TAMKO BATILI LILILOTOLEWA TAREHE 03/12/203 NA ALIYEKUWA
MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA SINGIDA NDG. WILFRED NOEL KITUNDU KWENDA KWA VYOMBO
VYA HABARI. TAREHE 6/12/2013
Ndugu waandishi wa habari,
wanachama na viongozi wa CHADEMA,
Baraza la uongozi mkoa wa Singida
lilipata taarifa za kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa Ndg WILFRED NOEL
KITUNDU kutoka kwenye mitandao ya kijamii kama vile Jamiiforum, kutoka kwa
waandishi wa habari waliopewa taarifa hata kabla ya uongozi wa chama kupata
taarifa kutoka kwa mhusika. Mara baada ya kupata taarifa hizo na kuzipitia kwa
kina, tumeona ni vyema na haki kuwapa taarifa sahihi juu ya upotoshaji
uliofanywa na ndg.WILFRED NOEL KITUNDU.
Baada ya baraza la uongozi kukaa
kikao cha dharura tarehe 4/12/2013 siku moja baada ya ndg WILFRED NOEL KITUNDU
kujiuzulu umejadili na kujiridhisha kuwa tuhuma zilizotolewa na bwana huyu ni
za UONGO, UZUSHI, UPOTOSHAJI USIYOMITHILIKA. Hivyo hatuwezi kuzifumbia macho
bali tumeamua tutoe taarifa sahihi ili kuweka kumbukumbu sawa sawa.
Ndugu waandishi wa habari,
wanachama na viongozi wa CHADEMA, katika kupitia barua yake ya kutangaza
kujiuzulu uongozi tumebaini makosa yafuatayo ambayo ni MATUMIZI MABAYA YA LUGHA
kama ifuatavyo:-
1.“….chama kinabaka na kudhalilisha
demokrasia…” katika hili tunaomba muelewe kuwa CHADEMA haijawahi na haitawahi
kutenda kosa hilo la ubakaji na udhalilishaji wa demokrasia kama alivyodai huyu
bwana kwani kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na jina lenyewe la chama kama
linavyojipambanua kwenye katiba ya 2006 CHAMA CHA “……DEMOKRASIA…..? ili
kuhakikisha hata yeye anafuata neno hilo ndiyo maana leo hii ameamua kujiuzulu
kwa shinikizo la hofu ya kuvuliwa uongozi.
2.“…upuuzi huu uliofanywa na kamati
kuu……” tunaomba ieleweke hapa kuwa kamati kuu ni chombo halali cha kikatiba
alichoshiriki yeye mwenyewe kukiuunda akiwa mjumbe halali wa vikao
vilivyoandika katiba hii. Hivyo laana hii ya upuu itamrudia yeye kwani na yeye
mwenyewe alishiriki kuunda chombo hiki. Kwa kifupi yeye amekuwa ni mzigo mkubwa
kwa kushindwa kuisimamia katiba ya chama na ndiyo maana kaondoka kwa aibu kubwa
kwani hatukutegemea mwenyekiti wa mkoa wenye majimbo 8 na kata 124
aondoke na apigwe picha na vyombo vya habari peke yake.
3. “……..kufumbia macho ujinga
wa kamati kuu….” Hapa napo kuna walakini kwani mwanademokrasia wa kweli
kama anavyojiita hawezi kukimbilia mafichoni ndipo atoe tamko kama alivyofanya
yeye kwani kama alikuwa anafikiri yuko sahihi angetumia ofisi ya chama na kuita
kikao halali ambalo ni baraza lake la uongozi na wanachama wake ndipo atoe
tamko lake. Hakuna ujinga unaoweza kuungwa mkono na mtu mmoja kama
anavyouaminisha umma. Hapa ni lazima watanzania wahoji udemokrasia wake wa
kweli upo wapi? Na hii yote ni kutokana na ujinga wakutokujua maana sahihi ya
neno “DEMOKRASIA.” Kwa ufupi huu ni ukibaraka tu.
Ndugu waandishi wa habari,
wanachama na viongozi wa CHADEMA, kwa kuwa aliyeyasema hayo alikuwa kiongozi
ambaye hatuna shaka na uelewa wake wa katiba, kanuni, itifaki na maadili ya
chama hiki ambacho sasa yeye amebaki kuwa mwanachama wake wa kawaida na tayari
matumizi ya lugha yanaonyesha kuwa yanaangukia kwenye ibara ya 10.0, 10.3 (4)
…kujiepusha na upinzani dhidi ya chama na wagombea wake na makundi ya majungu
ya kuwagonganisha viongozi na wanachama haswa wakati wa chaguzi za kichama ama
za kiserikali…” anastahili kuvuliwa uanachama wake. Hivyo apime mwenyewe.
Vile vile amevunja katiba ya chama
sura ya tano ibara za 5.1, 5.1.4, 5.1.5 kwa hiyo hastahili kuendelea kuwa
mwanachama wa Chadema chama ambacho kinabaka demokrasia.
Ndugu waandishi wa habari,
wanachama na viongozi wa CHADEMA, pia kwenye taarifa yake aliyodai ni ya chama
mkoa wa Singida ina mapungufu makubwa ambayo tunaona hakuyaandika mwenyewe bali
aliandikiwa kwani maudhui yake hayaonyeshi kama kweli yeye alikuwa mwenyekiti
wa mkoa. Katika taarifa hiyo umeudanganya umma kwani madai aliyoyatoa ni ya
UONGO ULIOVUKA MIPAKA.
Alidai kuwa yeye amejitolea kwa
hali na mali kwa kujinyima na kuipunja familia yake ili ajenge chama mkoani
Singida. Ni jambo la kusikitisha tunapoona hata wazee wanasema uongo kwa
kiwango hiki. Ili kuweka kumbukumbu sawa, CHADEMA mkoa wa Singida tunasema haya
yafuatayo:-
1.Mzee WILFRED NOEL KITUNDU
hakuwahi kushiriki hata siku moja kufanya mkutano wowote akiwa kama mwanachama
na akiwa kama mwenyekiti wa mkoa kwenye jimbo la Singida Mashariki lenye vijiji
49.
2.Hakuwahi kushiriki hata siku moja
kwenye kampeni za kugombea ubunge za Mh. Tundu Lissu. Kwa hiyo si kweli kwamba
ameleta mafanikio ya kupata wabunge 3 mkoani kwake.
3.Vile vile yeye mwenyewe ni
mtuhumiwa aliyeharibu mchakato wa kwanza wa ubunge wa viti maalumu na
hili analijua vizuri sana na kutokana na uharamia anaoujua yeye ndiyo maana
uongozi wa juu uliamua kumteu Dr Kitila Mkumbo kutengeneza utaratibu wa
kuwapata wabunge wa viti maalumu. Kwahiyo wabunge hawa wa viti maalumu siyo zao
lake.
OFISI YA CHADEMA
Ndugu waandishi wa habari,
wanachama na viongozi wa CHADEMA, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
amedai kuwa tangu mwaka 1992 hadi 2011 chama kimekuwa kikitumia nyumba yake
kama ofisi ya chama. Jambo hili si la kweli kwani kumbukumbu zetu zinatunyesha
kama ifuatavyo:-
1.Mwaka 1992 hadi 2000 ofisi ya
CHADEMA ilitolewa na Mzee KALALU ambaye kwa sasa ni marehemu. Wakiti huo mzee
Wilfred Kitundu alikuwa Mwenyekiti.
2.Mwaka 2000 hadi 2004 ofisi ya
chama aliitoa mwanachama wetu alimaarufu MAMA VERO. Kwa kipindi hiki chote yeye
hakuwa mwenyekiti wa chama bali mwenyekiti alikuwa ndugu NATANIEL MPANYA. Kwa
hiyo sikweli kwamba yeye amekuwa mwenyekiti toka 1992-2013.
3.2000 aliondolewa kwenye uongozi
kutokana na kudharau kikao cha uongozi mkoa hivyo aliondolewa kwenye uenyekiti
kabla ya kuomba kugombea tena mwaka 2004.
