KATIBU wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Adam Ngalawa, juzi alipatwa na
fedheha kubwa baada ya Katibu Mwenezi wa CHADEMA, Tawi la Bulyanhulu, Kata ya
Kakola, Philemon James, kukataa hadharani mpango wa kununuliwa ili ajiunge na
chama hicho. Akizungumza
na Tanzania Daima kwa simu jana, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha
Bulyanhulu, Emmanuel Gombega, alisema mkakati wa viongozi wa CCM katika eneo
hilo kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa, kuwashawishi wanachama wa CHADEMA kwa
fedha ulianza muda mrefu katika eneo hilo. Alisema
kuwa wiki moja iliyopita walifanikiwa kumshawishi James na mwanachama mwingine
wa CHADEMA kwa kuwapatia kiasi cha sh 300,000 kwa lengo la kuangamiza nguvu za
chama hicho cha upinzani katika eneo hilo.
Kwa mujibu
wa Gombega, baada ya viongozi hao kukubaliana na James, waliandaa mkutano wa
hadhara na kumualika Katibu wa CCM mkoa kwa ajili ya kumpokea mwanachama huyo
wa CHADEMA mwenye na nguvu za ushawishi kwa wananchi wa Bulyanhulu. “Kila hatua
waliyokuwa wakifanya, James alikuwa anafikisha taarifa kwa uongozi wa CHADEMA,
tukamueleza sasa ni wakati wa kula fedha zao na kuwakataa hadharani,” alisema
Gombeza. Aliongeza
kuwa kabla ya mkutano uliohutubiwa na Ngalawa, walifanya kazi ya kuwashawishi
wananchi wahudhurie kwa wingi wakijua kitakachotokea. Baada ya
katibu huyo wa mkoa kumaliza kuhutubia, mshereheshaji katika mkutano huo
alimuita James jukwaani kwa lengo la kurudisha kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa
ya CCM.
Pia alikiri
James kupanda jukwaani huku akikanusha kuwapo kwa mkakati wa kuwanunua
wanachama wa vyama vingine wajiunge na CCM. “Ni kweli
nilikuwa Kakola na mmoja wa wananchi aliomba kipaza sauti akauliza maswali,
lakini hakuna mtu aliyeshawishi kuwanunua wanachama wa vyama vingine, na hata
huyo unayemsema hana hadhi ya kununuliwa,” alisema Ngalawa. Alipoulizwa sifa za wanachama
wa vyama vingine wanaopaswa kununuliwa, Ngalawa alisema CCM hakina utaratibu wa
kuwanunua wananchi.
No comments:
Post a Comment