Mh. Sabreena H. Sungura, (MP) viti
maalum Kigoma, CHADEMA, aanzisha program ya kusomesha watoto yatima katika
manispaa ya Kigoma Ujiji. Kwa mwaka huu, 2014, anasomesha watoto Mia moja
(100). Ni wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule zote za manispaa. Kwa sasa amesha wapatia uniform na kuwalipia ada Watoto wote mia moja. Ms. Sungura ana imani ambayo ipo kutoka chini ya moyo wake kuwa elimu ni msingi wa maisha ya binadamu katika kufanikiwa na kuishi maisha ya furaha. Zaidi, anaamini kuwa ujinga ni audi mkubwa wa maendeleo na uwepo wa binadamu. Kwa ku simamia anacho amini kutoka moyoni mwake, Ms. Sungura ameenda kilometa zaidi na kuanzisha hii program ya kusomesha watoto ambao anaamini ni taifa la kesho.
Pichani Ms. Sungura's Graduation ceremony; Chuo cha East Ukraine National
University alipo kamata nondo ya Masters in Internatinal Law speciality. Hii inaonyesha ni vipi Ms. Sungura anathamini elimu na anatenda anacho kihubiri na kukiamini.
CHADEMA DIASPORA INATOA PONGEZI ZA DHATI KWA MOYO ANAONYESHA MBUNGE WETU MSOMI
WA SHERIA. PIA TUNAMUOMBEA AJALIWE NGUVU ZAIDI KATIKA UTUMISHI WAKE WA UMMA. ASANTE MS. SUNGURA KWA KUONESHA KUJARI UMUHIMU WA ELIMU.
No comments:
Post a Comment