Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, March 11, 2014

Kalenga Msikosee; Tagamenda ni tupa T-sheti, Kanga na Skafu:

Na Bryceson Mathias

WENYEJI wa Mkoa wa Iringa, Njombe na Mikoa ya Jirani kama mimi, wanaelewa vizuri sana maana ya kijiji cha Tagamenda kuwa ni ‘Tupa Nguo’. Lakina nguo ninazotaka wana Kalenga watupe, ni T-Sheti, Kanga Skafu na Hongo za Madebe ya Pombe katika Uchaguzi wa 16.3.2014.

Lakini pili ninachotaka wana Kalenga wasitupe, ni Shahada ambapo Thamani yake ni kubwa kuliko Sh. 15,000/-, Debe la Pombe au Mfuko wa Mbolea wanaopewa ili wabadilishane na Almasi hiyo, ambayo kimsingi Shahada ni Shule, Zahanati, Barabara, Maji na ni Dawa.

Mtu hatupi Nguo kama hazijachakaa! Najua mmepewa T-sheti, Kanga na Skafu ambazo hazijachakaa, nikisema uzitupe huku ni mpya hutanielewa; ila nataka ufunguke kuwa Nguo hizo ni Chakavu na Chafu, maana zinawapumbaza msihoji Zahanati, Dawa, Shule, Barabara na Maji.

Nasema Nguoa hizo ikiwemo Pombe zimechakaa, hasa kutokana na kwamba zimechakachuliwa kwenye Kodi yenu, ili mkivaa, msiulize Zahanati, Dawa, Shule, Barabara, Maji na Maendeleo mengine muhimu katika eneo lako. 

Hii ina maana gani, kama kwenye Vijiji vya Kalenga hakuna Miundo mbinu hiyo, muelewe kuwa fedha iliyotakiwa iwape maendeleo na vitu hivyo muhimu ikiwemo mbolea, imo kwenye Kofia, Kanga, T-Sheti na Pombe mnayopewa.

Pengine ni vema mkawauliza wanaowapa Kanga, Kofia, T-Sheti, Skafu na Pombe hizo leo, Je walikuwa wapi kuwapa tangu zamani? Kwa nini gharama iliyotumika kuwanunulia Nguo hizo isitumike kuwapa Maji, Barabara, Shule, Zahanati, Dawa na Mbolea kabla ya Uchaguzi?

Waulizeni tena; Mtakula Kofia? Mtakunywa T-Sheti? Mtatibiwa na Pombe? Mtasafirisha Mazao kwenye Skafu? Mtasoma Maandishi ya Kanga badla ya Elimu? Kumbukeni Waswahili wanasema wajinga ndio waliwao.

Kama Mtu anakuja kukuletea msaada wakati Shida imeshaisha; Je mtu huyo ana nia njema ya kukusaidia? Kama mtu anawaletea Mbolea wakati mahindi yameharibika! Ni dhahiri hawatakii mema, na wala hana nia njema na ninyi.

Kimsingi mtu anayemchangia fedha nyingi maiti wakati wa mazishi badala kumsaidia wakati anaumwa ili kuokoa uhai wake; Hafai! Kama ukimfuatilia kwa makini inawezekana ni mmoja wa wachawi  au wabaya wako.

Kama Vocha za Mbolea na Pembejeo zenu zinachakachuliwa na Viongozi hao hao wanaowapatia Nguo hizo zilizochakaa na kunuka Rushwa na Ufisadi; watashindwaje kuwachachua wana Kalenga?

Wananchi wa Kalenga kumbukeni kuwa, Kodi yenu ya Nyanya, Viazi, Mahindi, Vitunguu, Maharage, Alizeti, Njegere, Mbaazi, Matunda, Mboga Mboga na Mazao mengine, ndizo zinazotengeneza T-Sheti, Kanga, Skafu na Kofia tena kwa bei ndogo ila taarifa ni Mamilioni.

Ni rai yangu kwa Wapiga kura wa Kalenga wafahamu kwamba, kuchezea Shahada ya Kura, ni sawa na kuchezea uhai wao kama mtu anayekudanganywa unywe sumu kwa maana ya kuionja kama Mboga.

Sumu si Mboga au Pombe ikaonjwa; ukionja sumu ni hakika utakufa; hivyo kuchezea kura ni sawa na kuchezea Shilingi Chooni, ikitumbukia huwezi kuiokota na kuichukua maana adha yake ni kubwa kutokana na shimo kuwa refu.

Kama Mwanamke hapigwi Mangumi ila anapigwa kwa Idadi ya Matoleo ya Kanga na Vitenge! Ni wakati muafaka kwa wapiga Kura wa Kalenga, kukataa udanganyifu wa kupigwa kwa Kanga, Skafu, Kofia na Pombe, bali wafanye mabadiliko ya kukataa vipigo hivyo, na hivyo kudai Vipigo vya Maendeleo. Usitishwe kapiga kura.

1 comment:

Anonymous said...

Mimi binafsi naunga mkono hoja hiyo ya msingi, hivi hiyo si rushwa je, u na hakuna serikali? ila ni kweli, mtu huwezi kulikata tawi ulokalia!!!!!!
wananchi wa kalenga tumia busara, najua ccm wananguvu, na wana fedha nyingi kuwaonga nyote ila hawafikiriii kuboresha maisha ya wanakalenga, msiwe viziwi fungukeni tazama mbele!!!!!