Na Bryceson Mathias, Kata ya Mpwayungu.
Wapembuzi wengi wa duru za kisiasa, wamekuwa wakihoji ni nani aliyefaidika na Uchaguzi wa Uchaguzi mdogo wa Kata 27 uliomalizika hivi karibuni kati ya Chama Tawala na Vyama vya upinzani! Na hasa mahasimu wakubwa, CCM na CHADEMA?
Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa ‘Domestic Political’ ya CHADEMA. Ikizingatiwa katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general politics) na siasa za kijiografia (geography politics).
Mathalani uchaguzi huu CHADEMA ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol. Kigoma, amabapo ilipoteza Kata ya Nyaisura, na Kigoma, na ikaipoka CCM Kata za Sombetini na Njombe.
Thamani ya kata ilizoshinda CHADEMA nikubwa kuliko CCM, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini Arusha ambapo sasa rasmi CCM inakuwa chama cha upinzani Arusha, CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata.
Kwa lugha nyingine ni kwamba hakukuwa na Mshindi baina ya CHADEMA na CCM dhidi ya Tathimini ya Kata hizo, lakini ukichunguza kwa undani, CHADEMA wananafasi ‘Golden Goal’ kwa kubeba Kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za CCM kuwa, CHADEMA ni Chama cha ukanda,
Kwa msingi huo, sasa inaonesha CHADEMA siyo Chama cha ukanda tena, bali ni Chama cha kitaifa na kipo kila pembe ya jamhuri hii.
Izingatiwe kuwa oparesheni M4C Pamoja Daima haikuwa maalumu kwa ajili ya uchaguzi huu bali ulikuwa sehemu ya ratiba ya chama hicho katika kutoa elimu ya uraia kwa umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Kuna wanaoamini kuwa CHADEMA kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama akina Zitto Zuberi Kabwe, Dr. Killa Mkumbo na Samson Mwigamba, eti ni "Mgogoro" uliochangia kwa 100% CHADEMA kutopata kata nyingi zaidi katika uchaguzi huo.
Kwanza ieleweke kuwa, daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba CCM, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya ambao utafiti unaonyesha ni kundi kubwa la vijana wenye umri kati ya miaka 18-26 ambao hawakuwa na sifa ya kupiga kura 2010.
Lakini hata hawa waliojiandikisha yaani wenye fursa ya kupiga kura sasa, idadi kubwa ya wapiga kura hao hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuuza shahada zao, vitisho vya Jeshi la Polisi au Green Guard na Rushwa.
Pili; Tume ya Uchaguzi, hii ni lazima juhudi za maksudi zitumike kuitoa mikononi mwa CCM, maana ni hatari kuiacha iendelee kuwa wakala wa CCM badala ya kuwa na Tume huru.
Tatu Vyombo vya dola, hapa ndipo panahitaji mkakati mkuu wa kisiasa, Jeshi la polisi ni lazima likabiliwne nalo na ieleweke vema kuwa CCM haitakoma kulitumia Jeshi hilo ama vyombo vya dola kwa ujumla; Hivyo njia mbadala ni mpaka kiwe hakipo madarakani.
SHEKHE wa Msikiti wa Nunge Dodoma, Shaban Kitilla, amekishauri Chama cha Demokrasia na Maendeleo (HADEMA) kishituke na kuangalia upya uwajibikaji wa Viongozi wake wa Mkoa na Wilaya wa Kanda ya Kati, Morogoro, na Dodoma kwa kukosa viti vyote vya Udiwani.
Akizungumza na Tanzania Daima mara baada ya Kata Tatu za Dodoma na zile za mkoani Morogoro kuchukuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati wagombea wake walikuwa wanakubalika kuliko wa CCM, Kitilla alisema;
“Wagombea wa CHADEMA walikubalika na kuvuta watu wengi kwenye mikutano yao, lakini pia wote walikuwa wazuri wa kujieleza na kueleweka na wananchi kiasi cha hotuba zao kuvuta hisia na wananchi, kiasi kwamba siku za kufunga Kampeni mikutano yao iliwafuni CCM! Kulikoni?
“Yawezekana ushirikiano wa Viongozi hawa ni Mdogo, Hawana Mkakati wa kulinda Kura, wanazidiwa na Vitisho vya Green Guard, Uwezo na Mbinu za Kiuongozi zimegota mahali hauwezi kuendelea, au wananaswa na Mtego wa Rushwa, na mengineyo mengi”. Alisema Kitilla.
No comments:
Post a Comment