Katibu
Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibroad Slaa ameendelea na ziara ya ujenzi na kukagua
uhai wa chama, ambapo leo alikuwa na mikutano miwili kadri ya ratiba yake
aliyopangiwa na wenyeji.
Mkutano
wa kwanza ulikuwa Kijiji cha Mabamba, Jimbo la Muhambwe na mkutano wa pili
ulikuwa mjini Kibondo, ambapo pamoja na mvua kubwa kunyesha watu wamejitokeza
kwa wingi, wengine wakilazimika kusimama upenuni mwa maduka pembeni mwa Uwanja
wa Community Centre, kumsikiliza Dkt. Slaa.
Akiwa
kijijini Mabamba, Dkt. Slaa alitumia fursa hiyo kutoa salaam za rambirambi kwa
msiba mzito wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, akimtaka Rais
Jakaya Kikwete si tu kutangaza siku tatu za maombolezo bali serikali yake
inapaswa kutafakari juu ya vitendo vya kikatili inavyowafanyia watu wake, kwa
namna ile ile au zaidi ya walivyokuwa wakifanya makaburu wa Afrika Kusini.
Alisema
kuwa kutangaza siku tatu za maombolezo wakati serikali inafanya vitendo vile
vile ambavyo Mandela alivipinga kwa nguvu zote hadi akaitwa gaidi na kufungwa jela
ni sawa na kumdhihaki Kamanda huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi,
akipigania haki na utu wa binadamu.
Aliongeza
kuwa Mandela alikuwa mpigania haki ambaye hakusita kusimama na wananchi wake
hata mara moja, akiwa tayari kufa kwa ajili hiyo, kiasi ambacho alibambikiwa
kesi na kuitwa gaidi kutokana na sheria za kikandamizi zilizotungwa na
makaburu.
"Hakuwa
tayari kuwapigia magoti watawala wanaonyanyasa wananchi wasiokuwa na hatia kwa
kutumia sheria mbovu, hakuwa tayari kuona watu wanafanyiwa ukatili. Aliwapinga
makaburu kwa kila hali na mali. Tanzania tuliwaunga mkono wapigania uhuru wa
Afrika Kusini. Wengine tukawatunza hapa kwetu, tukaanzisha undugu. Ndiyo maana
nasema kwetu huu ni msiba mzito sana.
"Bahati
mbaya mie huwa sipendi unafiki na kuzunguka zunguka, leo Serikali imetangaza
siku tatu za maombolezo. Nilitarajia serikali makini badala ya kuomboleza tu,
ijitazame na kutafakari kama haifanyi matendo aliyokuwa akiyapinga Mandela. Leo
hii sisi tuna ushahidi wa wazi, mabomu yanapigwa kwenye mikutano ya hadhara,
vijana wetu wamesingiziwa ugaidi.
"Wamepigwa
shoti za umeme, wameingiziwa vyuma na chupa sehemu za siri ili tu waseme Slaa
na Mbowe waliwatuma. Ninyi hapa nasikia wanataka kuwahamisha bila hata
kuwauliza, manyanyaso ya watendaji wa serikali na vyombo vya dola yako wazi,
sasa haya si ndiyo walikuwa wanafanya makaburu na mengine hata tumeanza
kuwazidi," alisema Dkt. Slaa akishangiliwa na wananchi.
Katibu
Mkuu Dkt. Slaa pia amesisitiza kuwa kama CHADEMA kitashindwa kuchukua hatua za
kukisaidia kujisahihisha, kisha kikaanza kupindisha hata misingi yake, ikiwemo
kusimamia katiba yake, hakitaweza kufaa kukabidhiwa mamlaka na dhamana ya
kuongoza dola.
Katika
mazingira yanayofanana na yale ya jana mjini Kakonko, huku pia yakihusisha watu
'wale wale', leo kijijini Dkt. Slaa alilazimika kuingilia kati kuwazuia askari
polisi waliokuwa wakiwazuia vijana takriban saba waliokuwa wamelewa huku wakiwa
na mabango yenye ujumbe mbalimbali (ulioonekana kuandikwa kwa hati moja)
wakidai wanapingana na maamuzi ya Kamati Kuu ya kumvua nafasi ya uongozi wa
chama Ndugu Zitto Kabwe.
Dkt.
Slaa aliagiza vijana wale wapishwe njia ili wasimame mbele kabisa asome vizuri
ujumbe walioandika kwenye mabango yao, akisema hata wale ambao hawajaandika
mabango lakini wana maswali ya kuuliza kuhusu jambo lolote, watapata fursa
wakati wa 'maswali na majibu' atakapokuwa amepanda jukwaani kuzungumza na
wananchi.
Alisema
kuwa majibu yote ya masuala ya CHADEMA mbali ya kujadiliwa kwenye vikao rasmi
vya chama, majibu yake yako ndani ya katiba, ambayo ndani yake kuna maadili,
kanuni, itifaki na miongozo.
Vijana
wale waliokuwa na mabango, walionekana kukataa kupigwa picha za mnato na video,
huku baadhi yao wakiweka mabango yao kwa namna ya kuficha sura, hasa baada ya
kubainika kuwa ndiyo 'wale wale' waliobeba mabango kwenye mkutano wa jana mjini
Kakonko.
Baadae
vijana wale badala ya kutumia fursa waliyopewa ya kusikilizwa, walianza kufanya
fujo, jambo ambalo polisi hawakukubaliana nalo, hivyo wakaanza kuwasogelea kwa
ajili ya hatua, ambapo Dkt. Slaa aliwaambia kama vijana hao wameshindwa kutumia
demokrasia aliyowapatia na wanaanza kuvuruga mkutano huo, basi polisi wanajua
wajibu wao katika hali hiyo.
Jumla
ya vijana 11 walikamatwa na polisi kisha kwenda kufunguliwa jalada kituo cha polisi.
Dkt.
Slaa alitumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa maeneo hayo kwa ujasiri wao wa
kuchagua viongozi wa serikali wanaotokana na CHADEMA, wakiwemo wanawake,
akiwataka kujiandaa kufanya mabadiliko makubwa mwaka 2014, kwani utakuwa mwaka
wa ukombozi wa kweli kwani ikulu ya kwanza kwa wananchi ni Serikali ya Kijiji
au mtaa.
Kwa
hatua hiyo waliyokwisha kupiga katika mapambano ya awamu ya pili ya kutafuta
uhuru wa kweli na mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, Katibu Mkuu alitumia
mrefu kuwaambia umuhimu wa ikulu ya kwanza ambayo ni serikali ya kijiji, kisha
halmashauri ya wilaya, badala ya kuanza kufikiria ikulu ya magogoni.
Ili
kufikia matumaini ya kupata ikulu ya kijiji kisha halmashauri ili hatimaye
wapate uongozi bora na sera makini za CHADEMA wanahitaji kuendelea kujipanga
kuimarisha chama katika maeneo hayo, kwa kutumia operesheni mbalimbali
zinazoendelea ndani ya chama, hususan CHADEMA ni msingi, maandalizi ya uchaguzi
wa ndani na mafunzo kwa viongozi.
Katibu
Mkuu pia alizungumzia dhana ya haki na amani ndani ya nchi, akihusisha na
mkutano uliopaswa kufanyika mjini Arusha ambao iwapo wanasiasa wa chama tawala
wangelikuwa na dhamira ya dhati ungeweza kusaidia siasa za Arusha kufanyika
katika misingi inayothamini haki, matumaini na utu wa mwanadamu badala ya
kusimamia kiburi cha madaraka yanayopatikana kwa maguvu ikiwemo kumwaga damu za
watu wasio na hatia.
Alisema kuwa katika majadiliano yoyote yale
Kurugenzi ya Habari CHADEMA

No comments:
Post a Comment