Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, August 4, 2013

Umeya waigawa CCM


     KUMEZUKA hali ya sintofahamu miongoni mwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa Tabora na uongozi wa CCM, baaada ya mwenyekiti wa chama mkoa, Hassan Wakasuvi, kuahirisha uchaguzi wa naibu meya. Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike Julai 31, mwaka huu, lakini haukufanyika ambapo nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na diwani wa kata ya Ipuli, Waziri Mlenda. Licha ya uchaguzi huo kuahirishwa, hakuna taarifa yoyote ya mkoa iliyoonyesha ni lini utafanyika, zaidi ya kudaiwa kuwa kuna mipango ya kutaka kuchakachua wagombea wasiotakiwa na baadhi vigogo wa mkoa. CCM wilaya ilipendekeza majina ya Musa Msamazi, Salum Luzila, Shaban Kaombwe, Alfonce Shushi, Waziri Mlenda na Ndaki ambapo ilipanga uchaguzi huo ufanyike Julai 31 mwaka huu.

       Baadhi ya madiwani wamelidokeza gazeti hili kuwa Wakasuvi ameahirisha uchaguzi huo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa kuna mgombea mmoja alikuwa hamtaki na hivyo kutaka kuchomeka chaguo lake. Kutokana na hilo, baadhi ya madiwani wamesikika wakitamka kuwa ipo siku viongozi hao wa mkoa watakiingiza chama kwenye mgogoro usioisha kutokana na ubinafsi wao kwenye uchaguzi. Inadaiwa kuwa ndani ya CCM mkoa kila kiongozi ana mtu wake katika mbio hizo za uchaguzi wa naibu meya, ambapo mstahiki meya wa manispaa hiyo, Ghulam Remtulah, akidaiwa kumbeba diwani wa Ikomwa, Musa Msamazi, japo amekana tuhuma hizo.

Source: Tanzania Daima ( August 2013). Umeya waigawa CCM. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: