Na Bryceson Mathias
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinafanya usafi kwenye nyumba yake, ilai kimepata Jalala la kuweka takataka kinazofagia kwa sababu wakazi wa Jalala hilo, wameaminishwa na viongozi wao, eti takataka hizo zinaweza kuwasaidia kuziba Mashimo.
Usafi huo ndio uliomfanya Katibu Mkuu wa (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, aseme kama yupo Mbunge au Diwani wao anataka kuondoka CHADEMA, milango iko wazi, kwa sababu hawawezi kumvumilia kiongozi au Mwanachama msaliti.
Uwajibikaji, Usafi, Uadilifu, Uwazi na Haki ndani ya Chadema, si kitu cha Hiari bali ni lazima tangu, Mtarajiwa, Mkereketwa, Mpenzi, Mfuasi na Mwananachama, lazima awe navyo ili kuwakomboa watanzania waliovikwa minyoro ya Ufisadi na wizi wa rasimali za Taifa.
Mwanachama Mkongwe wa Miaka ya 1954 aliyeomba asitajwe alidiriki kusema, ‘Kama Chadema kisingekuwepo kukemea uchafu wa Rushwa na Ufisadi uliopo nchini kwa maandamano, nchi ingebaki mashimo, Rasilimali na Wanyama, vingebaki Miiba na Mifupa ya Mizoga’.
Alisema, Hakutegemea aone Chama cha Siasa kinachosajiliwa kikiwa na Nembo ya Nyota au Msalaba, kwa sababu ni Alama ya Taasisi za Dini na zinazofanana na hizo [Msalaba Mwekundu], hivyo kikiwepo Chama cha Siasa cha namna hiyo, kinaashiria ni cha Udini.
Nadhani Kauli ya Dk. Slaa inakwenda mbali, kwamba, wanaotaka kueneza Utakataka na Usaliti kupitia kueneza Udini, Ukabila, Ubinafsi, Upeke pekee, unaoendelea kuwanyonya na kuwafunga tena Nyororo Watanzania kama enzi za Utumwa, Waondoke Chadema.
Upeke pekee huo, unatuthibitishia kuwa watu wa namna hiyo wamekula vya watu, hivyo lazima walipe fadhira ya kula vya watu, na kwa Chadema hizo ni Takataka lazima zitupwe jalalani, ili kama kuna watoto wa mitaani, wakaokote huko Masalia.
Katika Ziara ya M4C–Operesheni Pamoja Daima [OPD] nchini, ambapo mbali ya kudai kuwepo kwa Uboreshaji wa Daftari kura ili kizazi cha Vijana takribani Mil. Nne kisichojiandikisha kijiandikishe ili kipate haki ya kupiga kura, iliwaamusha wazee na vijana usingizini!.
Miongoni mwa wananchi walisikizishwa kuwa, Uwajibikaji, Usafi, Uadilifu, Uwazi na Haki ni Mapambo, kama Rushwa na Ufisadi dhidi yao, hawajui kama wachache miongoni mwao wamelambishwa Asali ya Kanga, Kofia, Skafu na Pilau, wamegundua Mboga ni Muhimu maishani mwao.
Wamebaini, Ndani ya Chadema, Uwajibikaji, Usafi, Uadilifu, Uwazi na Haki ni sabuni ya kutolea Uchafu, na kujiletea Mustakabali wa Taifa hili, tofauti na pengine ambapo, japo sabuni hizo zipo, watu hawana usafi, ni kama Jalala la takataka.
Katika Misikiti na Makanisa tutashangaa tukiona Viongozi wake wanakataza waumini wao, wasinywe Pombe, Wasizini, Wasiue, Wasitukane na mambo yanayofanana na hayo, huku wao wakiyafany hadharani.
Lakini Waasisi wa baadhi ya Vyama takataka, vinavyojiita vinajali watanzania, na havitaki maandamano na vina Umoja wa Mabadiliko na Uwazi, viongozi wake licha ya kwenda kuhiji nje ya nchi na kutubu, tunashuhudia wakitukana watu, na kuonesha hawana Usafi, wapo jalalani.
Viongozi wa namna hii, ni wale ambao, Wananchi au Walimu wakidai haki kwa maandamano, wanapigwa Mabomu na kumwagiwa Maji ya Pilipili wakiwapa Ulemavu wa Maishi kama si VIfo; ila Wabunge wakidai Posho, Wanalindwa na Farasi na Mbwa wadai vizuri Kodi yetu bila Bughudha.
Mtumba ni Nguo nzuri, lakini haina Hadhi!! Kama hivyo ndivyo, basi watu tunaibiwa kweupe!
No comments:
Post a Comment