KESI inayomkabili mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kuhusiana na vurugu zilizotokea katika chuo cha uhasibu hivi karibuni imeshindwa kuendelea jana kama ilivyopangwa hadi Julai 10, mwaka huu. Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha, Devota Msofe iliahirishwa kutokana na kutokuwepo kwa Lema mahakamani hapo. Akitoa ombi la kuahirishwa kwa kesi hiyo, mdhamini wa Lema, Sabina Francis alisema mbunge huyo amepata udhuru na hivyo kutofika mahakamani hapo jana na kuomba mahakama iahirishe kesi hiyo. Kufuatia taarifa hiyo ambayo haikupata pingamizi lolote kutoka kwa mwendesha mashtaka wa serikali, Elianenyi Njiro, Hakimu Msofe aliamua kuiahirisha keshi hadi siku hiyo. Kesi hiyo ya uchochezi wa vurugu jana ilitakiwa kuanza rasmi kusikilizwa baada ya upande wa mashtaka kusema ushahidi umekamilika na hivyo itaanza kusikilizwa tarehe hiyo iliyotajwa.
Source: Siwayombe R. (July 2013), Kesi ya Lema yakwama. Arusha. Retrieved from Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment