Huu ndiyo mkutano wa Dkt. Slaa leo Kahama mjini ambao umeanza majira ya saa 12.15 jioni ambapo watu wamekuwepo uwanjani tangu saa 8 mchana kama walivyotangaziwa.
Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), Dk. Willibrod Slaa akiagana na wananchi wa mji wa Kahama baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa CDT mjini huo jana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Kigoma na Singida. (Picha na Joseph Senga)
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibrod Slaa akiwahutubia wanachi wa mji wa Kamaha na vitongoji vyake, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuimarisja uhai wa chama katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida, uliofanyika kwenye Uwanja wa CDT mjini Kahama jana. (Picha na Joseph Senga)
Dkt. Slaa "Watanzania
tulieni, tulieni, tulieni. Wingi wenu hapa na kunisubiri kwa muda mrefu namna
hii tangu mchana kwenye jua kali ni ishara kubwa ya upendo wa dhati kwa chama
chenu na viongozi wenu, asanteni sana sana sana Kahama.
"Chama hiki ni chenu,
kipo kwa ajili ya kuwatumikia na kusimamia maslahi na matakwa yenu. Hakiwezi
kuwa chama legelege. Ni lazima ili kiweze kuwasemea watu, kwanza muhimu kiweze
kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba, kanuni, maadili na itifaki, mambo ambao
hata CCM hawana pamoja na ukongwe wao.'
"Wakati wa kampeni
2010 tuliwaambia tutasimama kidete kwa ajili yenu kuwavusha kutoka hapa kwenda
nchi ya matumaini. Ni lazima mtuone hivyo bila chembe ya shaka kuwa chama chenu
ni imara, kinaweza kusimamia misingi yake ambayo ni pamoja na katiba yake,
kisha tutakuwa na ubavu wa kupigania maslahi yenu."
"Haya
mambo tunayopitia sasa wapo wanofikiri yatatukwamisha, tunawaambia ndiyo kwanza
yanatukomaza na kutuimarisha kuwa chama imara kwenda kushika dola," Dkt.
Slaa leo mjini Kahama.



No comments:
Post a Comment