- Mbowe asema wajibu wake uko kwa Watanzania si CCM
- Chenge amgeuka, Lowassa asifia kasi na viwango vyake
SIKU moja baada ya mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa bunge hilo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka atambue wajibu wake kwa Watanzania na si kwa Chama chake Cha Mapinduzi (CCM).
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi mgombea wao, Grace Tendega uliofanyika kwa nyakati tofauti katika vijiji vya kata za Ifunda, Lyamugungwe, Magulilwa na Luhota.
“CHADEMA inamtakia kila la heri Sitta kwa nafasi hiyo nyeti aliyoipata, lakini kinamtahadhalisha kutambua wajibu wake kuwa upo kwa Watanzania ambao ni wengi wanaofuatilia mwenendo wa mchakato huo bungeni na si kwa chama chake,” alisema Mbowe.
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment