Mjumbe wa Bunge
Maalum la Katiba, John Mnyika (pichani), amemtaka Mwenyekiti wa muda wa Bunge
hilo, Ameir Pandu Kificho, kuwasilisha taarifa ya kazi zilizofanywa na kamati
ya kufuatilia posho na kanuni ili iwe wazi kwa wajumbe na jamii. Kadhalika,
alisema usiri, udhaifu na uzushi uondolewe mjadala ni Katiba mpya na siyo
posho.
Katika taarifa yake, alisema usiri na udhaifu wa uongozi wa Bunge
katika kutoa taarifa na uzushi wa baadhi ya viongozi au watendaji wa serikali
na baadhi ya wajumbe umesababisha majalada wa Rasimu ya Katiba kubadilika na
kuwa posho.
Alisema ili kulirudisha Bunge Maalum katika mkondo sahihi kwa
kujadili kanuni na rasimu ni vyema Katibu wa Bunge na Baraza la Wawakilishi
watoe taarifa ya ziada ya kazi ambazo kamati za muda za uongozi na kanuni za
kumshauri zimefanya.
“Makatibu wasipofanya hivyo, Mwenyekiti wa muda, Pandu
Ameir Kificho, atumie ufunguzi wa semina ya kanuni za Bunge kueleza kazi kubwa
iliyofanywa na namna ambavyo kwa ukubwa wa kazi muda umeongezwa na muda wa
ziada wa kuwasilisha kanuni zilizofanyiwa marekebisho,” alisema.
Kitomory S./ Ippmedia-Nipashe
No comments:
Post a Comment