TAARIFA KWA UMMA
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
itafanya mkutano wake wa kawaida kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia
tarehe 20 hadi 21 Novemba, 2013.
Ajenda za mkutano ni kupokea, kujadili na kufanya maamuzi
kuhusu: Mihutasari ya mikutano iliyopita na yatokanayo na mikutano hiyo,
taarifa ya hali ya siasa na ripoti ya fedha.
Ajenda nyingine ni pamoja na: taarifa kuhusu mchakato na maudhui
ya mabadiliko ya katiba, taarifa ya utekelezaji wa Programu ya CHADEMA ni
Msingi na shughuli za Kanda na taarifa ya utekelezaji wa Mpango Mkakati kuhusu
maboresho.
Imesambazwa kutoka Uturuki tarehe 19 Novemba 2013 na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
No comments:
Post a Comment