WAKILI WA HENRY KILEO
NA JOYCE KIRIA WAFUNGUKA
RE: HENRY JOHN KILEO.
BAADA YA SINTOFAHAMU
KUHUSU KILICHOMSIBU HASA HENRY JOHN KILEO, NA BAADA YA MAJIBU YA JESHI LA
POLICE KUHUSU JUHUDI ZA JOYCE KIRIA KILEWO KUFAHAMISHWA ALIKO MUMEWE HENRY JOHN
KILEWO, NA BAADA YA MASWALI MENGI KWANGU KAMA WAKILI WA KILEWO NA KIRIA, NIMEONA
YAFAA NITOE MAELEZO HAYA KWA KIREFU.
Henry John Kileo
alipiwa simu na Maafisa wa Police Makao Makuu mnamo Tarehe 17/6/2013,
wakimuarifu kwamba wanataka kufanya mahojiano naye.Hawakusema ni kuhusu
nini.mara moja Kilewo akawasiliana nami kama wakili wa familia yao na Joyce
Kiria,nami nikawasiliana na maafisa hao kuwaarifu kwamba kwa kuwa nina majukumu
kadhaa ya kkimahakama, na kwa kuwa Kilewo yuko nje ya mkoa,basi ninaahidi kama
wakili kuhakikisha ninamepeleka binafsi Kilewo Makao Makuu Police mnamo Ijumaa
ya tarehe 21/6/2013.
Tarehe 21/6/2013
tuliambatana mimi, Kilewo na John Mnyika (MB) mpaka Police Makao Makuu, ambapo
Mnyika alituacha na Kilewo;mahojiano yakaanza.Kwa ujumla walimuhoji Kilewo
mambo mbalimbali kuhusiana na tukio la kumwagiwa tindikali kijana aitwaye Mussa
Tesha katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mnamo mwaka 2011.Wakati
mahijiano hayo yanafanyika,tayari kulikuwa na Case ya jinai ikiendelea huko
Igunga, ambapo washtakiwa Wanne (4) ambao ni makada wa Chadema kutoka maeneo
mbalimbali nchini walishtakiwa kama mshtakiwa nambari moja mpaka
nne.Walishtakiwa kuhusiana na tukio hilo nililolisema, la Mussa Tesha kumwagiwa
Tindikali.Walishtakiwa chini ya vifungu vya sheria ya kanuni ya adhabu, (Penal
Code, na si ugaidi).
Baada ya mahojiano na
Police yaliyomalizika kwa Kileo kuandikisha statement mpaka mnamo saa 11.30
hivi za jioni ya hiyo Tarehe 21/6/2013, Police walimnyima Kilewo dhamana, na
wakampeleka remand iliyoko Central Police Station,akalala huko. Jumamosi ya mnamo
tarehe 22/6/2013, mimi wakili, Joyce Kiria na John Mnyika tulifika Central
Police station, ambapo OCS wa hiyo Central Police Station alituarifu kwamba
amri alizonazo ni kwamba Kilewo haruhusiwi kuonana na mtu yeyote. Kama wakili
nilijadiliana masuala ya kisheria na OCS, ikalazimu kuwasiliana na maafisa wa
Police Makao Makuu ambao hatimaye waliniruhusu mimi kama wakili kwa mujibu wa
sheria kuonana na mteja wangu.
Tukazungumza na
kupeana "moyo", nikahakikisha amekula chakula kilicoletwa na mkewe
Joyce Kiria (ambaye muda wote alikuwa akimuangalia mumewe kwa mbali tu,kwani
mazungumzo yangu na Kilewo yalifanyika faragha).
Mnamo saa 7.30 hivi
tuliondoka sote (wakili, Kiria na Mnyika), na kukubaliana kurudi tena Central
Police Station Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 kumtembelea tena Kilewo, na pia
kufahamu mipango hasa ya jeshi la Police kuhusu Kilewo kwani mpaka tunaondoka
si wakili wala mkewe Kilewo aliyefahamishwa rasmi kuhusu mipango hiyo.
Nikiwa Nyumbani
nilipokea simu toka kwa Joyce Kiria akiniarifu kwamba amefika Central Police
Station jioni ya Jumamosi ya tarehe 22/6/2013 na kuarifiwa tu kwa mkato kwamba
Henry John Kilewo "ameondoka".
Ukweli kama mke
alikuwa amechanganyikiwa, na jukumu la kwanza lilikuwa kumtuliza kisaikoilojia
kwani nilifahamu kina Kilewo walikuwa wamepata mtoto muda si mrefu huko
nyuma;kwa hiyo hali ya Joyce ilikuwa delicate sana kiafya na kisaikolojia. Nikapambana kama
wakili kwa kutumia uzoefu na contacts (P.R) ili kupata tarifa ya aliko mteja
wangu.
Niliariwa tu
"off record" na maafisa wa Police kwamba Kilewo amesafrishwa kwa
ndege ya Precision kuelekea Tabora kupitia Mwanza chini ya ulinzi wa maafisa
Senior wa Police ili kule Tabora afunguliwe Case.Sikuwa na mawasiliano yeyote
na mteja wangu, na hizo taarifa "off record" ndo cha pekee
tulichokuwa nacho mimi, Joyce Kiria na uongozi wa Chadema kuhusu nini kimemsibu
Henry Kileo.
