CHADEMA: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) itakutana kwa ajili ya kikao cha dharura, Februari 14,
mwaka huu, jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Kamati Kuu
itajadili na kufanya uteuzi wa mwisho wa jina la mgombea ubunge wa CHADEMA
katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa, unaotarajiwa
kufanyika Machi 16, mwaka huu.
Kikao hicho kitafanya uteuzi wa
mwisho, baada ya mchakato wa ndani wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la
Kalenga kwa tiketi ya CHADEMA, kuwa umepitia hatua za awali, ambazo ni pamoja
na watu wote wenye nia ya kugombea, kuchukua fomu za uteuzi wa ndani tangu
Februari 5-10, mwaka huu.
Kama ilivyoelezwa kwa umma kupitia
vyombo vya habari, Februari 6, mwaka huu, fomu hizo zilitolewa katika maeneo
matatu, Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam, Ofisi za Jimbo la Kalenga
na kwenye tovuti ya chama, ambayo ni; www.chadema.or.tz. Jumla ya watu 16 waliweza kuchukua
fomu za kuwania uteuzi huo, ambapo hadi siku ya mwisho, watu 13 waliweza
kurejesha fomu zao na kupita kwenye mchakato wa kura za maoni, zilizofanyika
Februari 12, mwaka huu.
Imetolewa leo Februari 13, 2014,
Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA
No comments:
Post a Comment