa kumwangushia 'jumba bovu'.Mchawi wa matokeo haya.

Kwani ni dhambi wapinzani kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

No comments: