Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, April 20, 2014

Polisi Kuizuia Ukawa, inawasaidia wananchi kuhoji kulikoni!

Na Bryceson Mathias

KOSA linalofanywa na Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutumia vyombo vya Dola (Polisi na vingine) kuwazuia Ukawa, vinaakisi kosa la Shetani kumuua Yesu akidhani kuwa amekufa, lakini kila alipokwenda alimuona akitenda kazi, kumbe yu hai!

Kosa kama hilo pia alilifanya Farao ili kuwazuia wana Israel wasitoke Misri kwenda nchi ya Ahadi ya Asali na Maziwa, wakiongozwa na Musa, ili waendelee kuteswa na kufanya kazi ngumu za matofali na Chokaa. Kutoka 1:7.

Vivyo hivyo Serikali ya CCM katika hali inayoonekana inaivisha Polisi na Vyombo vya Usalama Joho lake kupambana na UKAWA, inafanya kosa pasipo kujua, kwa sababu kimsingi wakienda mikoani, watayaona mapambano na madai hayo yakihojiwa midomoni mwa wananchi.

Askofu Peter Konki katika Mahojiano na Startv kuhusu maana ya PASAKA kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba alisema,

“Mtu haheshimiwi kwa Matusi ila kwa Hekima”, ambapo katika Maoni viongozi wa Dini waliyotoa walisema, wangependa kuonaKufa na Kufufuka kwa Yesu kunalifufua Bunge hilo litoke katika Uovu wa Mtusi na badala yake liwe na Hekima.

Mbali ya ushauri mwingi uliotolewa na Viongozi hao pia walisema, wanachoona Wajumbe hao wanagombea Fito, na wanachojadili ni Rasimu tu siyo Katiba, ambayo mwisho wa yote wananchi ndiyo watakaamua kwa kupiga kura ya maoni.

Pengine ni vizuri Polisi na watawala kuelewa, kuwasambaratisha UKAWA si kufanikisha  azima ya mfumo wa serikali mbili inayotakiwa na serikali, tofauti na serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba iliyokusanya maoni ya watu nchini kutaka serikali tatu.

Hivi karibuni UKAWA walifanya uamuzi wa kususia Bunge Maalum la Katiba kutoka ndani ya Bunge kwa madai ya kuchoshwa kusikiliza matusi, ubaguzi na kauli za chuki zinazotolewa na wajumbe kutoka CCM bila viongozi wakubwa kukemea.

Kama vile Nyakati za Yesu  Viongozi walivyoshindwa kuwakemea watawala waa misri kuwatesa wana wa Israel wasiende nchi ya asali na maziwa na 
badala yake waendelee na mateso, Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Kutoka 1:12a.

“Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali”.Kutoka 1:13-14.

Kosa la Farao, lilisababisha Yoshua kuongoza Mapambano yaliyoangusha Kuta za Yeriko kwa kuimba huku wakizunguka Ngome ya Mji huo mara Saba;  Hivyo sioni haja ya Serikali na Polisi kuwafanya Ukawa wanachokiamini wakati watu wanaotegemewa wanamwaga matusi na kejeli zisizo na uadilifu bungeni.

Matusi ya bungeni yanailaani nchi yetu hata Mungu hawezi kufurahishwa kuona inalaaniwa badala ya Baraka alizoiwekea ikiwa ni pamoja na watu wake; Nilitegemea kuona Watawala hasa aliyewateua Wajumbe hao wa Katiba, anawawajibisha wanaotoa matusi, ili nchi ioshwe na kuwa safi.

Ni wakati muafaka wajumbe wa Katiba wajitazame kwa mfano huu; Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.

Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;  bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.

 


No comments: