M/KITI CHAMA CHA CHADEMOKRASIA
NA MAENDELEO CHADEMA,
WILAYA YA MBARALI,
S.L.P 11,
RUJEWA-MBEYA.
KUMB. NA. CDM/MBR/RJ/01 22/12/2013
MKUU WA WILAYA YA MBARALI,
S.L.P 20,
RUJEWA-MBARALI.
YAH: MALALAMIKO YA KUBAMBIKIZWA MAKESI VIONGOZI NA
WANACHAMA WA CHADEMA KATA YA UBARUKU
Sawa na somo la hapo juu.
Ninawasilisha malalamiko kwako kuhusiana na uonevu unaofanywa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Jeshi la Polisi na kwa kushirikiana na Mwekezaji wa Mbarali ambao ulianza tangu mwaka 2010 kipindi cha kampeni. Kwanza ninaanza na viongozi wa CCM mwaka 2010 mwezi wa kumi waliorodhesha majina ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kumi (10) kuwa wameandaa mabomu kwa ajili ya kulipua Mkutano wa Mgombea Urais wa CCM ambaye ni Rais kwa sasa atakapofika Rujewa na lengo kuu waweze kukamatwa wasiweze kupiga kura na pamoja na kuwatishia wasiendelee kuunga mkono CHADEMA; mbaya zaidi waliorodhesha na biashara zao na hao wameshashitakiwa kwa makosa mbalimbali likiwemo la uchomaji moto wa kituo cha mafuta na gari ambao ni:-
1. Mhe. Diwani - Alikuwa mgombea udiwani wakati huo.
2. Alex Kiswaga - K/Katibu Kata.
3. Jackob Lyandala - Mtunza hazina wa Kata.
4. Josk Bange kwa sasa marehemu na alikufa akiwa na kesi ya kubambikizwa CCM.
5. Aldo Masangula - Mwanachama
6. Yusuph Kigunga - Mwanachama
7. Zakayo Mbila
8. Israel Mwasiyanga
9. Mikidadi Lugenge
10. Mzee Mlali - Shabiki CHADEMA
Mnamo mwezi wa nane kilifanyika kikao cha S/Kijiji vya Kata ya Ubaruku pamoja na Mwekezaji kwa Mwekezaji na kilisimamiwa na Mkuu wa Wilaya na mwezi mmoja baadaye ambao ni mwezi wa tisa waliitwa watu sita, watano wakiwa viongozi wa CHADEMA ambao ni:-
1. Mh. Diwani
2. Jackob Lyandala
3. Alex Kiswaga
4. Israel Mwasiyanga
5. Tengamaso
6. Mdindile si mwanachama.
Wakituhumiwa kuwa wanatindikali wanataka kummwagia Mwekezaji wa Mbarali na waliohudhuria kikao hicho ni Mhe. Diwani na Jackob Lyandala wengine hawakuwepo. Kwa hiyo tunaamini kuwa CCM ndio waliopeleka majina hayo kwa Mwekezaji na akayapeleka Polisi.
- Vurugu za tarehe 07/11/2013:
CHADEMA inashangaa kuona viongozi na wanachama wake kuhusishwa na kukamatwa na kufunguliwa kesi na wengine ndio walioambiwa wanatindikali na kuachwa wanachama na viongozi wa CCM wakilandalanda mitaani wakati wao ndio chanzo cha vurugu hizo.
Alex Kiswaga amekamatwa na kufunguliwa kesi ya kufunga ofisi Urunda ambayo iko Kijiji na Kata tofauti anayoishi na Jeshi la Polisi kumfungia dhamana asipewe. Kwa nini tusiamini kuwa Polisi nao wanahusika na mpango wa kuwabambikiza kesi watu hasa wanachama wa CHADEMA.
CHADEMA tunaamini Jeshi la Polisi linajua kabisa matukio yote ya Ubaruku hayakusababishwa na CHADEMA na viongozi wake kutoka tukio la kituo cha mafuta na hili la juzi, tukio la kituo cha mafuta lilichochewa na Mbunge Kilufi kwenye mkutano wa hadhara.
Na hili la juzi Chama cha CCM na viongozi wake walipiga ngoma ya maandamano ya kwenda kwa Mwekezaji na Jeshi la Polisi linajua ni kwa nini wakamatwe viongozi wa CHADEMA na wanafungiwa dhamana sababu ni hali haijatulia mara upelelezi haujakamilika.
Mwisho napenda kuitakia ofisi yako kazi njema na kuendelea kuiweka Mbarali kuwa katika amani.
Ahsante,
……………………..
PETER MWASHITI
MWENYEKITI WILAYA
CHADEMA
0753-786792
No comments:
Post a Comment