CHAMA cha
Wananchi (CUF) kinaandaa utaratibu wa kufungua kesi mahakamani dhidi ya
ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) kwa watendaji wa chama hicho. Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi Mipango, Uchaguzi
wa Bunge Shaweji Mketo,kwa niaba ya wanachama wenzake alisema, bado
wanawasiliana na wanasheria, taasisi za haki za binadamu na mamlaka nyingine
ili kupata mwongozo waweze kufungua kesi hiyo. Mketo na
wenzake watano, ni miongoni mwa watu walioonja joto ya mateso ya siku 28 kutoka
kwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambao wameweka kambi Mtwara
kudhibiti machafuko yanayotokana na madai ya kuzuia bomba la gesi asilia
lisijengwe Dar es Salaam.
Mbali na
Mketo wengine ni Mwenyekiti wa Vijana Mtwara mjini Salum Mohamed, Mwenyekiti wa
Mtwara mjini Salum Mohamed, Mwenyekiti wa Wilaya Mtwara vijijini Ismail
Jamal,Katibu wa Wilaya Mtwara mjini Said Kulaga na dereva wa CUF makao makuu
Kashinde Juma. Akisimulia
mkasa huo uliompata yeye na wenzake alisema wakiwa njiani walikutana na gari
mbili za jeshi kubwa na ndogo zikiwa njia panda ya newala na mtwara mjini,na
kuwasimamisha huku walitokea askari wapatao 50 vichakani na kuanza kuwapiga
huku wakiwasachi mifukoni. “Askari
wa JWTZ walikuwa 50 walitusachi na kuchukua fedha zangu shilingi 85,000 na
nilipoanza kuzuia fedha hizo wasizichukue ndipo walipoanza kunipiga kweli
wakanivua viatu vyangu nilivyowahi kununua nje ya nchi wakavichukua na mimi kuniachia
vyao vya jeshi hivi hapa ,”alieleza Mketo.
Alisema
walikuwa wakipigwa na fimbo, kumwagiwa maji yaliyokuwa yamewekwa barafu na
pilipili jambo ambalo liliwafanya waendelee kupata maumivu makali sana. Mketo
alisema hata hivyo kuteswa kwao ni ishara kuwa Mtwara bado inanuka damu na
hakuna usalama huku wananchi wengi wakihofiwa kufariki dunia. Hata
hivyo alisema wakati wakiendelea kuwatesa alisikika mwanajeshi mmoja akisema
wao wapo pale kwa ajili ya kutekeleza amri ya Waziri Mkuu aliyoitoa Bungeni kwamba
wananchi watakaokaidi amri ya serikali wanatakiwa kupigwa. Kiongozi
huyo ambaye aliongea kwa masikitiko makubwa huku akiwataka wenzake kuonesha
majereha kwa wanahabari alisema kuwa licha ya kuwaambia wanajeshi waliokuwa
wakiwatesa kuwa amefanyiwa upasuaji mkubwa wasimpige eneo hilo hawakujali kwani
waliendelea kumchapa na bakora katika eneo la mshono hadi lilipogeuka rangi na
kuwa nyeusi.
Alisema
kiongozi mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Mtwara mjini Salum Mohamed aliambiwa
azivute ndevu zake kwa kutumia mikono na alifanya hivyo hadi haapo zilipoanza
kuvuja damu ndipo wakamwambia walichokuwa wanakihitaji. Mketo
alisema vitendo hivyo ni vya kinyama na kwamba haviwezi kuvumilika hivyo
serikali inatakiwa kuviangalia utendaji kazi wa vyombo vya dola kwani ni
kulinda raia na si kutesa Hata
hivyo aliilaumu serikali kwa kuvifungia vyombo vya habari mkoani humo kwa
kigezo cha kwamba vinawashawishi wananchi kuandamana jambo ambalo si kweli.
Source: Palalisota (July 2013). Ushuhuda wa wanachama watano wa CUF walioteswa na askari Mtwara. Mtwara. Retrieved from Jamii Forums
No comments:
Post a Comment