Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, September 18, 2013

Wanasiasa wameuteka mchakato wa Katiba Mpya


  Baada ya muda mrefu wa Watanzania kutoshirikishwa katika mchakato wa kuandika katiba, fursa hiyo imetolewa na Rais Jakaya Kikwete. Tangu wakati wa uhuru, nchi yetu imekuwa na katiba tano ambazo ni ile ya uhuru iliyoandikwa na Waingereza na ya pili ni ile ya Jamhuri iliyoandikwa mwaka 1962. Katiba ya tatu ni Muungano iliyopatikana baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana mwaka 1964 na ya nne ilikuwa ya mpito iliyoandikwa mwaka 1965. Katiba ya nne ilidumu kwa miaka 12 hadi 1977 ndipo ikaundwa katiba ya kudumu ambayo imeendelea kuishi hadi leo. Katiba zote hizo hazikuwashirikisha wananchi kikamilifu katika uundwaji wake, bali kilifuata matakwa ya wanasiasa hasa wa chama, TANU na baadaye CCM kwani wakati huo kilikuwa kimeshika hatamu.

      Hadi Desemba 2010 wakati Kikwete anafungua mlango wa kuandikwa kwa Katiba Mpya, hapo sasa wananchi wakapewa fursa ya kutoa maoni. Ikumbukwe kwamba makada wengi wa CCM hawakufurahishwa na uamuzi huo wa Kikwete kutoa fursa kwa wananchi kuandika katiba yao. Ndiyo maana kabla ya tamko lake, viongozi wengi walibeza maoni hayo. Hoja ya kuandikwa kwa Katiba Mpya lilikuwa shinikizo la vyama vya upinzani na asasi za kiraia. Baada ya agizo la Kikwete na hatimaye kuundwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo sasa inasimamia mchakato huo, bado kiu ya wana CCM kutaka chama kiendeleze matakwa yao imeendelea. Kwa mfano, katika suala la Serikali tatu katika muungano kama lilivyopendekezwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba, limewatesa CCM kiasi cha kuendesha kampeni maalumu.
      Suala jingine linaloendelea kugomba ni kuhusu uwakilishi wa wabunge wa Bunge la Katiba ambapo inaelezwa kati ya wabunge zaidi ya 600 watakaohusika, wengi watakuwa wa CCM na bado Rais (Kikwete) atakuwa na uwezo wa kuteua nafasi 160 za makundi maalum. Hali hiyo inatoa taswira kuwa mchakato wa Katiba Mpya utatekwa na CCM, hivyo huenda tukarudi kwenye historia ileile ya chama kimoja kuandika katiba kwa niaba ya Watanzania.  Mabadiliko ya sheria yaliyopitishwa bungeni hivi karibuni na kusababisha vurugu baina  ya wabunge wa CCM na upinzani bado ni mkakati wa chama tawala kuhodhi mchakato wa katiba. Wakati CCM wakisubiri Kikwete asaini muswada uliopitishwa kwa mizengwe, vyama vya NCCR Mageuzi, Chadema na CUF vimejipanga kupinga kwa mikutano. Maoni yangu, kama kweli Kikwete alianzisha mchakato huu kwa lengo la kurudisha madaraka kwa wananchi katika katiba yao, asisaini muswada huo asubiri na kuzingatia  maslahi ya wananchi kwanza.
Source: Msuya E. ( Sept. 2013).Wanasiasa wameuteka mchakato wa Katiba Mpya. Retrieved from Mwananchi

No comments: