Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, July 19, 2013

Wadau waanza kuichambua Rasimu ya Katiba


        Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yakiongozwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) yameanza kuchambua rasimu ya katiba ili kupata maoni ya pamoja watakayowasilisha kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Zoezi hilo la siku mbili kwa wadau hao, lilianza jana jijini Dar es Salaam na wanachama wa mashirika hayo kutoka mikoa 28 hapa nchini walishiriki. Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba, alisema washiriki watafanya kazi ya kupitia na kujadili vipengele mbalimbali vya rasimu hiyo ya mwaka 2013.

     Alitaja maeneo watakayojikita kuyachambua katika rasimu kabla ya kupata maoni ya pamoja ya kuwasilisha Tume hiyo, ni pamoja na yale yanayohusu haki za binadamu. Dk. Bisimba alisema wanachama wanaoshiriki kuchambua vipengele hivyo wamegawanywa katika makundi manane, ambao watakutana kwa siku mbili makao makuu ya LHRC ili kuhakikisha wanapata maoni ya kuwasilisha kama wanaharakati. “Tunataka kuona kama maoni tuliyoyatoa kipindi kile cha kutoa maoni yetu yaliingizwa kwenye rasimu iliyotangazwa na Jaji mstaafu Warioba,” alisema. 


Source: Makore R. (July 2013).Wadau waanza kuichambua Rasimu ya Katiba. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: