JUA
HAKI ZAKO ;Katiba ya Jamuhuri wa Muungano Tanzania ipo vizuri sana kwenye haya,
lakini serikali/utawala umekua ukikiuka HAKI hizi mbili muhimu kila kukicha.
JUA HAKI YAKO ILI UWE MTANZANIA BORA NA TETEA KATIBA YA NCHI YAKO
Katiba
yetu ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977, ibara ya 18 inayotoa haki ya
uhuru wa maoni, inasema:
(1)
Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwana maoni yoyote na
kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote
kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru
wamawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli
za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii".

No comments:
Post a Comment