Na Bryceson Mathias
IMEDAIWA Chama cha Siasa cha Alliance for Change and Transparency–Tanzania (ACT), kimeanza kujipenyeza mkoani Morogoro na wilaya zake, ambapo Viongozi na Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliofukuzwa kwa tuhuma za kukihujumu, wameanza kujiunga nacho kwa siri.
ACT kilichopata Usajili wa muda hivi karibuni, ambapo Viongozi waliodaiwa kuitwa MM, M2 na M3 kugundulika na Interejensia ya Chadema, wafuasi wao waliojificha, wameanza kujionesha, na inawezekana walio nje ya Vyama vingine nao wakaanza kujiunga.
Viongozi hao ni pamoja na wale waliojiunga na CCM, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi, Tanzania Labour Party (TLP), ambao kutokana na maandalizi ya Uongozi wa ACT mikoani na wilayani, watalazimika kuvihama tena vyama hivyo ili kuwania uongozi.
Mmoja wa Viongozi wa Chadema aliyegoma kushawishika alisema, baada ya Usajili wa muda wa ACT, baadhi ya vinara wa chama hicho ambao majina yao hayamo kwenye usajili wa Chama hicho alidai, ACT wamefika mkoani na kujipenyeza Chadema ili kuanza ushawishi.
“Siyo siri, ni kweli ACT wamefika mkoani morogoro na Wilaya zake, na hivi sasa wameanza kujipenyeza miongoni mwa wananchama na Viongozi wa Chadema Usaliti, wakiwataka wajiandikishe Uanachama ili kukifanya kipate usajili wa Kudumu”.kilisema Chanzo.
Hata hivyo chanzo kilisema, Chama hicho kina nafasi kubwa ya kujichanganya kikafa na kushindwa mbinu ya kukiua Chadema, kutokana na kwamba baadhi ya wasaliti tayari walishajiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivyo watalazimika kukihama tena chama hicho.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa, kitendo hicho kitawafanya wasiaminike na Jamii kutokana na kutangatanga kwao, ambapo wale walioshikilia madaraka kwa sasa ndani ya ACT, hawatakubali baadaye waje wang’olewe na watu waliokuwa vyama vingine wakiogopa kujitokeza hadharani.
Waasi wakuu wa Chadema takribani 14 ambao hawamo ACT kwa sasa, nao wametajwa kuwa walikuwa viongozi wa Ngazi za kitaifa ndani ya Chadema Taifa, wakiwemo waliokuwa kwenye Baraza la Vijana (BAVICHA).
Wale waliochomekwa uongozi, tayari wameanza kupewa bendera na Katiba ya Chama hicho ili vianze kutumika, huku bendera hizo zikitakiwa zipeperushw mara moja mikoani na wilayani kuanzia Vitongoji, Vijiji, Kata na Tarafa, lakini viongozi hao baadhi yao wanasita.
Mtoa habari huyo alipoulizwa iwapo na yeye ni miongoni mwa wasaliti ambao wameshawishiwa na hivyo kutaka kuhamia ACT alidai, “Tumekuwa tukitumainishwa na Viongozi wanafiki, kuwa Chadema kina Udini, Ukabila, Ukanda na Umajimbo; lakini Nembo ya bendera niliyoiona ndiyo inayoakisi hayo.
“Sipo tayari kujiunga na ACT; Unaweza kubadili dini ukawa Mkristo au Mu-Islamu, na unaweza kubadili Chama ukawa leo CUF kesho NCCR Mageuzi, lakini huwezi kubadili kabila lako. Mimi ni Kabila la Chadema siwezi kuwa kabila la ACT”.alitoa kabehi mtoa habari.
Mtoa habari huyo alionya kwamba; Enzi ya Babu wa Loliondo, wananchi wengi walidanganywa hata wagonjwa walitolewa Ma-Hospitalini tena kwa vibali vya Madaktari wa Serikali na Viongozi wa Serikali yenyewe! Pamoja na Viongozi wake kunywa Kikombe na kukisifu, walikataa kuipitisha kuwa ni dawa halisi.
Hivyo, sipo tayari kujitumainisha kujiunga na ATC ambacho kina jina lakini wanasiasa wanaojiunga humo ni wale walioasi kwenye vyama vyao; Ugonjwa wasaliti wa Chadema, wataufanya huo huo watakapokuwa ACT, kwa hiyo SIDANGANYIKI!.
Hata hivyo mtoa habari huyo mwisho aligusia waliokuwa wana CCJ pia wamo kwenye ATC
No comments:
Post a Comment