WABUNGE wa kuchaguliwa ambao pia ni wajumbe wabunge maalumu la Katiba watapimwa na watanzania kama kwelini wazalendo kwa nchi yao au ni wazalendo kwa vyama vyao. Watapimwa jinsi watakavyokuwa wanachangia ibarambalimbali za rasimu, rasimu ambayo inakwenda kuwa katibaya nchi (sheria mama).
Watanzania wa maeneo wanapotoka wabunge watapimwa Je,anafaa kurudi bungeni 2015? Kama kweli wabunge wa kuchaguliwa wanaupenda ubungewao wanatakiwa wachangie michango yao kama watanzania,siyo kama wabunge wa kutoka chama fulani.
“Wabunge mnatakiwa kuingia kwenye bunge maalumu lakatiba mkijua mnawakilisha watanzania million 47, siyokuwakilisha vyana vyenu vya siasa, makundi yenu, taasisi zenu, NGO’s zenu, makundi maalumu yenye malengo yanayofananaau wachawi wenzenu mliwawakilisha.
Kusema ukweli mkiingia na mawazo ya kuwakilishamakundi niliyoyataja hapo juu makundi ambayo wamewaingizahapo hamtarudi mjengoni tena 2015. Kumbukeni watanzaniawa 2005 siyo hawa wa leo 2015, kwa hiyo kuweni makini namichango yenu mnapojadili rasimu, rasimu ambayo imetokanana watanzania na ikumbukwe pia rasimu hii haikutokana naninyi wabunge wa bunge maalumu la katiba.
Mkumbuke pia baadhi yenu wabunge mlichaguliwa kwamadhumuni ya kutunga sheria na kuisimamia serikali nammeingizwa katika bunge hili na sheria siyo na watanznaia. Nikiwa na maana mmebadilisha masharti ya kombati, mashatiya kijani na blue na mkavaa nguo za jadi lakini bado ninyi niwale wale wenye asili ya kubishana hata kwa jambo dogo sana.
Kubadilisha mashati ya vyama vyenu hakubadishi mawazoyenu mnabaki wale wale. Sasa msipoacha tabia yakubishana/kuvutana hata kwa jambo la ukweli mfano: 1 + 1 = 2lakini mwingine anaweza akatokea akasema 1 + 1 = 11 halafumkaanza kubishana na baadaye mbishano/mvutano kuamuliwakwa 2/3. Ikitokea 2/3 wamekubaliana 1 + 1 = 11 maana yake 11itakuwa jibu sahihi, sijui kama watanzania tutawaelewa.
Nawasihi wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuachakubishana na kuvutana kwa mambo ambayo yako wazi hasayale ambayo yana manufaa kwa watanzania kwanimnawakilisha watu ambao wengine ambao hawana vyamakabisa. Nawasihi kwa namna ya pekee wajumbe wa chamatawata (CCM) kwani ninyi ndiyo mko wengi.
Mkumbuke pia ninyi ni wajumbe wa bunge la “kihistoria”kwa kuwa Tanzania hatujawahi kuwa na bunge kama hili tangutupate uhuru 1961, kwa hiyo mnayoheshima ya pekee, kwanihili ni bunge la kwanza la kupitisha rasimu ya watanzania kuwakatiba yao; kwahiyo mnaombwa kulinda heshima hiyo yakipekee.
Aidha napendekeza ili kulinda heshima ya bunge hili, yalemambo ambayo yanaonekana yana mabishano/mvutano wa hojakwa mfano aina ya muungano wanaotaka watanzania namaadili ya viongozi wa umma na yale yote yatakayoonekanaya mawazo tofauti yasiamuliwe na 2/3 ya wajumbe, badalayake liundwe jopo la majaji 11 toka nje ya bunge hilo ambalolitakuwa na kazi ya kupima uzito wa hoja ya mzungumzaji nakutoa alama. Na mwisho wa mabishano/mvutano majaji watatoauamuzi wa upande upi imeonekana una hoja nzito na kwamanufaa ya watanzania wote na uamuzi huo usionekane kuwaupande umeshindwa, ila hoja yao imekuwa nyepesi na hainamaslahi si tu kwa yule aliyekuwa anatetea jambo au alikuwaanapinga jambo hilo bali ni watanzania wote.
Kuamua kwa kutumia 2/3 itakuwa ni sawa na mfano wawanafunzi wawili wanabishana/wanavutana moja anasema 1 + 1 = 2 na mwingine hesabu hiyo hiyo ya 1 + 1 = 11 halafuubishani/mvutano huo uamuliwe kwa kura 2/3 ya wanafunzidarasani, na aliyesema 1 + 1 = 11 akashinda Je, litakuwa ni jibusahihi? Kwa kuwa 2/3 ya wanafunzi wameamua jibu ni 11?

Nia njema ya Rais Kikwete kuwatengenezea watanzaniakatiba yao inaweza kugeuka majanga kama wajumbe wa bungehili la katiba watakuwa mnabishana na ukweli. Na kusababishaMhe. Rais Kikwete badala ya kuingia katika historia yakuwaletea watanzania katiba yao, akaingia kwenye historianyingine kabisa ambayo hata mimi siombei kabisa. Nawataomwingiza katika hoja kati ya historia hizo ni ninyiwabunge wa bunge maalumu la katiba.
Likiundwa jopo la majaji 11 kuamua mambo yenyemvutano badala ya 2/3 litamwingiza Rais Kikwete katika historianzuri ya kuwapatia watanzania katiba waitakayo na kusababishapia wapate Tanzania waitakayo.
Ila mambo yakiamuliwa kwa kura 2/3 utashangaa 1 + 1 = 11badala ya 1 + 1 = 2, na kuharibu mchakato mzima wakumwingiza Rais Kikwete katika historia na “sisemi ibara zoteziamuliwe jopo la majaji hapana” ninasema “ibara ambazozitakuwa na mvutano mkali hasa suala la aina ya muungano namaadili ya viongozi, “ndiyo maamuzi yake yaamuliwe na jopola majaji baada ya kupima uzito wa hoja za pande zinazovutanaau kubishana badala ya kutumia 2/3 ya wajumbe wa bara naZanzibar.

Pendekezo la kutumia majaji badala ya 2/3 ni kuepukaushabiki wa vyama kwa wajumbe kupiga kura kwa upande wamjumbe wake badala ya kupigia kura uzito wa hoja kwamanufaa ya watanzania milioni 47.
Jopo la majaji nililopendekeza litoke nje na wajumbe haolijumuishe wanasheria, watu wa haki za binadamu, viongoziwa dini na watu wanaoaminiwa na umma.
Jopo la majaji nililopendekeza litoke nje na wajumbe haolijumuishe wanasheria, watu wa haki za binadamu, viongoziwa dini na watu wanaoaminiwa na umma.
Nawatakia kila la heri “bunge maalumu la katiba”
Na Mwl Anthony Gella (agella72@yahoo.com)
No comments:
Post a Comment