Kimsingi hatupaswi
kupoteza muda kujibizana na Hamy-D. Wote tunajua hoja zake siku zote ni za
upotoshwaji. Hamy Hakushindwa kuuliza a pate ufafanuzi kwa njia ya kawaida.
Bila kurejea niliyosema kwenye threads nyingine,
I) akili ya Hammy
ndiyo zilikofikia na kuishia. Hata mtoto wa darasa la pili ataona kuwa hakuna
kupishana katika kauli ya Mbowe na ya Slaa.
2)Hammy angelikuwa na
nia njema alitakiwa aulize mambo ya msingi a) mwaliko wa Mbowe ulifikishwa kwa
njia gani, ofisi ya Chama au Ofisi ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani ambayo
kimsingi ni Ofisi ya Serikali. Kama Serikali ilitaka kumwalika Mbowe Kama
Mwenyekiti wa Chama, haifahamu Ofisimya Mbowe Kama Mwenyekiti wa Chadema?
3)Hammy alitakiwa
kuuliza Kama mwaliko wa Mbowe ulifikishwa ofisini kwake tarehe ngapi na saa
ngapi! Kwa mtu yeyote mwenye akili na busara kabla hujafanya conclusion yeyote
lazima ujiridhishe na facts zako na chronological order ya facts zako ili
ufanye conclusion objective. Kwa manufaa ya wanaJF mwaliko wa Mgowe ulifikishwa
majira ya saa 5 asubuhi siku ya Dinner, kupitia ofisi ya Kambi ya Upinzani.
4) Kama Hammy
angelikuwa na dhamira safi hatua ya pili ni kuuliza Kama Mbowe alimshirikisha
Dr Slaa kuhusiana na kushiriki kwake. Kama asingelimshirikisha, conclusion
ingelikuwa sahihi.
Kwa Taarifa yenu;
mara baada ya kupata
mwaliko Mhe. Mbowe alinishirikisha na kushauriana kuhusiana na kushiriki kwake.
Tulikubaliana ashiriki kimsingi kwa kuwa kaalikwa Kama KUB, lakini pia hata
taarifa yangu ya awali ilisisitiza kuwa hatujapata mwaliko. Busarabya Hammy
ingelikuwa kuuliza je, tungelipata tungelienda au la.
Rejea kauli ya Dr
Slaa, ambayo haikusema Chadema imesusia Bali "hatujapata mwaliko".
Wrong premise produces wrong conclusion, a logical elementary philosophical
principle. Lakini kwa kuwa mwaliko wa Mbowe ulifika siku mmoja baada ya Dr.Slaa
kuhojiwa na vyombo vya habari, na kutoka kwenye magazeti asubuhi, kabla ya
Mbowe kupata mwaliko, dhana ya kupingana inatokana wapi isipokuwa kwenye akili
mgando yenye kutaka tu kuwaaminisha Watanzania kuwa Chadema kuna mgawanyiko,
kuna kutofautiana.
Kwa vile asubuhi hiyo
Mimi sikuhojiwa na gazeti lolote tena, na position ya Chama kimsingi ilibaki
hivyo kuwa Chadema Kama Chama, Mtendaji Mkuu Ofisini kwangu sina Mwaliko wala
wa Mwenyekiti wa Chama Wala wa Katibu Mkuu, sasa kupishana kunatoka wapi na
katika nini. Moja anazungumzia Ng'ombe, mwingine, Punda.Kupishana kunatoka
wapuuzi hapo. Unahitaji kwenda shule kugundua kuwa mmoja anaxungumzia ng'ombe
na mwingine Punda.
Nadhani ufafanuzi huu
unajitosheleza kwa wote wenye nia njema na kutaka kujua nini hasa kilitokea.
Imeandikwa na Dr. Slaa
Katibu mkuu CHADEMA
No comments:
Post a Comment