UTANGULIZI
Mabadiliko
ya tabianchi ni jambo bayana linalotokea kwa dhahiri na kuathiri kila sehemu ya
dunia tuishiyo kwa kasi ya ajabu. Nchi yetu
ya Tanzania ni mhanga mkubwa tayari imeshaathirika sana na mabadiliko ya
tabianchi, kama inavyobainika katika namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukame
uliokithiri na wa mara kwa mara ambao una athari kubwa sana kwenye kilimo,
usafirishaji, nishati, biashara, na sekta ya uchumi-jamii. Hivi sasa zaidi ya asilimia 70 ya majanga
yote ya asili yanayotokea Tanzania yahahusiana na mabadiliko ya tabianchi
vikiwemo ukame na mafuriko.
Wakati wa
matukio hayo, kilimo katika maeneo husika hudorora au kusimama kabisa, mifugo
mingi na wanyama pori hufa kwa kukosa chakula na maji na wakati mwingine
husambazwa na mkondo wa maji yaliyofurika.
Kutokana na ukame wa muda mrefu, Tanzania kwa vipindi tofauti, imekuwa
ikiathirika na ukosefu mkubwa wa nishati, ambao umekuwa na athari kubwa kijamii
na kiuchumi. Aidha, matukio ya mafuriko
ya mara kwa mara yamekuwa na madhara makubwa kwa binadamu, mali na miundominu.
Kilimo na
ufugaji, ambavyo ni shughuli kuu za kiuchumi kwa wananchi wengi wa Tanzania,
kwa kiasi kikubwa zinategemea mvua za misimu.
Hii inamaanisha kwamba uchumi wa Tanzania, kwa kiasi kikubwa, unategemea
tabianchi. Kwa hiyo, ingependa kutoa
mwongozo katika jambo hilo. Hivyo,
waraka huu ni mwongozo wa Sera ya CHADEMA ya mabadiliko ya tabianchi.
Waraka huu
wa Sera unafafanua mpango mzima wa CHADEMA wa namna ya kushughulikia mabadiliko
ya tabianchi na masuala mengine husianifu. Inatarajiwa kwamba viongozi wetu wa
kisiasa katika ngazi za kanda, mikoa.
Wilaya na kata wataiweka sera hii
katika muktadha wa maeneo yao ili iendane na maeneo husika. Mwisho,
ninawashukuru Wajumbe wote wa Kamati Kuu kwa kuona umuhimu wa sera hii na kutoa
mawazo ya awali ambayo wataalamu wetu waliyatumia hadi kuwa na mwongozo kamili
wa sera.
Ninamshukuru
Bwana Finias Magesa kwa kuratibu mawazo yote mpaka kuandikwa kwa rasimu ya
awali ya waraka huu. Pia ninaishukuru
Kamati ya Wataalamu ya CHADEMA inayohusika na Sera kwa ajili ya kuuhariri
waraka huu na kuuboresha. Juhudi zao
zinapaswa kuthaminiwa sana kwani wamekifanya CHADEMA kuwa chama tofauti chenye
mawazo mbadala na bila shaka cha kwanza kuwa na sera inayotoa mwongozo wa mambo
yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa namna
ya kipekee kabisa, ninapenda kumshukuru kwa dhati, mshirika wetu muhimu na wa
muda mrefu, Konrad Adeneur Stiftung (KAS), kwa kugharamia uzalishaji wa waraka
huu.
………………………
Freeman
Aikael Mbowe
Mwenyekiti
wa Taifa,
CHADEMA
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
1.1 MAELEZO YA
AWALI
Athari na
Viashiria vya Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania.
Tanzania
tayari inaathirika kwa uwepo wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo pamoja na ukame
wa muda mrefu unaojirudia rudia ambao unaambatana na athari kubwa katika
kilimo, usafirishaji, nishati, biashara na sekta mbalimbali za uchumi wa
jamii. Hivi sasa zaidi ya asilimia 70%
ya majanga yote ya asili katika Tanzania yanahusika na mabadiliko ya tabianchi
ikiwemo ukame na mafuriko. Wakati wa
majanga hayo, kilimo katika maeneo yanayohusika kinadorora au kusimama, mifugo
mingi na wanyama wa porini wanakufa kwa kukosa chakula na maji, na wakati
mwingine wanabebwa na mkondo wa maji yaliyofurika.
Kama
matokeo ya ukame wa uda mrefu, Tanzania kwa vipindi tofauti imekuwa ikiathirika
na matatizo katika kilimo kinachotegemea mvua na ukosefu mkubwa wa nishati ya
kisasa, ikiwemo umeme, ambao unasababisha matatizo makubwa ya kijamii na
kiuchumi. Kwa upande mwingine, mafuriko
husababisha hali ya kukatisha tama kwa binadamu na wanyama ikiwemo uharibifu wa
mali na miundombinu.
Baadhi ya
viashiria vya uwepo wa mabadiliko ya tabianchi katika Tanzania ni pamoja na
vifo vya mifugo vilivyokithiri kutokana na ukame uliokithiri katika maeneo ya
kaskazini mwa Tanzania kama vile Monduli na Longido.
Kulingana
na takwimu za Wakala wa Hali ya Hewa Tanzania, (TMA), kwa kipindi cha miaka 50
iliyopita (kutoka 1961 mpaka 2005), hali ya hewa ya Mkoa wa Arusha inaongezeka
joto na ukavu. Wastani wa mwaka wa joto
umeongezeka kwa nyuzi moja ya sentigredi na Wastani wa mwaka wa joto
umeongezeka kwa nyuzi moja ya sentigreti na Wastani wa mvua wa mwaka umepungua
kwa asilimia 25%.
Utokeaji
wa mafuriko unaosababishwa na ongezeko lililokithiri la mvua zisizotabirika
katika maeneo makavu yasiyo na mimea inayozuia maji kutiririka na kuzama chini
kwa urahisi. Mifano iko mingi ikiwemo
mafuriko yaliyotokea Dar es salaam tarehe 21 mpaka 23 Desemba, 2011 na kuua
zaidi ya watu 40, yakiharibu nyumba nyingi na miundo mbinu. Matukio mengine ya karibuni ya mafuriko ni
pamoja na yale yaliyotokea Kilosa, Singida, Kilimanjaro na Mbeya – Mbozi katika
miaka kati ya 2006 na 2008.
Aidha,
ongezeko la joto duniani linalosababishwa na ongezeko la hewa ukaa angani
linasababisha ongezeko hatari na utokeaji wa magonjwa mapya kwa mamilioni ya
watu, hasa yale yanayoenezwa na vimelea na bacteria (vectorborn diseases)
ikiwemo magonjwa kama malaria katika maeneo yenye baridi na milima ambako kwa
asili hayakuwepo. Maeneo kama hayo ni
pamoja na Lushoto na Muheza – Amani (Tanga), Rugwe (Mbeya), Bukoba na Muleba
(Kagera), Njombe na Mufindi (Iringa).
Kwa takwimu za Wakala wa Hali ya Hewa Tanzania, Wastani wa Joto kwa
mwaka wa Mbeya na Iringa imeongezeka kwa nyuzi joto 2 za sentigredi katika
kipindi cha miaka 50 iliyopita (1963 – 2007).
Takwimu
zilizochukuliwa katika hospitali ya wilaya ya Njombe, zinaonesha kuwa wagonjwa
wa malaria hospitalini hapo waliongezeka kidogo sana katika miaka ya
tisini. Mwanzoni wagonjwa walikuwa
wachache, lakini mwaka 2007, takribani wagonjwa 10,000 walifika hospitalini
hapo na 211 walikufa. Ikumbukwe, Njombe
ni moja ya maeneo yaliyokuwa na baridi sana na hivyo kutotoa mazingira mazuri
kwa uwepo wa mbu. Magonjwa mengine ni kipindupindu,
kuhara, kichocho, typhoid na ebola katika maeneo mapya ambayo hayakuwa na
magonjwa ya aina hiyo awali.
