Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, April 27, 2014

Mh. Mwigulu Nchemba aacha sherehe za muungano na kwenda kufunguwa tawi la CCM wanawake DMV

    Huku akiendelea kutafuna pesa za masikini walipa kodi jijini Wshington D. C. , Mh. Nchemba ameacha sherehe za muungano ambazo kilele chake kilikuwa leo Jumapili April 27, 2014 kwa mpambano kati ya Zanzibar vs Tanganyika na kwenda kufungua tawi la wanawake District of Columbia, Maryland na Virginia (DMV).

         Mshangao mkubwa ulikuwa ni pale ambapo Mh. Mwigulu alikuwa amealikwa kama mgeni rasmi ambaye alipaswa kutoa kombe kwa mshindi na medali kwa timu zote mbili. Mwigulu alikuwepo tang mechi inaanza na alifanya ukaguzi wa team zote mbili. Alikuwepo pia wakati kipindi cha pili kinapo anza, lakini haikujulikana alitoweka muda gani. Kwa kutawaliwa na uchama na kuweka utaifa pembeni, aliwaacha balozi Mulamula na waTanzania solemba uwanjani huku akikimbilia shughuri za chama. Ilibidi Balozi na afisa mwingine watoe medali kwa wachezaji badala ya Mwigulu aliye uacha utaifa hapo uwanjani na kukimbilia uchama

      Wachezaji na waTanzania wengi wameonyesha masikitiko ya kuachwa mataa na kiongozi huyu hapo uwanjani bila kujua hatima ya kukabidhi kombe na medali. Wengi ya waTanzania hapa DMV wamekuwa wakihoji kuwa huyu jamaa, Mwigulu, ujio wake hapa USA ulikuwa muariko wa kufunguwa tawi la wanawake DMV au sherehe za muungano. Kwa bahati mbaya maafisa ubalozi walio ulizwa swali hili walimung'unya maneno na swali lilienda bila jibu.


Swali ambalo halina jibu hadi hivi sasa kwa wana DMV: Ujio wa Mh. Mwigulu DMV, USA ulikuwa kufungua tawi la CCM wanawake au sherehe za muungano?

WE REPORT, YOU DECIDE

No comments: