MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kalenga
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Tendega, jana
amechukua fomu ya kuwania kiti hicho huku msafara wake ukizuiliwa na polisi
mkoani hapa kwa madai kuwa haukuwa na kibali cha kuandamana na kumshikilia
Diwani wa Kata ya Mivinjeni, Frank Nyalusi.
Msafara huo ulipokewa maeneo ya
Igumbiro, kilometa nane kutoka Iringa mjini ukiwa unasindikizwa na pikipiki
zaidi ya 50 na magari ya M4C zaidi ya manne na magari mengine madogo sita na
kusababisha msafara huo kusimama zaidi ya saa moja baada ya polisi kuuzuia
katika Mlima Ipogoro.
Maofisa wa polisi waliofika kuzuia
masfara huo walisema wasingeweza kuuruhusu kupita katikati ya mji kwa madai
kuwa maandamano hayo ni batili, hali iliyoibua malumbano kati ya uongozi
wa polisi na CHADEMA mkoani hapa.
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment