Leo kuna kikao
kinaendelea katika Hoteli ya White Sands , ambacho KIMEANDALIWA na TCD ,
ambacho kimepewa jina la "Mkutano wa Tafakuri na Maridhiano kuelekea
Katiba Mpya" ambacho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,
Bunge na Vyama vya Siasa , Viongozi wa Dini, wabunge wapya wa Bunge la Katiba
na Tume ya Mabadiliko ya Katiba .
Baadhi ya
Viongozi wa Kitaifa waliohudhuria ni pamoja na Dr.Gharib Bilal, Mizengo Pinda,
Anne Makinda, Pandu Kificho,Joseph Warioba,Pius Msekwa, Philip Mangula,Freeman
Mbowe, Dr.Wilbroad Slaa, Prof.Lipumba, James Mbatia,Stephen Wassira, Asha Rose
Migiro,Mathias Chikawe, Askofu Mokiwa, Amir Kundecha,Butiku na wengineo wengi
wa aina hiyo.
Katika kikao
hicho aliyetegemewa kufanya hotuba yaUfunguzi ni Rais Kikwete, ila badala yake
alimtuma Bilal kumwakilisha, ndipo katika hotuba yake ya ufunguzi
alipoishambulia tume ya Warioba na kuweka msimamo kama ifuatavyo;
1.Kuwa tume
haikutumwa kwenda kuandaa rasimu itakayopendekeza uwepo wa serikali tatu ,
hivyo hayo ni mambo ambayo tume ilijitungia yenyewe , na hivyo Bunge la katiba
litaenda kufanya uamuzi kwa misingi ya KURA .....na kila mmoja ajiandae kupokea
maamuzi ya kura , hata kama yataenda kinyume na mawazo ya tume ya Warioba .
2.Wao
hawakutumwa kwenda kupunguza mambo ya Muungano bali ni kwenda kuyaongeza kama
vile suala la Afya, Elimu yalipaswa kuongezwa kwenye rasimu hiyo , ila tume
imeenda kuyapunguza , hivyo wanatishia uhai wa Muungano na hivyo ni mawazo
ambayo hayapaswi kuungwa mkono na mtu yeyote mwenye akili timamu.
3. Kongamano ,
limeandaliwa kwa lengo la kupigia debe mawazo ya wakina Warioba ambao ni
kikundi kidogo katika jamii na ambao hawawakilishi mawazo ya wengi.
Baada ya maneno
hayo na mengine mengi alifungua mkutano , na akitaka kuondoka ila aliombwa
anakiri ili aupate majibu kutoka tume na ili asiwe wa kwenda kuambiwa nini
kimesemwa , ndipo Warioba alipomuoa kumjibu kwa hoja na vielelezo vya kutosha
kuhusu walivyoweza kufikia kwenye HITIMISHO la kuwepo kwa Serikali tatu.
Majibu ya
Warioba yalikuwa kama ifuatavyo;
1.Wao
walichofanya ni kukusanya maoni ya wananchi na kuyachambua , na hivyo
kutengeneza rasimu kutokana na maoni yao na sio kuwa walijifungia na kuanza
kuandika maoni yao binafsi.
2.Wananchi
ambao walipendekeza muundo wa Muungano ni kuwa 4% walisema Muungano usiwepo,
13% walisema uwe wa serikali moja , 22% walisema Muungano wa serikali mbili na
61% walisema kuwa Muungano uwe wa serikali tatu, hivyo kiongozi kusema kuwa
tume imejitungia ni kutokujipa muda wa kutazama video na nyaraka mbalimbali
walizopewa kama vielelezo vya maoni ya wananchi.
3. Kuwa
serikali ya Muungano , imejivika koti la Muungano wakati ikiwa inajishughulisha
zaidi na mambo ya Tanganyika , ndio maana Waziri Mkuu hajawahi kwenda Zanzibar
kufanya shughuli za kimaendeleo wala kukagua miradi ya maendeleo huo , kwani
anajiona yeye ni wa Tanganyika, pia alisema kuwa ukitazama Bunge la Muungano ,
maswali asilimia 90 yanayoulizwa ni kuhusu mambo ya Tanganyika , kuliko ya
Muungano, bajeti ya Muungano asilimia 80 inashughulika na mamb ya Tanganyika
kuliko mambo ya Muungano, ndio maana hakuna pesa inatengwa kwa ajili ya
maendeleo ya zanzibar , hakuna mtu anajiuliza Zanzibar utapata wapi fedha za
kujiendesha nk.
4.Zanzibar ni
nchi na katiba yao imepuuza kabisa uwepo wa serikali ya Muungano , ndio maana
katiba yao inasema kuwa wao ni nchi na wana Wimbo wa taifa, bendera nk , hivyo
kuendelea kujidanganya kuwa Muungano wa serikali mbili upo ni kujivika Tabia za
mbuni...
5.Tume ili
pitia ripoti ambazo waliochukua kwenye ofisi ya makamu wa Rais kama vile ripoti
ya kamati ya Amina, Shelukindo, Kisanga nk kuhusu Muungano na kote huko kuna
malalamiko juu ya Tanganyika kujivika koti la Muungano , nashangaa hata waziri
mkuu hapa aliposema Zanzibar sio nchi mnakumbuka yaliyokumkuta huko
Bungeni.....
Pius Msekwa,
amemuunga mkono Warioba na Kumtaka Wassira ajenge hoja ni kwanini serikali
mbili ni muhimu , na sio kuishia kuwa na Mazoea kuwa tumezoea hivi , fear of
the unknown....na pia hata hati za Muungano ziliweka wazi kuwa serikali mbili
ilikuwa ni kwa interim period only.....sasa je ? Tuendelee kuwa kweye hai hyo
baada ya miaka50
Hayo ni ni
baadhi ya mambo yalivyo kuwa kwenye kikao na bado kikao kinaendelea .
No comments:
Post a Comment