WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel
Sitta amesema kuwa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka kesho na
uchaguzi mkuu wa 2015, liko kundi la matajiri lililoibuka kusaidia harakati
za mmoja wa watu wanaotajwa kutaka urais. Alitaja kundi hilo kuwa linaundwa na matajiri ambao
wengi wao ni wakwepa kodi mashuhuri, watoroshaji nyara na maliasili za nchi,
watoroshaji madini, wafalme wa magendo na viongozi waliojitajirisha kupitia
rushwa na mikataba mibovu. Kwa mujibu wa Sitta, katika kundi hilo wamo pia
mawakala wa maovu mbalimbali nchini ambao kwa ujumla wao wameamua kuwa baada ya
uchaguzi mkuu 2015, nchi iongozwe na mtu ambaye pia ni mpenda utajiri kwa njia
za mkato.
“Katika mazingira haya inasikitisha kwamba viongozi
wengi hususani wenye uroho wa madaraka na mali, wamejiguza kuwa ni wachekeshaji
wa mfalme. “Wengine ni wabunge, mawaziri. Watu hao wanaonekana
kumuunga mkono na mara nyingine kujipendekeza na kumsifia kiongozi wanayejua
maovu yake kwa mategemeo ya hatimaye kupewa fedha ama vyeo,” alisema Sitta. Sitta aliongeza kuwa watu hao walianza kujipambanua
miaka miwili iliyopita kwa harambee mbalimbali kwa baadhi ya makanisa, misikiti
na makundi mengine kwa kuchangia fedha. “Harambee zimekuwa zikitangazwa kwa mbwembwe na kelele
katika baadhi ya makanisa na misikiti na makundi mengine ya kijamii kwa
kuchangia fedha ambazo kwa hesabu nilizonazo kwa kipindi cha miaka miwili ni
kiasi cha sh bilioni saba,” alisema Sitta.
Alisema kuwa kwa mkakati huo, ukusanyaji wa kodi na mapato mengine ya serikali utadorora kwa sababu matajiri waovu wanamuunga mkono mtu ambaye akishika madaraka atawaachia mianya ili wasilipe kodi. “Mtu hawezi kuchangia milioni 60 kwa sababu anampenda yule anayechangisha harambee. Anatoa fedha hizo kama kitangulizo ili na yeye aje asamehewe milioni 200,” alisema. Alisema mbali na matokeo hayo, pia huduma zote za jamii na kipato cha kila Mtanzania kitapungua na hatimaye misingi ya umoja na usawa itabomoka na kulitumbukiza taifa katika machafuko.
Source: Busagaga D. (Nov. 2013).Sitta awalipua mahasimu wake. Retrieved from Tanzania Daima

No comments:
Post a Comment