Na Bryceson Mathias,
Mvomero
KAMATI ya Utendaji ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Mvomero, imedaiwa kumvua
Uongozi Katibu wa Wilaya wa Chama hicho hicho wilayani humo, Mrisho Ramadhani,
kwa madai ya kukisaliti Chama.
Habari toka ndani ya kikao
cha siri kilichoketi Ofisi ya Wilaya zinadai, Kamati ilimvua ukatibu
Mrisho kutokana na kufanya maamuzi ya kukiunganisha Chadema na Vyama vingine
bila ridhaa ya Chama, na kumdharilisha Diwani wake, Luka Mwakambaya.
Akizungumza na gazeti hili
kwa masharti ya kutotajwa jina Mtoa habari wetu alisema, Mrisho amebakiwa na
Ukatibu Mwenezi wa Wilaya, amabapo suala lake limepelekwa kwenye Mkutano Mkuu
akajadiliwe na kutolewa maamuzi.
“Baada ya Chadema
kutangaza kufanya mkutano wa M4C–Opresheni ya Pamaoja Daiama (OPD) Kata ya
Mtibwa 29.1.2014, Mrisho aliacha Sera za Chadema za kutatua kero za wakulima na
wafanyakazi zilizofanywa na Mwakambaya na kuungana na wanaokwamisha OPD.
“Kama haitoshi, 29.1.2013,
alimdharilisha Diwani wa Kata ya Mtibwa, Mwakambaya (Chadema) katika Mkutano
hadhara, akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe, aliyetaka aelewe
Kero za Mwekezaji wa Mtibwa aende nazo bungeni”.alisema mtoa habari.
Katika Mkutano huo Mrisho
alisema, ‘kutokana na kero za mwekezaji wa Mtibwa kukithiri akiwacheleweshea
malipo Wakulima wa wadogo wa miwa na wafanyakazi, Chadema kimeungana na Vyama
vingine kudai haki kwa maandamano baada ya Diwani Mwakambaya kushindwa, jambo
ambalo halikuwa kweli na lilipingwa na wananchi, kwa sababu amekuwa akilala
langoni mwa lango la mwekezaji na kulazimika kuwalipa.
Aidha baada ya gazeti hili
kumtafuta Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mvomero Saimanga Kashikashi bila
mafanikio, lilimtafuta Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Msingi Chadema, Innocent
Zawadi kutaka kujua suala hilo, naye alisema ngoja awasiliane na uongozi wa
Wilaya ya Mvomero kupata habari sahihi.
Nafasi
ya Katibu wa Wilaya ya Mvomero (Chadema) tangu uchaguzi ufanyike, imekuwa
ikipyaya na kukaimishwa kwa mara pili sasa, ambapo baada ya kikao hicho jana
imekaimishwa kwa, Rosemaary Kimune, huku wapenzi wa Chadema wakikitaka chama
kutafuta mtu makini
No comments:
Post a Comment