Mkataba wa kimataifa wa Vienna wa mwaka 1961 unakataza
Wanadiplomasia kujihusisha na mambo ya ndani ya nchi au taasisi
wanazowakilisha. Sheria ya Tanzania ya mwaka 1986 ina akisi vienna kama chanzo
chake. Balozi wa China amejihusisha na mambo ya ndani ya Tanzania na siasa za chama
tawala akiwa katika vazi rasmi na kutoa kauli za kukiunga mkono Chama hicho
katika mikutano ya hadhara. Balozi aliambatana na katibu mkuu wa CCM bwana Kinana na katibu wa uenezi wa
CCM bw Nape Nnauye.
'Kelele' zilipopigwa Nape alitoka kwa mtindo wa kupotosha umma akisema Balozi
alikuwa akifuatilia uwekezaji wa Pamba. Nape,mwenyeji wa Balozi alipaswa kuwa kiongozi wa serikali na si chama na wala
balozi hakupaswa kuvaa vazi la chama. Hakuna habari za serikali kumkaribisha
balozi.Nape ni kijana wa kumpuuza kwasababu yupo tayari kwa tumbo lake hata
kama kufanya hivyo ni dhalili kwake na maafa kwa taifa. Nape ni mfano mbovu wa
vijana kupewa uongozi na vijana wa nchi hii wanapaswa kumlaani kila anpotokea
hata kabla ya kunena. Mheshimiwa kinana haonekani kutumia uzoefu katika kulisaidia taifa. Jambo hili
halipaswi kufanywa na mtu wa kiwango chake. Pengine ni hofu ya chama kufia
mikononi ndiyo inamsukuma kufanya madudu haya ya aibu.
Waziri Membe amethibitisha balozi kukiuka taratibu za kimataifa na kitaifa. Taarifa ya Membe ni ya ndumilakuwili kwani mwisho amemsifu kwa kazi nzuri ili
kufunika uvunjaji sheria. Hatutegemei Membe kuchukua hatua nyingine zaidi ya
taarifa hii ya kupooza hasira za Watanzania. Yote yametokea baada ya wananchi kuonyesha kutoridhika na ukikukwaji wa sheria
za nchi na wakuu wa chama tawala kinachounda serikali iliyopo madarakani na
inayopaswa kulinda sheria za nchi. Pamoja na harakati za kuutarifu ulimwengu kuna eneo muhimu linalohusika katika
sakata hili.
CCM kimehusika kama chama cha kisiasa tena kwa uongozi wa juu wa chama. Tulitegemea msajili wa vyama vya siasa alione tatizo hili na kuchukua hatua
stahiki. Hadi sasa pengine bado anatafakari. Tunachukua fursa hii kumkukubusha kuwa kuna dalili za chama tawala kukiuka
taratibu za vyama vya kisiasa kwa kumburuza balozi katika mikutano ya kisiasa
huku CCM ikijua hilo ni kosa la kimataifa na kitaifa kwa sheria za nchi yetu. Upo uwezekano hakuna sheria ya msajili iliyokiuka. Muhimu ni kumtaka ajitokeza
kufafanua kama kilichotokea kipo katika taratibu za uendeshaji wa vyama vya
siasa au la. Ufafanuzi ni muhimu na hana sababu zozote za kujificha kwasababu anaongozwa na
sheria.
Hili tunadhani ni muhimu kwa wakati huu na kwa uzito wa tatizo kiserikali na
kichama. Endapo msajili atakaa kimya bila kutoa ufafanuzi basi tutamuomba aendelee kukaa
kimya pale Alshabaab watakapokuwa na tawi na uhusianio na vyama vya siasa au
taifa lingine litakapokuwa katika uhusiano wa kisiasa wa mambo ya ndani ya nchi
na chama kingine. Tutamataka akae kimya na kuacha kila chama kitafute njia zake hata kama kufanya
hivyo ni kuliangamiza taifa.
Nguruvi3/Jamii Forums
No comments:
Post a Comment