Na Bryceson Mathias
KUNA wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamekuwa wakitumia muda wetu vibaya kupigana vijembe dhidi ya wajumbe wenzao (bila kuwataja majina), kuwa Tanzania ina majasiri wengi na wengine walishafariki dunia, badala ya kujadili mustakabali wa nchi yetu.
Nimeshawishika kuandika udhaifu na ulegevu huo wa watu wanaoitwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kushindwa kujadili mambo ya maana na kuanza kujadili waliofariki wakati maandiko [Biblia] inasema, “Nifuate; waache wafu wazike wafu wao” Mathayo 8:22b.
Kama Mwingine katika wanafunzi wake Yesu alimwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu, aliambiwa, ‘Nifuate; waache wafu wazike wafu wao’, Katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba nashindwa kuwaelewa wajumbe kwa nini wanafanya mambo ya utoto.
Niliteegemea niona wajumbe wanajdili kuonesha ujasiri wa kuboresha Katiba ili ikomeshe Ubakaji wa watoto wadogo uliomo miongomi wa jamii ya wajumbe hao, ikomeshe Ujangili wa rasimali ya taifa,ikomeshe rushwa na Ufisadi uliokidhiri kiasi cha wao kutaka Posho kubwa.
Nilitarajia nione wajumbe wakijadili vitu vilivyohai vitakavyokisaidia kizazi hiki na kinachokuja kwa sababu na wasijisahau kiasi kwamba hawajui wanachojadili kwenye Bunge hilo kitawafaidisha au kuwaumiza wao, watoto na ndugu zao waliopo, na watakaokuja siku zijazo.
Ukabila haubadiliki, labda mtu ana upungufu wa akili sawa na mtu anayewakaa wazazi wake waliomzaa! Nini ninachotaka kusema, Misimamo ya Dini na Itikadi, inaweza kubadilika, mtu anaweza akawa Mkristo Kesho akawa Mu-Islam, Mtu akawa CCM kesho akawa Chadema au CUF na kadharika.
Hivyo wajumbe wa Bunge la Maalum la Katiba, waelewe kwamba, wakitunga Sheria Mbovu, kama alilenga Iuumize Ukristo au Mu-Islamu, kesho ndugu yake, Mwanae au yeye mwenyewe, atakuwa Mkristo au Mu-Islam, Katiba hiyo itamuuiza au kumsaidia.
Nilitegemea nione, itakapofika katika muda wa Bunge Maalumu la Katiba, wajumbe wanakuwa makini na watashindana kwa hoja kwa faida ya nchi, si Misimamo duni ya Vyama, Itikadi au Udini.
Nilitegemea kuwaona watu makini ambao Rais Jakaya Kikwete amewachagua kwa ajili ya kutetea maslahi ya nchi, wanaweka historia itakayothaminiwa na kukumbukwa na Vizazi akiwemo aliyewateua.
Sikutegemea kuwaona wajumbe badala ya kujadili mambo ya msingi wanageuka na kuacha hoja muhimu pembeni na kugeukia kujadili posho, huku wakipigana vijembe vya nani Jasiri, badala ya kufikiria kukomesha Ubakaji wa watoto wadogo na Ujangili uliokithiri nchini..
Ninachosikitika ni kuona kuwa, kuna kila dalili za mashaka tunaweza kutumia fedha nyingi za nchi [Kodi ya wananchi], bila kufikia lengo lililokusudiwa, huku wateuliwa wakitoka Dodoma wamevimbiana kwa afya, lakini wananchi wao wamekonda!
Kama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanaweza wakang’ang’ania kujadili Posho kwa nguvu kama Luba, basi agharabu wanaweza hata kuiwekwa nchi rehani kwa ajili ya kupata fedha kibindoni.
Katika aibu hii; Rais Kikwete Kikwete, aliyewateua, anaweza kuwaondoa katika Bunge la Katiba wale ambao wameonekana wazi kuwa wapo Dodoma kwa ajili ya Maslahi ya posho na si kujadili rasimu ya katiba inayoelekea kutupatia katiba mpya kwa faida ya wananchi.
Maoni ya watu waliowengi nje ya Bunge la Katiba kila mmoja anaonyesha kukerwa na wateule wa rais kwa ajili ya kuacha kujadili mambo ya msingi na kujadili Maslahi yao, wanadai wangeweza kuandamana kupinga hatua hiyo lakini watapigwa Mabomu.
Mbali ya Mabomu wanadai, watapigwa Virungu na kumwagiwa maji ya kuwasha, ingawa wao wanalindwa na Farasi na Mbwa ili waendelee kuchezea na
kuhujuma Kodi ya Manati wanayokatwa katika maisha magumu waliyonayo.
No comments:
Post a Comment