4.2004 aliomba kugombea uenyekiti
akapitishwa bila kupingwa kwani hakuwa na mpinzani na mwaka 2009 akagombea tena
ambapo muda wake ulipaswa kuisha mwaka 2014 mwaka kesho. Kwahiyo kuanzia mwaka
2004 – 2011 ndipo ofisi ilihamia kwenye chumba cha sebule yake.
Kwahiyo si kweli kwamba yeye
amekuwa ndiye mwenyekiti tangu 1992 – 2013 kama alivyosema kwenye taarifa yake.
MADAI YA HISTORIA YA USALITI KWENYE
CHAMA
Mzee huyu anataka umma uamini kuwa
Dr. AMANI KABURU hakuwa msaliti. Ili kujua uongo wa mzee huyu tuwakumbushe
baada ya Dr. Kaburu kufukuzwa chama ilikuwaje.
1.Nani
asiyejua kuwa baada ya Kaburu kufukuzwa CHADEMA alipewa ubunge wa Afrika
MAshariki kupitia CCM? Je, ni kweli huyu hakuwa msaliti? Majibu mnayo.
2.Nani
asiyejua kuwa Dr. Kaburu ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma? Hili i halihitaji
maelezo marefu.
3.CHACHA
WANGWE mzee huyu anafahamu vizuri kuwa yeye ni miongoni mwa wajumbe wa kamati
kuu ya wakati huo iliyomvua ungozi CHACHA WANGWE mwaka 2007. yeye kama mjumbe
wa kamati kuu iliyokaa na kuuaminisha umma kuwa WANGWE ni msaliti na akajenga
hoja ya kumuondoa madarakani sasa leo anaiona kamati kuu ni ya kupuuzi na
maamzi yake ni kipuuzi na kijinga???
Kwa hiyo udanganyifu wa namna hii
hauwezi kufumbiwa macho kwani wanaoathirika ni watanzania wanaopenda kuona
wanaongozwa na viongozi wa kweli na wenye nia ya dhati juu ya maslahi mapana ya
chama chao na taifa kwa ujumla.
HOJA YA UKANDA
Ndugu waandishi wa habari,
wanachama na viongozi wa CHADEMA, kwanza tungependa mfahamu kuwa hoja hii
imeshajibiwa sana na viongozi wetu wa sehemu zingine na hata viongozi wakuu wa
chama kitaifa lakini kwa kuwa mzee huyu ameizungumzia kwenye taarifa yake ni
vyema kuijibu.
Katika kuhakikisha chama hiki
hakimuonei mtu yeyote msaliti ndani ya chama,ndiyo maana Mwenyekiti wa CHADEMA
mkoa wa Arusha amevuliwa uenyekiti ni wa Arusha. Juzi tu mwenyekiti wa Babati
amevuliwa uongozi kwa usaliti huo huo ni kutoka kanda ya Kaskazini. Sisi
tunasema badala ya watu kutumia vivuli vya demokrasia ya kweli kupotosha umma
ni vyema wakatafakari pia kuwa kuna watu wenye uwezo wa kutafakari zaidi yao.
Vile vile tunatoa wito kwa watanzania na wanachama wote kupuuza kauli hizi za
ukanda au udini kwani zinawabagua watanzania na kutengeneza fitina na chuki
ambazo mwisho wake ni mbaya sana.
WAVAMIZI NDANI YA CHADEMA
Ndugu waandishi wa habari,
wanachama na viongozi wa CHADEMA, Katika hoja hii mzee huyu amesema uongo wa
kiwango cha hali ya juu na ambao umevuka mipaka ya uongo. Amewataja watu kuwa
wanavuruga chama na wengine hawajawahi kufanya hata mkutano mmoja wa kujenga
chama mkoani mwake. Tunasema mtu ukizeeka na akili zinazeeka tu.
