Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, February 25, 2014

Wabunge, Madiwani; Wanapojiuzulu bila ridhaa za wananchi! wawajibishwe?

Na Bryceson Mathias

KUMEKUWA na Vitisho kwa wanasiasa wakiwemo wabunge na hasa zaidi Madiwani, ambao wamekuwa na tabia ya kutishia au kujiuzulu na kuwaacha wapiga kura   hawana Mwakilishi. Je wabunge na madiwani hao wanapojiuzulu bila ridhaa ya wananchi; wawajibishwe?.

Pia imekuwepo tabia ya Wabunge, Madiwani na baadhi ya Ma-Meya, wakiwajibishwa na Wananchi au Vyama, kutokana na kutowajibika, Wamekuwa wakienda mahakamani kupinga, na wanasikilizwa! Je huu si wakati wa wapiga kura, nao wapinge mahakamani kuachwa Solemba?

Chaguzi za Serikali za Mitaa hivi karibuni, ukiwemo Uenyekiti wa Vitongoji, Vijiji, Kata na Udiwani, baadhi zimetokana na Vongozi hao kuamua kujiuzulu, ambapo wamesababisha usumbufu kwa wapiga kura, Gharama na kupotea kwa Muda. Je kwa nini wahusika wasifidie gharama?

Iwapo Katiba itatoa ufafanuzi wa kifungu cha kuwawajibishe wabunge wanaposhindwa kuwaridhisha wapiga kura wao, kifungu hicho kiende mbali kiwahusishe Viongozi wote wa kisiasa na Serikali, kuwafanya waogope, ukizingatia baadhi hupata Mirungula wa Kitu kidogo.

Mfano; Hivi karibuni Madiwani 14 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mbeya walitishia kujivua nyadhifa zao kwa madai kuwa Serikali Kuu imekuwa ikiwafanyia vitendo vya ubabaishaji. 

Malalamiko waliyotaja na baadhi ya vitendo hivyo ni vya kweli, likiwemo dai la kuwaletea watumishi wasiokuwa na viwango katika halmashauri kinyume cha utaratibu! Lakini kwa maana ya wananchi kukosa wawakilishi kwa kipindi hicho, ni adha kwa umma.

Mgogoro mwingine ni ule wa ardhi eneo la Loliondo, Ngorongoro, Arusha, ulioshika kasi kiasi cha Mbunge wa Ngorongoro, Saning’o Ole Telele na madiwani wilayani humo kutishia kuachia ngazi ikiwa Serikali itaendelea na msimamo wa kumega kilometa za mraba 1,500 za eneo hilo.

Hapa ndipo ninaposema, kama wananchi ndio waliotoa Kodi zikafanikisha Chaguzi hizo, halafu ghafla Kiongozi huyo anasababisha kufujwa fedha ili kufanyika uchaguzi mpya kwa gharama zingine! Nashauri gharama za uchaguzi zibebwe na wahusika.

Tumekuwa tukipate upekuzi kuwa, baadhi ya viongozi hao huingia kujiuzulu nyadhifa zao kwa sababu ya njaa, lengo likiwa ni kuvikomoa vyama fulani, kwa faida za Mtu binafsi aliyemwaga fedha kwa uroho wa madaraka.

Mtindo huo ukiachwa uendelee bila uthibiti, ili Bumu letu la Kiuchumi ambalo badala ya kufanyia vitu vyenye maana kwa Taifa, kama Kujenga Shule, Maji, Maabara na Zahanati, zinachezewa na Mchwa kiholela.

Wabunge wanaowajibishwa kwa makosa ya uzembe katika vyama vyao na kukimbilia mahakamani kupinga adhabu zao wakasikilizwa. Ifika mahali sasa, hata Wabunge, Madiwani na viongozi wanaojiuzuli bila ridhaa ya wananchi, wapingwe mahakamani na Mahakama ziwasikilize pia.

Nilitegemea; Viongozi Wabunge, Madiwani na Viongozi wengine wa Vyama na Serikali, kabla hawajafanya maamuzi yao ya kujiuzulu au kuacha nyadhifa na nafasi zao, wawasiliane na wananchi waliowachagua, ili waombe ridhaa kwao wakubali au wakatae.

Waswahili wanasema Mkuki kwa Nguruwe, kwa binadamu uchungu; kama hivyo ndivyo, basi na iwe, ‘Mkuki kwa Binadamu na kwa Nguruwe usiwe Uchungu! Kama hilo kwao  haliwezekani, basi wasitake kuwasumbua na kuwakera wananchi kwa vijisalio vyao.

Ifike mahali sasa, Viongozi wanaofanya hayo, ikiwemo kuwashawishi na kuwarubuni kwa makusudi, kwa kutokuelewa au kwa shinikizo la vijisenti, wasidhani wanavikomoa vyama pinzani au mahasimu wao, bali waelewe wananchi na kodi yao ndiyo inayoteketea, huku Serikali ikidharauliwa wakiwemo viongozi wake.

No comments: