Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, July 23, 2013

Mwigulu aipongeza CHADEMA


      NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba, amekipongeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa ushindi, huku akitoa angalizo kwamba ushindi wao umetokana na chama hicho kuwa watetezi katika kata hizo. Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) aliyasema hayo jana asubuhi alipokuwa akihojiwa kupitia kituo cha Radio cha Passion kinachorusha matangazo yake jijini Dar es Salaam kuhusu mambo mbalimbali yaliyolihusu taifa. Alisema chama tawala kimepata funzo kupitia chaguzi hizo na ikiwamo Watanzania kutopenda kupiga kura katika mazingira hatarishi.

       “Kwa hilo tunawapongeza wameshinda, ninachoweza kusema sisi tumeondoka tu na mafunzo kwenye eneo lile kwamba Watanzania hawapendi mazingira hatarishi ya kupiga kura,” alisema. Alisema kuwa Watanzania wasifurahie ushindi peke yake, bali wanapaswa kuangalia waliotakiwa kupiga kura ni wangapi na wangapi waliojitokeza, kwa kuwa katika uchaguzi wa Jiji la Arusha wapiga kura walikuwa wachache. Alisisitiza kwamba angeweza kusema hilo ni anguko kubwa katika kata hizo endapo kata hizo zilikuwa ni za CCM halafu watu wote au zaidi ya asilimia 75 wakajitokeza kupiga kura.

Uundaji wa vikosi kwenye vyama


    Katika hilo, Mwigulu alikiri kwamba Green Guard ipo siku nyingi na hata hayo mazoezi hufanywa kwa ajili ya halaiki, kwa sababu kila mwaka CCM huwa na maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama chao. “Utaona hata picha wanazoweka, moja ilikuwa halaiki ya Kigoma ya juzi, nyingine ya Mwanza miaka 36, kwa hiyo ni halaiki na si kikosi cha mapigano,” alisema Mwigulu. Alijitetea kwamba kinachotofautisha ni mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, inaonekana kwamba wao (CCM) wanawaonea kijicho, lakini kilichopo ni malengo ya vikosi hivyo.
“Wao wanataka kuanzisha kikosi cha kujilinda, ambacho hakitakuwa kikitegemea polisi wala Jeshi la Wananchi, kwahiyo wewe hutegemei polisi na wala hutegemei Jeshi la Wananchi, hiyo umeenda kinyume cha Katiba ya nchi, kwa sababu hairuhusiwi kuanzisha jeshi lako,” alisema Mwigulu.

Source: Ngoromero H. ( July 2013). Mwigulu aipongeza CHADEMA. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: