Mnamo tarehe
09/07/2013, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe,
Freeman Mbowe alitoa kauli kwamba wanaunda kikundi chao cha kuwalinda ambacho
watakipatia mafunzo ya ukakamavu.
Kitendo cha
chama chochote cha siasa ikiwemo CHADEMA kuanzisha kikundi cha kujihami ni
kinyume cha sheria za nchi na endapo watafanya hivyo hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
Kufuatia
kauli hiyo, Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi na litachukua hatua
kulingana na ushahidi utakaopatikana. Aidha, Jeshi la Polisi litamshughulikia
mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria bila kujali wadhifa wake.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment