JESHI la Polisi mjini Kasulu jana lililazimika kupiga mabomu ya
machozi, kuwatawanya vijana takriban 15 ambao wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), walioanza kuwarushia mawe polisi na wananchi
waliokuwa wakisikiliza mkutano huo. Kitendo cha vijana hao kuwarushia mawe polisi na wananchi
kilizua mtafaruku ambapo polisi waliamua kupiga mabomu ya machozi, wakati Dk.
Slaa akiwataka vijana waliokuwa na mabango waende mbele ya mkutano awasikilize. CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kubaini
mkakati mzima unaoandaliwa kwa ajili ya kuvuruga na hatimaye ikiwezekana kufanya
jambo baya la kudhuru au kuua, ili kuharibu ziara ya Katibu Mkuu wa chama
hicho, Dk. Willibrod Slaa inayoendelea mkoani Kigoma kwa sasa.
Wakati chama hicho kikibaini njama hizo, Dk. Slaa ametoa kauli
nzito akisema kuwa atazunguka nchi nzima kama ambavyo amefanya kwa kwenda kila
mahali tangu mwaka 2011, kwa sababu Katiba ya nchi inampatia uhuru huo bila
kutegemea hisani ya mtu. Aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia wananchi wa kijiji cha
Malumba, jimbo la Kasulu Mjini, ambapo wananchi walimsubiri kwa muda mrefu
kisha kuvumilia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika maeneo hayo, wakati
wakisikiliza hotuba yake. “Naona ofisa wangu hapa Waitara anazungumza kwa kusita, mwisho
atawatia hofu wananchi wangu bure. “Kwanza sipendi sana kujibizana na hao anaowasema Waitara, hao
si saizi yangu.
“Ninachoweza kuongezea katika maneno yake hayo ni kwamba Dk.
Slaa hajawahi kuogopa, Dk. Slaa si mtu wa hofu, Dk. Slaa hajawahi kutishika. “Nilisema baada tu ya uchaguzi wa 2010 kwa sababu sijaenda
Ikulu, kazi yangu itakuwa ni kujenga chama, hiyo ndiyo kazi ya katibu mkuu. “Katika hilo tena kiongozi wa kisiasa sina mipaka. Nitakwenda
kila mahali katika nchi hii kama ambavyo nimepita kila jimbo, kila kijiji tangu
2011. “Hakuna mtu mwenye hatimiliki na eneo lolote la nchi hii. Kwangu
mimi si mara ya kwanza kutishiwa maisha. “Nimetishiwa mno. Sitaacha kuzunguka na kutetea wananchi wangu
wanyonge hawa sababu ya upuuzi fulani tu hivi. “Wanapoteza muda wao. Mlinzi
wangu ni Mwenyezi Mungu pekee,” alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa na wananchi
wa Malumba.
“Kuna vijana wanapewa mafunzo pale ofisi ya mkoa na mtu
anayejulikana kwa jina la Hamis, mtu huyo na wenzake ndiyo waliotumika kwenye
tukio la kukata mapanga wabunge wetu Machemli na Kiwia pale Mwanza. “Tunajua kuna kundi la watu walitoka jana Mwanza kwenda Kigoma
mjini kwa ajili ya kufanya vurugu, wako kwenye magari kadhaa, wanafikia idadi
ya watu 60 hivi, wanaongozwa na mabaunsa wa Matata aliyefukuzwa unachama wa
CHADEMA lakini CCM wakampatia umeya,” alisema Waitara. Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma na Meya wa Ilemela aliyeenguliwa CHADEMA,
Matata, ndiye anayeongoza kufanya hujuma hizo.
Source: Senga J. (Dec. 2013). CCM wamhujumu Dk. Slaa. Retrieved from Tanznia Daima

No comments:
Post a Comment