Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, September 9, 2013


   MBUNGE wa Arusha mjini Godbles Lema amewaomba viongozi wa dini nchini kuwaombea viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuliombea taifa katika kipindi hiki kigumu cha mchakato wa katiba mpya ambayo imeanza kuleta shida. Lema alitoa ombi hilo juzi mjini hapa katika harambee iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Frandis Ksavery Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Parokia ya Olosipa, ambapo alikuwa mgeni rasmi. “Naomba mtuombee kwani tumedhamiria kuwapigania wanyonge ndani na nje ya Bunge na hatujali majina yoyote tutakayoitwa kwa kuwa tunaamini lengo letu ni kuwakomboa Watanzania hivyo kama tutaitwa majina mabaya kwa lengo hilo basi na tuitwe,” alisema Lema.

       Katika Harambee hiyo, jumla ya sh milioni 43, zilipatikana ambapo Lema na marafiki zake walichangia sh milioni 10. Fedha hizo zilizopatikana ni sehemu ya sh milioni 120 zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya padri wa kanisa hilo ambaye hivi sasa anaishi katika nyumba ya kupanga. Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa harambee hiyo, Kaimu Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki, Arusha Padri Simoni Tengesi, alisema mbali ya ujenzi wa nyumba hiyo, kanisa lake lina mpango wa kujishughulisha na huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali na huduma nyingine za wananchi wote bila kujali madhehebu yao.

Source: Siwanjombe R. (Sept. 2013). Lema: Viongozi wa dini tuombeeni. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: