Mtakumbuka kuwa mapema mwaka jana, CHADEMA kilizindua uendeshaji wa chama kwa mfumo wa kanda nia ikiwa kugatua madaraka na kupunguza mzigo wa uendeshaji kutoka makao makuu ya chama (DSM) kwenda kwenye kanda husika ili kuendelea kukisimika chama mikononi mwa wanachama kuanzia ngazi ya msingi, mwanzoni chama kilikuwa kinajiendesha kutoka makao makuu yake ya DSM, hivyo kila kitu kilikuwa kinategemewa kufanywa na kupangwa kikianzia makao makuu, kwa sasa baada ya kuzinduliwa mfumo wa kanda ambao kwa maana nyingine ni kuiishi sera ya majimbo kama jinsi ilivyo asisiwa na chama mambo mengi yanafanywa kwa usimamizi wa kanda kwa maana ya mipango ya kuimarisha chama kwenye kanda, usimamizi wa raslimali, utafiti, sera na Ilani, Mafunzo ya aina mbalimbali, program ya CHADEMA ni Msingi, sheria na haki za binadamu pamoja na masuala mengine vipau mbele kwenye kanda husika.
Makao makuu kwa sasa yamebaki na jukumu la kuhahakikisha kila kanda inapata mahitaji muhimu ya kiuendeshaji ili kila kanda ijiendeshe kwa ufanisi kwa maana ya mikakati makini, uongozi bora, sera sahihi na organisation thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na Taifa. Kwa kusimamia haya, Tayari makao makuu yameziwezesha kanda zote! na kila kanda imepatiwa gari mpya aina ya Ford Ranger, Pikipiki mpya zenye brand ya CHADEMA M4C zaidi 126 zenye PA system zenye uwezo wakuhutubia umati wa watu kuanzia 500 hadi 1000 zimeshagawiwa kwenye kanda, Megaphone ndogo zaidi ya 256 kwa ajili ya mikutano pia zimeshagawiwa kwenye kanda husika.
KANDA 10 ZA TANZANIA CHINI YA UONGOZI WA CHADEMA
1. KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI - Iringa, Mbeya, Njombe na Rukwa. Makao makuu ya kanda yako Mbeya. Mwenyekiti ni Dr Stephen Kimondo na Mratibu wake ni Frank Mwaisumbe
2. KANDA YA KASKAZINI- Kilimanjaro, Arusha, Manyara, na Tanga. Makao makuu ya kanda yako Arusha. Mwenyekiti wake ni Mh. Israel Natse na Mratibu wake ni Amani Golugwa
3. KANDA YA KATI - Dodoma, Singida, na Morogoro. Makao makuu ya kanda yako Dodoma. Mwenyekiti ni Mh. Tundu Lissu na Mratibu ni mhadhiri Emmanuel Yohana
4. KANDA YA ZIWA MAGHARIBI- Mwanza, Kagera, na Geita. Makao makuu ya kanda yako Mwanza. Mwenyekiti wake ni Peter Mekere, Mwenyekiti msaidizi ni Dr Rodrick Kabangilla na mratibu wake ni Renatus Bujiku
5. KANDA YA ZIWA MASHARIKI - Shinyanga, Simiyu, na Mara. Makao makuu ya kanda yako Shinyanga. Mwenyekiti wake ni Mh Silivester Kasulumbai, mwenyekiti msaidizi ni Madata Bernad Madata na Mratibu ni Renatus Nzemo
6. KANDA YA MAGHARIBI - Kigoma, Tabora na Katavi. Makao makuu ya kanda yako Tabora. Mwenyekiti ni Shaban Mambo, Makamu mwenyekiti ni Mussa Masanja Katambi na Mratibu wake ni Christopher Nyamwanji
7. KANDA YA PWANI - Pwani, Temeke, Ilala, na Kinondoni. Makao Makuu yako DSM ofisi ndogo Kibaha. Mwenyekiti wa kanda ni Prof Abdallah Safari, makamu mwenyekiti ni Mabere Marando na Mratibu wa kanda ni Machale Tugara
8. KANDA YA KUSINI - Lindi, Mtwara na Ruvuma. Makao makuu yako Mtwara, Mwenyekiti ni Matiko Matare, Mwenyekiti msaidizi ni Lusajo Mwangupili (Mratibu alisimamishwa, nafasi itajazwa mapema mwezi huu)
9. KANDA YA PEMBA - Kusini Pemba, na Kaskazini Pemba. Makao makuu yako macho mane Pemba Kusini. Mwenyekiti ni Zainabu mussa bakari, Makamu mwenyekiti wake ni Omar Othman Nassoro, na Mratibu wa kanda ni Hamiss issa Mohamed
10. KANDA YA UNGUJA - Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, na Mjini Magharibi. Makao makuu yako Mjini Magharibi (ina uongozi wa mpito, Bado kufanya uzinduzi na kufanya uchaguzi wa viongozi)
Ni matumaini yangu kuwa bandiko hili litasaidia wengi kujua mikoa yao iko kanda gani na hivyo kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa chama kwenye kanda zao husika hasa ukizingatia kwa sasa chama kinaendesha program ya CHADEMA ni Msingi kwenye kila kanda.
No comments:
Post a Comment