Niliendelea kupambana
kupata taarifa rasmi, na hatimaye Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 majira ya saa 6
hivi (noon) ndipo nilipopigiwa simu na mmoja wa maafisa waliomsindikiza Kilewo
kuelekea huko Tabora kwa utaratibu ule ule wa "off record", na
kuniunganisha na Kilewo, ambapo nilizungumza naye kwa kifupi kumjulia hali na
kumuhakikishia kwamba tutapigana kwa uwakili wetu wote kwa ajili yake.
Kwa hiyo mpaka muda
huo hatukuwa bado na uhakika wa 100% kwamba Kilewo yuko wapi hasa. Kw wale
mawakili wenzangu wanafahamu kwamba huwezi tegemea taarifa za kusikilizishwa
mteja kwenye simu ambayo hata si ya kwake.Wala huo si ushahidi wa alipo mtu
huyo kisheria.
Lakini ikatubidi
ku-"assume" kwamba Kilewo yuko/atapelekwa Tabora kushtakiwa.mimi na
Prof Abdallah Safari tukaanza maandalizi ya upesi upesi ya safari kuelekea
Tabora kwa gari (kwani ndege kuulekea Tabora ni Jumamosi na Jumatatu tu).
Tuliondoka kwa gari ya makao makuu ya Chadema Jumapili ya tarehe 23/6/2013,
majira ya saa 11.30 hivi za jioni. Tulisafiri usiku kucha, na tulichukuwa
"risk" ambazo kwa kawaida tusingechukuwa, ikiwemo kupita katika
mapori maarufu kwa utakaji;kilichotusukuma na kutupa moyo ni kwamba Henry John
Kilewo yuko mahali ambapo anatuhitaji sana, na hana tumaini lingine bali sisi
mawakili wake.
Tukisafiri usuku
kucha na kufika Tabora asubuhi ya Jumatatu tarehe 24/6/2013, majira ya saa 2.30
asubuhi;tumechoka hakuna mfano.Tukabadili mavazi upesi upesi na kuvaa suits
zetu na kukimbilia mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, ambapo turiarifiwa kuwa wao
hawana taarifa zozote za Kilewo. Tukaelekea Makao Makua ya Police Tabora;jibe
likawa ni lile.
Maana yake ni kwamba
sisi mawakili wa Kilewo, tuko Tabora ambayo ni kubwa has, na hatujui mteja yuko
wapi hasa. Nikafanya juhudi zile zile za "off record", na
kufahamishwa kwamba Kilewo alishikiliwa Police Station ya Nzega (masaa matatu
toka Tabora), na kwamba yuko njiani kuletwa Tabora.Hatukuwa na uhakika bado,
ila ilitulazimu kushikilia hako kataarifa kasiko rasmi, na kuendelea na
maandalizi ya case.
Majira ya saa 9 hivi
za alasiri ya Tarehe 23/6/2013 Kilewo, akiwa chini ya ulinzi mkali sana wa FFU
katika Land Cruisers Mbili za Police waliwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi
Tabora; hajala tangu jana yake. Alikuwa yeye na
wenzake wanne ambao walikuwa wamefutiwa mashtaka kwa hati ya "Nolle
Prosequi" huko Igunga, kisha kukamatwa tena mara moja na kusafirishwa kwa
ulinzi mkali sana mpaka Tabora.
Ukweli ni kwamba
tulivyoonana na Kilewo si mawakili wala KIlewo mwenyewe aliyejizuia kulengwa na
machozi;yeye akimshukuru MUNGU kwamba tumepambana na yote mpaka Tabaora kwa
ajili yake kwa kasi vile, nasi kwamba hatimaye tumeonana na mteja wetu. Tukaingia Mahakamani,
Kilewo na wenzake wakasomewa mashtaka mawili; moja chini ya sheria ya kuzuia
ugaidi kwamba walimteka kwa nia ya ugaidi Mussa Tesha huko Igunga, Tabora na la
pili kwamba walimdhuru kwa kumwagia Tindikali.
Makosa ya Ugaidi
hayana dhamana.
Mawakili tulipambana
na kutoa hoja za kisheria nne (4) dhidi ya uhalali wa mashtaka yenyewe na
utaratibu wa kufungua case husika. Tumeoimba mahakama kufuta mashtaka ya
ugaidi, au la iamuru kila mshtakiwa arudishwe kushtakiwa mahali alikokamatwa
(mfano Kilewo, Dar es Salaam).
Uamuzi wa Mahakama ni
tarehe 8/7/2013.
Kabla ya kuondoka
Tabora jana, tulipita kumuaga Henry Kilewo na wenzake katika gereza la Uyui.
Wote wako na combat zao za chama chao, na wako imara, hasa baada ya kuona
mawakili wako imara.
Cha msingi ni kuomba
MUNGU aipe mahakama ujasiri.
Peter Kibatala,
Advocate
No comments:
Post a Comment