January Y. Makamba afunguka hivi kuhusu John Mnyika
JohnMnyika kaweka namba yangu ya simu ya mkononi ili watu wanipigie
na kutukana. Nadhani ni siasa isiyo ya kistaarabu. Hadi sasa nimepata messages
zaidi ya 600. Sio sahihi kabisa.
Wabunge
WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini.
Harakati za mitandaoni haziondoi ukweli huo. Vilevile, kodi hii imepitishwa
tarehe 29 Juni 2013. Kwa Mbunge ambaye alikuwa na wajibu wa kulipinga siku hiyo
na kulisemea kuanzia tarehe 30 Juni 2013 kuamka leo na kutapatapa mitandaoni ni
unafiki mkubwa na ni siasa za kuangalia upepo unapovuma na ni unafiki mkubwa.
Namheshimu Zitto Kabwe kwasababu alitoa kauli immediately ya kusema anaona aibu kuwa sehemu ya Bunge
hili na kwamba wawakilishi wa wananchi wamewaangusha wananchi. Mwenzake John
Mnyika anajitoa fahamu na kufanya harakati kupitia press releases.
Suluhisho
hapa sio kulumbana wala kutupiana lawama. Suluhisho ni kurudi Bungeni na
kubadilisha pale tulipokosea. Sio kutafuta umaarufu mitandaoni. Kunapotokea
kosa, tunasahihisha haraka then we move on. Siasa sio kwenye kila jambo.
MAJIBU YA MNYIKA KWA MATUSI YA
MAKAMBA.
Kufuatia
kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu;
nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao:
Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya
Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.
Kwa mliotaka
msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la
Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January
Makamba kwamba “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika
ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia
mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:
Nieleze kwamba
sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa
kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa
maendeleo. Sitaacha
kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya
ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake.
Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu
iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.
Ambacho
sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema uongo, kwa
kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu suala hili baada
ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza kulishughulikia bungeni mara
baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi
lukuki za simu ikiwemo hii. Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba
muswada huo wa sheria ya fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni
‘muswada wa majanga ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi.
Aidha,
sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa mujibu wa
kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya kupinga kodi ya
umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote zenye kuongeza mzigo wa
gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta ya mawasiliano bali pia kwenye
sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub sector) nyeti ya mafuta.
Mlioniuliza
kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba
kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye
ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya
kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na ikalirudia
kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya Serikali; ni wakina nani
hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge walioingiza kodi hii? Na ni wakina
nani hasa waliopigia kura ya ndio kuipitisha?
Aidha,
amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba
hakubaliani na suala hili na kupita kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo,
ataje kwa majina hayo waliozidi nguvu serikali kinyume na matakwa yake.
Amenukuliwa akisema pia kwamba anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na
kwamba ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi. Ni
vizuri akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha
kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati
maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa kodi hiyo
katika mkutano ujao?
Wakati Naibu
Waziri akisema hayo, Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo
hiyo yeye ametoa kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti
la Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa
ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu
za kiganjani.
Na kwa kuwa
amesema kwamba Serikali inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito
kwa wananchi kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi
0754/0684-765644. Aidha, ni
vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa kwa majina
waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake aliyosoma bungeni
kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa majina waliomfanya arejeshe
kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la marekebisho ya muswada wa sheria ya
fedha alilowasilisha bungeni.
Nasisiza kuwa
kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni za kujivua
mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo
kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla
za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine mwenye mamlaka ajitokeze
kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha mchakato wa muswada wa kufuta kodi
hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti
2013.
Majina ya
wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika mkutano wa
hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara
kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni nitatoa mrejesho kuhusu
yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na kueleza hatua zaidi zinazopaswa
kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge hao kutajwa hadharani na hatua za
kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa.
Uongozi bora
na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa
uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi. Twende kazi.
John Mnyika (Mb)
19 Julai 2013
No comments:
Post a Comment