Usahihi katika jambo hili, kwanza
kabisa tunapenda mfahamu kuwa CHADEMA kipo kwa ajili ya watanzania wote
wanaopenda na kukubaliana na sera za chama juu ya mstakabali w taifa lao la
baadaye. Hivyo ni haki ya kila raia wa Taaanzania kujiunga na Chadema ili mradi
halazimishwi kujiunga nacho. Vile vile lengo la mtu yeyote anayejiunga na chama
ni kuongeza mtandao na nguvu ya kujenga chama kwa uwezo wake kwa kumjibu ya
katiba na misingi yake. Hivyo hawa anaowaita wavamizi wachama ni bora zaidi
kuliko yeye kwani michango yao inaonekana kwenye chamba ambacho yeye amekuwa
mwenyekiti na mwanachama kwa miaka 20 sasa lakini mchango wake ni wa mashaka.
Mfano amewataja Mh GODBLESS LEMA
(MB), Mh MCH.PETER MSIGWA (MB) Mh. TUNDU LISSU (MB) na wengine hawa wote kwa
muda mfupi waliojiunga Chadema wameonyesha mafanikio makubwa kuliko yeye
aliyekaa zaidi ya miaka 20 kwenye chama.
Tunapenda tutoe ufafanuzi kwa
kutaja mifano michache ya michango yao katika chama ya baadhi ya watu hawa
anaowaita WAVAMIZI.
Mh GODBLESS LEMA ameshiriki kujenga
chama mkoani Singida kwa kufanya mikutano ya hadhara maeneo yafuatayo:-
1.Jimbo la Singida Mjini stendi ya zamani
2.Jimbo la Singida Kaskazini kata za MSANGE, NGAMU, ILONGERO
Je, Mzee Wilfred Kitundu amewahi
kufanya wapi mkutano hata mmoja wa hadhara wa kujenga chama?
Mh TUNDU LISSU
Ndugu waandishi wa habari,
wanachama na viongozi wa CHADEMA, kuhusu Tundu Lissu, mzee huyu amedai kuwa
Kamanda Lissu hakuwahi kufanya mkutano hata mmoja wa kujenga chama mkoani
Singida zaidi ya Jimbo lake la Singida Mashariki. Huu ni uongo na pengine nia
yake ni kutaka kuuaminisha umma kuwa kamanda Lissu hana mchango wowote wa
kujenga CHADEMA mkoani Singida. Hapa tuna wasi wasi na taarifa hii aliyoitoa
hakuiandika yeye maana aliyoyaandika hayajui.
Labda kwa faida ya wanachadema na
watanzania kwa ujumla tunapenda kutoa mifano michache tu juu ya ushiriki wa
Kamanda Tundu Lissu kujenga chama kabla na baada ya kuwa Mbunge.
1. Mh Lissu alianza kazi ya ujenzi
wa chama mkoani Singida tarehe 4,January 2008 katika jimbo la SINGIDA
KUSINI likiwa na jumla ya kata 26 na vijiji 104 kabla ya kugawanywa na
kupata majimbo ya
(i)
SINGIDA MASHARIKI
(ii)
SINGIDA MAGHARIBI
2.Kabla ya kuwa mbunge alifanya
kazi ya ujenzi wa chama kwenye JIMBO LA SINGIDA KASKAZUNI kwenye vijiji
vifuatavyo:-
i.
KINYETO
ii.
MKIMII
iii.
NTUNDUU
iv.
MINYAA
v.
MWANYONYE
vi.
KINYAGIGI
vii.
MERIYA
viii.
MIPILO
ix.
MSANGE
x.
NGAMU
xi.
MPIPITI
xii.
MTINKO
xiii.
MATUMBO
xiv.
ILONGERO.
xv.
MAKURO
3.Mh Lissu amejenga chama JIMBO LA
IRAMBA MASHARIKI kata ya IGUGUNO
4.Mh Lissu amejenga chama JIMBO LA
SINGIDA MJINI na nyinyi ni mashahidi
5.Mh Lissu amejenga chama JIMBO LA
MANYONI MASHARIKI
6.Mh Lissu amejenga chama JIMBO LA
MANYONI MAGHARIBI
Swali la kujiuliza ni kuwa TUNA
AKINA TUNDU LISSU WANGAPI?
Tunasema huu ni uongo na unafiki
mkubwa. Yeye akiwa kama mwenyekiti aje hadharani aseme amewahi kufanya mkutano
wapi wa hadhara japo wa tawi tu. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa yeye amekuwa ni
kikwazo kikubwa tu cha ukuaji wa chama mkoani Singida kwa kuzuia kuchukua
maamzi ambayo yangekisaidia chama chetu kwani kama anawatu wasiyoweza
kufanyakazi ya ujenzi wa chama angewachukulia hatua na hawakustahili hata
kupitishwa kuwania ubunge.
Hatukatai kuwa Mh Zitto amefika
Singida na kuhutubia mikutano ila si kwa kiwango mzee Wilfred Kitundu anataka
umma uamini kuwa Mh. ZITTO KABWE ndiye amekuwa anajenga chama mkoani singida
badala ya Mh Tundu Lissu. Tunapenda umma ufahamu kuwa Mh Zitto kafanya mikutano
kwenye maeneo yafuatayo
1. 2011 Mh Zitto alikuja kumnadi mgombea udiwani kwenye uchaguzi mdogo akitokea
IGUNGA kwenye kampeni za uchaguzi mdogo za ubunge.
2. Tarehe 4, June 2011 Mh Zitto alifanya mkutano wa hadhara stendi ya zamani.
3. Alifanya Mkutano kata ya SHELUI jimbo la Iramba Magharibi akiwa na Dr Kitila
Mkumbo mwezi April 2013 kabla ya uanza kwa bunge la bajeti.
MSIMAMO WA CHADEMA MKOANI SINGIDA
Ndugu waandishi wa habari,
wanachama na viongozi wa CHADEMA, kuhusu msimamo anaodai kuwa ni wa chama mkoa
wa Singida ni upotoshaji mkubwa sana kwani hauna mantiki yoyote ile na hauna
baraka za chama.
Kupitia taarifa hii uongozi wa
CHADEMA mkoa wa Singida unakanusha vikali kuhusu msimamo alioutoa kwani hakuwa
na mamlaka kutoa msimamo huo kwa sababu zifuatazo.
1.Yeye
alitoa barua ya kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti hivyo kutokana na adhima
yake hiyo, hana haki, vigezo vya kutoa msimamo alioutoa. Hivy ni batili na ni
msimamo wake binafsi
2.Hakukuwa
na kikao chochote cha chama kilichokaa kuweka msimamo huo. Hivyo tunawaomba
wanachama na watanzania wote kutokuupa umuhimu wowote
3.Kuhusu
ziara ya Katibu mkuu. Hakuna kikao kilichozuia ziara hiyo. Hivyo ziara ya
katibu mkuu iko pale pale tarehe 23/12/2013 – 24/12/2013.
4.Uongozi wa CHADEMA mkoa wa Singida unaendelea kuheshimu maamzi
halali yaliyotolewa na kamati kuu ya Chadema kwani yalitolewa na kikao halali
kikatiba.
Kwa hiyo tunatoa wito kwa wakazi wa
Singida hususani wanachama na watanzania wanaoishi kata ya SHELUI
utakapofanyikia mkutano wa hadhara kuwa wajiandae kikamilifu kupokea ugeni huo.
MAAZIMIO
1.Tunamtaka
mzee Kitundu awaombe radhi mara moja wajumbe wa kamati kuu kwa kuona maamzi yao
waliyoyatoa kuwa ni ya kipuuzi na ya kijinga.
2.Awaombe
radhi wote aliowataja kwa majina kwenye taarifa yake batili.
3.Uombe
radhi uongozi pamoja na wanachama wa Chadema mkoani Singida kwa kuwasingizia na
kuwawekea maneno ya uongo vinywani mwao.
Mwisho
Tunawakaribisha wanachama
wapya kwenye chama ili tuendelee kukijenga mkoani hapa hatimaye tuweze
kulikomboa taifa hili kutoka kwenye makucha ya mafisadi wa rasilimali za nchi.
……………………………………………………………………...
SHABAN LYIMO, KAIMU MWENYEKITI WA
MKOA
……………………………………………………
PATRICK MSUTA, KATIBU WA
CHADEMA MKOA
No comments:
Post a Comment