Kwa upande
mwingine, ongezeko la joto angani na upungufu wa mvua, vimeendelea kuchangia
uyeyukaji wa barafu/theluji katika mlima Kilimanjaro.
Inakadiriwa
kuwa tangu 1912 hadi leo, takribani kati ya asilimia 50% hadi 80% ya kiwango
cha theluji katika mlima Kilimanjaro tayari imeyeyuka na kupotia. Ukweli huu unaathiri uendelevu na upatikanaji
wa maji katika mkoa wa Kilimanjaro na utalii katika mlima huu mrefu barani
Afrika. Inakadiriwa kuwa, kama hali ya
hewa itaendelea kama ilivyo sasa, kiwango cha theluji kilichobaki kitakwisha na
kupotea kati ya mwaka 2015 na 2020.
Kwa
umuhimu ule ule, kutotabirika kwa viwango na majira ya mvua na kiangazi, tayari
vinaathiri uwepo, maisha na uhamaji wa wanyama ikiwemo wanyama mwitu kwenye
mbuga za wanyama. Jambo hili ni wazi
katika Mbuga ya Wanyama ya Ziwa Manyara, ambako Ndege maji, hususani aina ya
Flamingo, wamepotea.
Kwa upande
mwingine, kuongezeka kwa usawa wa kina cha bahari, tayari kunaharibu kuta za
kuzuia maji ya bahari na kuingia maeneo ya watu na shughuli mbalimbali katika
sehemu za Pangani (Tanga) na Kunduchi Dar es Salaam), ikiwa ni pamoja na
kuchafua vyanzo vya maji ya kunywa yasiyo na chumvi chumvi katika eneo la
Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Aidha, ongezeko
hilo limesababisha uzamaji wa maeneo na baadhi ya visiwa katika bahari ya India
kama vile kisiwa cha Maziwe na Fungu la Nyani (Serikali ya Tanzania, 2006), na
uharibifu wa maisha katika mfumo wa bahari ikiwemo mimea inayolisha na kutumika
kama mazalia ya samaki na viumbe wa baharini.
Utegemezi
wa kilimo kwa mvua katika Tanzania unamaanisha kuwa uzalishaji wetu katika kilimo
unategemea kwa kiwango kikubwa mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi,
kutegemea upatikanaji na mtawanyiko wa mvua na joto.
Athari
katika kilimo ni pamoja na kupungua kwa uzalishaji katika kilimo, upungufu wa
ardhi yenye rutuba, upungufu wa chakula na mazao ya biashara na hivyo ongezeko
la umaskini.
Tafiti
mbalimbali zinazohusu mwelekeo wa joto wa muda mrefu katika ziwa Victoria,
Tanganyika na Nyasa, zinaonedha ongezeko la joto katika maji ya kina kirefu
kati ya nyuzi joto za sentigredi 0.2 mpaka 0.7 kuanzia mwanzoni mwa 1900
(Serikali ya Tanzania 2009).
Mabadiliko ya Tabianchi:
Mabadiliko
ya Tabianchi yanahusiana na mabadiliko na tofauti kubwa katika takwimu za ama
wastani wa hali ya hewa au tofauti ambazo zinadumu kwa muda mrefu (kuanzia
miaka 10 na zaidi). Maelezo haya ya
maana ya mabadiliko ya tabianchi kutokana na IPCC kwenye ripoti yake ya
tathmini toleo la tatu, yanaongeza kusema ya kuwa Mabadiliko ya Tabianchi
yanaweza kusababishwa na michakato ya ndani ya asili, ya nje isiyo ndani ya
michakato yetu, au mabadiliko ya kudumu katika historia ya mchanganyiko wa
mada/hewa angani au katika matumizi ya ardhi.
Mkataba wa
Mabadiliko ya Tabianchi wa shirika la Umoja wa Mataifa (UNFCCC) kwa upande wa
pili unatofautisha maelezo yake ya maana ya Mabadiliko ya Tabianchi
“yanayosababishwa na michakato na shughuli za wanadamu” na mabadiliko ya hali
ya hewa yanayosababishwa na kazi za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja za
wanadamu, ambazo zinabadilisha mchanganyiko wa viwango vya mada/hewa katika
anga la dunia, ambayo pia ni nyongeza kwenye mabadiliko ya asili ya hali ya
hewa yaliyotathminiwa na kulinganishwa kwa muda mrefu wa kutosha.
Maelezo ya
UNFCCC yanamtambua binadamu kama wakala muhimu wa moja kwa moja anayechangia
kwenye mabadiliko ya Tabianchi.
Kwa
kuzingatia maelezo ya IPCC, upo ushahidi wa nguvu na wa kutosha kuthibitisha
ongezeko la joto katika anga kwa miaka 50 iliyopita limesababishwa na shughuli
za binadamu. Shughuli hizo zimesababisha
kwa uchache kutokea kwa madhara makubwa ya kimazingira kama vile kulika na
kupungua kwa ukanda wa uozone, kupotea kwa biyoanuai na matukio haribifu ya
hali ya hewa kwa mazingira. Aidha,
athari za mabadiliko ya Tabianchi zinasababisha matatizo mbalimbali ikiwemo
upungufu na upatikanaji wa chakula, ukuaji duni wa uchumi, uhamiaji, usalama,
uchafuzi wa maji ya kunywa yasiyo na chumvi chumvi, ongezeko la umaskini na
usambaaji wa magonjwa ya kuambukiza katika maeneo mapya kama vile Ebola, Oma ya
Bonde la Ufa, Malaria na mengine mengi.
Sababu Zinazochangia Mabadiliko ya Tabianchi:
Sababu
nyingi zinazochangia mabadiliko ya Tabianchi zinatokana na kazi za wanadamu
kuanzia matumiazi ya nishati ya mafuta ya petrol kwa aina zake zote, matumizi
mabaya ya ardhi, na kuingilia mfumo wa ekolojia ikiwemo uchomaji na ukataji
misitu. Kazi za aina hii zinasababisha
ongezeko la uhakika la viwango vya hewa ukaa zinazoongeza joto kama vile carbon
dioxide, methane, nitrogen dioxide, na chlorofluorocarbons.
Uimara na
uthibivu wa muda mrefu wa ongezeko la viwango hivi vya hewa ukaa katika anga ni
wa muhimu kwa sababu ndivyo vinavyosharabu mionzi inayotoka duniani na kuinasa
ili kuongeza joto la dunia mpaka kiwango kinachoruhusu maisha kuendelea. Kiwango cha sasa cha hewa ukaa angani
kinakadiriwa kuwa vipande 390 kwa kila million (ppm) CO2e. kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa na kuacha
viwango vya hewa hiyo angani kata ya vipande 350 – 450 kwa kila million (ppm)
CO2e hakuepukiki.
Upunguzaji
huo ni wa lazima kwa kila sekta ili kuwezesha uwezo wa mataifa yote kustahimili
na kukabili mabadiliko ya tabianchi. Ni
lazima njia mbalimbali zilizopo za kukabili tatizo hili ambalo linaweza pelekea
mabadiliko ya kudumu ya tabianchi kwa sayari yetu dunia haziepukiki. Mfumo asilia wa ekolojia unatoa fursa muhimu
wa kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kwa haraka na kutunza uwezo wa sayari
dunia kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Ongezeko
kubwa la hewa ukaa angani linasababisha mabadiliko ya tabianchi yenye uwezo wa
kudhuru mustakabali wan chi mbalimbali duniani.
Sanyansi inakadiria kuwa kupunguza kiwango cha hewa ukaa angani hadi
vipande 350 kwa million CO2E kutasaidia dunia kurudisha nyuma hatari ya maji ya
bahari kuwa tindikali na kuyeyuka kwa ncha ya Aktika kunakosababisha kuongezeka
kwa kina cha bahari na visiwa kuzama. Kubakia katika kiwango cha vipande 450 kwa
milioni CO2einapendekezwa na sanyansi kuwa ndio kiwango cha juu cha hewa ukaa
kinachoruhusiwa angani kama hatuhitaji ongezeko la joto linalozidi nyuzi joto 2
za sentigredi, ambalo litakuwa na matokeo hatarishi na majanga ambayo
yatahatarisha uwepo wa sayari dunia yenye uwezo wa kutunza uhai wa binadamu na
wanyama na shughuli zao.
Ni muhimu
kutambua ya kuwa mfumo wa nishati wa dunia unahusika kwa zaidi ya nusu ya hewa
ukaa yote inayozalishwa duniani. Sehemu
kubwa ya hewa joto hizi ni hewa ukaa (CO2) na methane. Sehemu kubwa ya uzalishaji wa hewa joto hizi
unatokana na matumizi ya mafuta ya petrol kwa aina zake zote kama chanzo cha
nishati. Kuongezeka kwa hewa ukaa angani
kunasababisha kuongezeka kwa joto la anga ambalo wataalamu wameridhika
linahusika na mabadiliko ya tabianchi na madhara makubwa kwa mazingira.
Uchomaji
na ukataji wa Misitu kwa ajili ya malisho, makazi na shughuli zingine za
kiuchumi ni chanzo kingine kikubwa cha uzalishaji wa hewa ukaa angani, japokuwa
imekuwa inapewa uzito mdogo. Inachangia
takribani asilimia 16% ya uzalishaji wa hewa ukaa yote duniani. Hii ni sawa na hewa ukaa yote inayozalishwa
na magari yote duniani, malori, meli, matreni na ndege vikiunganishwa pamoja.
Kulinda
ekari moja ya misitu kwenye ukanda wa mvua nyingi ni sawa na kuondoa uchafuzi
wa magari 14 kutoka barabarani. Kwa
upande mwingine matumizi bora ya ardhi ni chanzo kingine cha uzalishaji wa hewa
ukaa. Upanuzi wa shughuli za kilimo
kwenye maeneo oevu na yenye maji maji, kwenye kingo za mito vimekuwa
vikiingilia uwezo wa ekolojia kuzalisha maji (chemic hemi za asili) na malisho
ya mifugo kwa nyakati zisizo na mvua.
Wanyama
mwitu na mifugo wanaathiriwa na ukame kwa sababu ya upotevu wa vyanzo muhimu
vya nyasi na ekolojia. Kama vile
haitoshi, wanadamu wameendelea kubadilisha uso wa dunia kwa njia mbalimbali
ikiwemo upanuzi wa miji, uvunaji na ukataji misitu, umwagiliaji wa maeneo kavu
na mazao, kutengeneza mabwawa na maziwa, upandaji miti, na matumizi ya ardhi
oevu na chemichemi kwa kilimo. Katika
mabara mengine, kama vile Amazon, ubadilishaji wa matumizi ya misitu kwenda
miji au shughuli nyingine kunachangia kama chanzo kikuu cha uzalishaji wa hewa
ukaa kinachoongoza katika nchi kwa takribani asilimia 70% ya hewa ukaa yote
inayozalishwa nchini mwao.
Bila
kujali vithibitisho mbalimbali juu ya uhusika wa mwanadamu katika kusababisha
mabadiliko ya tabianchi na matokeo yake mabaya kwa jamii, uchumi na maendeleo,
jitihada chache zimefanywa na kuinua uelewa wa jamii na kuwaelimisha, hususan
vijana kuhusiana na uwepo na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa mustakabali
wa maisha yao ya kila siku. IPCC
imeeleza katika ripoti yake ya tathmini ya nne, ya kwamba mabadiliko ya
tabianchi ni kitu halisi na tayari yanaendelea kutokea duniani katika spidi
kubwa. Japokuwa siyo rahisi sana
kutabiri kitakachotokea baadaye kwa usahihi mkubwa sana, ripoti hii ya nne ya
tathmini ya IPCC inaonesha kuwa kuna ujuzi na uelewa wa kutosha kuelezea na
kushughulikia athari na hatari za mabadiliko ya tabianchi yanayoendelea kwa
sasa (IPCC, 2007).
Juhudi za Kitaifa zilizopo:
Kupitia
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Serikali ya Tanzania inatoa elimu ya
mazingira kwa wanafunzi. Elimu hii
inatoa uelewa wa awali juu ya masuala mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi,
lakini mara nyingi imeshindwa kuunganisha vya kutosha uhusiano wa utaalamu wa
juu ya mabadiliko ya tabianchi, vyanzo vyake, mikakati ya kustahimili
mabadiliko hayo katika sekta mbalimbali za kiuchumi na maendeleo na njia bora
za kushiriki upunguzaji wa uzalishaji wa hewa ukaa nchini.
Aidha,
Idara ya Mazingira katika ofisi ya Makamu wa Rais, imekuwa ikijishughulisha na
mikakati mbalimbali ya kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi na
kuhamasisha upunguzaji wa uzalishaji wa hewa ukaa nchini kama sehemu ya mkakati
wa kitaifa na mchango wa nchi katika agenda za kimataifa. Hata hivyo kwa kuzingatia uwezo mdogo,
raslimali chache, mfumo legevu wa kitaasisi na mpangilio katika kushughulikia
masuala ya mabadiliko ya Tabianchi, ufanisi umebakia mdogo na hivyo matokeo si
yenye tija sana. Inatosha kusema kwamba
masuala ya tabianchi yamekuwa yakipokea umakini mdogo kutoka kwa serikali yetu
ukilinganisha na umuhimu wake.
Sera ya
Taifa ya Mazingira (1998), Sheria ya Mazingira (2004) na Mkakati wa Taifa wa
Mabadiliko ya Tabianchi na Mpango Kazi ambao unaotayarishwa kwa sasa,
havitoshelezi inapokuja kwenye ukamilifu wa muktadha, malengo, na uwepo wa
vyombo vya utekelezaji kufikia malengo kusaidiwa. Kwa upande mwingine, kwa miaka mingi serikali
imeendelea kutotoa umuhimu wa kutosha kwa suala la mabadiliko ya Tabianchi, kwa
kushindwa kutayarisha hata sera mahususi juu ya suala husika ambalo limebakia
muhimu kwenye agenda za kimataifa na hivyo kushindwa kunufaika kwa kiasi kikubwa
na fursa zilizopo.
Ni kwa
kuzingatia ukweli huu CHADEMA tunakuja na sera mbadala ya mabadiliko ya
Tabianchi ambayo itasaidia Taifa kuingia kwa undani na kivitendo na kimkakati
zaidi kuzingatia na kutoa majibu yanayotatua athari na matatizo ya mabadiliko
ya Tabianchi, wakati huo huo sera
ikijenga mazingira bora kwa watanzania kunufaika na fursa za kitaifa na
kimataifa zinazopatikana katika mabadiliko ya tabianchi ikiwemo biashara ya
hewa ukaa. Sera hii mbadala ya CHADEMA
ya mabadiliko ya tabianchi inalenga kuongoza jitihada za CHADEMA kama chama na
wadau mbalimbali katika nchi kufanikisha ushiriki wenye tija wa Tanzania katika
suala zima la mabadiliko ya tabianchi kitaifa na kimataifa.
Kimsingi
Sera mbadala ya CHADEMA ya mabadiliko ya Tabianchi inalenga kujenga uwezo na
ujuzi wa watanzania, kuwapa majukwaa ya kusemea na kushiriki utekelezaji,
kuandaa na kusimamia uwepo na upatikanaji wa dhana za utekelezaji wa sera,
kuonesha kivitendo katika jamii jinsi jitihada za kupunguza ongezeko la hewa
ukaa angani na kujenga uwezo wa kustahimili mabadiliko ya tabianchi ambayo
tayari yapo vinavyoweza kuleta tofauti kati maisha ya kawaida ya
mtanzania. Zaidi, ni kuwajengea
watanzania wa kada zote uwezo na uelewa wa kushiriki na kunufaika na fursa
zilizomo katika mabadiliko ya tabianchi katika ngazi zao zote za jamii ya
Kitanzania.
Kwa sababu
kazi za kila siku za kijamii na kiuchumi za wanadamu zinachangia kwa kiasi
kikubwa mabadiliko ya Tabianchi, ufumbuzi wa tatizo la athari za mabadiliko ya
tabianchi unapaswa pia kuhusisha uzingatiaji wa madhara na njia bora za
kustahimili na kudhibiti uzalishaji na ongezeko la hewa ukaa katika kazi za
kila siku za mwanadamu. Hivyo mikakati
inapaswa kuzingatia umuhimu wa kuzingatia masuala ya tabianchi kwa kila
mwanadamu kwa kila analolitenda kila siku.
Mfumo rasmi wa elimu na ule usio rasmi wa watanzania, taasisi za kidini
na kijamii, za serikali na zisizo za serikali, vyama vya siasa na sekta
binafsi, vyote vitumike kueneza na kusambaza taarifa sahihi, ujuzi na uelewa
juu ya athari na madhara ya mabadiliko ya tabianchi na namna bora ya
kustahimili athari hizo katika ngazi zote za jamii.
Kwa
kufanya hayo CHADEMA itakuwa imeshiriki na kuchangia kujenga uwezo na ushiriki
wa watanzania na kuingoza jamii katika kutathmini na kutumia njia bora za
kuendeleza maisha yao kwa ufanisi katika mazingira ambayo yameathiriwa au
yataathiriwa na mabadiliko ya tabianchi hivi karibuni. Sera hii inawasilisha kwa jamii uwajibikaji
wa kiwango cha juu wa CHADEMA katika kushiriki jitihada za kushughulikia na
kutatua matatizo na changamoto za kimazingira na mabadiliko ya Tabianchi kwa
faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Sera inazingatia hitaji la sheria za kimataifa za mazingira na
inaheshimu kanuni ya maendeleo endelevu ambavyo vimezingatiwa katika malengo ya
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC).
1.2
Sera za
Taifa na Mikakati iliyopo.
Kwa
kuzingatia ukweli kwamba Katiba ya sasa ya Tanzania ina udhaifu mbalimbali
katika kushughulikia changamoto mbalimbali muhimu za jamii, sera, mikakati na
sheria zingine za sekta zilizotungwa chini ya sheria hii mama zimezingatiwa
lakini uboreshwaji umefanyika na matumizi ya maeneo yanayolenga ukombozi wa
kweli wa mtanzania ndiyo yamezingatiwa zaidi.
Baadhi ya
sera za sekta zilizopitiwa kwa uchache na kuzitathmini ni zile za nishati,
mazingira, usafirishaji, ardhi, maji, misitu, kilimo, uvuvi, afya, majanga, jinsia
na utalii.
1.3
Mikataba
ya Kikanda, Kimataifa na Itifaki Mbalimbali
Sera hii
pia imezingatia mikataba ya kimataifa, kikanda na itifaki mbali mbali zilizopo
bila kuathiri matakwa ya kimaendeleo ya kitaifa. Sera imezingatia changamoto na ugumu wa
maridhiano katika suala la mabadiliko ya Tabianchi baina ya mataifa mbalimbali
yaliyoendelea na yanayoendelea yanayojikita katika maslahi binafsi na siasa za
kimataifa za nchi mbalimbali. Japokuwa
suala la mabadiliko ya tabinchi ni suala nyeti kwa mataifa yote, siasa za kimataifa
na maslahi binafsi yamelifanya kuwa suala gumu kufikia maridhiano mbalimbali ya
ushughulikiaji changamoto zilizopo.
Upunguzaji wa hewa ukaa angani na jitihada za kujenga uwezo wa mataifa
mbalimbali kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi ni za muhimu sana
lakini zimeendelewa kuathiriwa na mfumo na siasa za kimataifa (Einnersting,
2007).
Ukweli
kwmba madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanaathiri kila mwananchi katika kila
nchi, imepelkea uwepo wa maslahi binafsi yanayokinzana kimataifa na hivyo
kupelekea suala hilo kuwa gumu kufikia maridhiano katika historia ya
dunia. Masuala ya mabadiliko ya
tabianchi yanashughulikiwa kwa kuzingatia sayansi na ujuzi wa masuala ya asili
na hali ya hewa. Hata hivyo IPCC imezishinikiza
serikali za mataifa duniani kushughulikia suala hili. Msukumo na utaratibu huu mpya unatofauti na
ule wa asili wa ushirikiano wa kimataifa, na kwa nyakati tofauti umesababisha
misuguano baina ya mataifa mbalimbali.
Katika
siasa za kimataifa wakati mwingine maslahi binafsi ya taifa na itikadi yake
vinakuwa juu ya sababu zingine zozote za kuongoza maamuzi ikiwemo hata ile ya
sayansi na utaalamu unavyotaka.
Ni ngumu
kuelezea lakini sanyansi huwa inakosa nguvu yake ya kuongoza maamuzi katika
siasa za kimataifa, na mara nyingi ukweli unaweza kipindishwa au kutopewa
umuhimu stahili. Hili jambo linaweza
kuonekana kirahisi kwa maamuzi na misimamo ya Amerika, China, Kanada, Japan,
Brazil, India na nchi zingine ambao ni wachafuzi na wazalishaji wakuu wa hewa
ukaa duniani kuamua kutoendelea au kushiriki katika utekelezaji wa matakwa ya
Itifaki ya Kyoto ya upunguzaji wa uzalishaji hewa ukaa duniani huku wakijua
fika unyeti wa suala husika katika mkutano wa COP 17 Durban Africa ya Kusini.
Mikataba
ya Kikanda na Itifaki ambavyo vimezingatiwa katika utayarishaji wa sera hii ni
pamoja na Mkataba wa Uanzishaji Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki inayohusu Mazingira na Maliasili, Sera ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Itifaki ya Maendeleo Endelevu ya
Bonde la Ziwa Victoria, na mwongozo wa kufanya upembuzi yakinifu wa athari za
kimazingira na ekolojia inayoshirikisha nchi za jumuiya na mkakati wa maendeleo
ya Jumuiya ya Afrika mashariki (2011 – 2015).
Mikataba
ya kimataifa, Itifaki na sheria za kimazingira za kimataifa zilizopitiwa katika
utayarishaji wa sera hii ni pamoja na Mkataba wa shirika la umoja wa mataifa
unaohusu mabadiliko ya tabianchi na Itifaki ya Kyoto. Lengo kuu la mkataba wa umoja wa Mataifa
kuhusu mabadiliko ya tabianchi ni kufanikisha uthabiti wa mchanganyiko wa hewa
ukaa angani katika viwango ambavyo havitasababisha mabadiliko ya kudumu ya
tabianchi yatakayoshindwa kuruhusu uendelevu wa uwepo wa uhai katika dunia
yetu.
Kudumisha
viwango vya hewa ukaa angani ambavyo vitaruhusu ekolojia asilia kuwa na muda wa
kutosha kuhimili mabadiliko ya tabianchi yatokanayo na shughuli za watu na
maendeleo, kuhakikisha upatikanaji salama wa chakula na maendeleo endelevu
(UNFCCC 2005). Mikataba mingine ni ile
ya Umoja wa Mataifa kudhibiti ongezeko la jangwa (UNCCD); Mkataba wa bayonuai
ya kibailojia (CBD); Mkataba wa Biashara ya Kimataifa wa Maliasili zilizo
katika hatari ya kupotea duniani (CITIES); Mkataba wa Ramsar kuhusu ardhi Oevu
na unyevuunyevu yenye umuhimu wa kimataifa.
No comments:
Post a Comment