a.
UZITO WA KAULI YA LUKUVI.
Mwenyekiti
Mbowe alizungumza jana, na wakati anaeleza ushahidi uliopo, na ushuhuda uliopo
juu ya tukio hili, ameeleza vilevile kushangazwa na kauli za Waziri Lukuvi. Kwa
hiyo katika nukta hii, tuongeze tu baadhi ya mambo ya msingi, ikizingatiwa kuwa
waziri Lukuvi ni Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge. Kauli yake, akiwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, inamaanisha ni Ofisi ya Waziri Mkuu imezungumza
Bungeni.
b.
LUKUVI AMESEMA UONGO HUKU AKIJUA UKWELI
Kauli
ya Lukuvi inapaswa kubebwa kwa uzito mkubwa, na kwa kauli hiyo imedhihirika
kwamba ni sera ya serikali kusema uongo, huku ikijua ukweli. Kauli yake
imedhihirisha kwamba, jambo hili la kutaka kulidanganya Taifa, lina uratibu wa
serikali kwa ujumla wake. Kama Waziri wa Uratibu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri
Mkuu ndiye Mkuu wa shughuli za serikali bungeni) anaweza kutoa uongo wa namna
hiyo, maana yake kauli hizi zimeratibiwa, na hivyo serikali bungeni imepoteza
uhalali wa kimaadili (moral authority) wa kuzungumza, kwa sababu imeratibu
uongo wa moja kwa moja.
c.
ASKARI WA FFU ALITUPA BOMU NA ALITOROSHWA NA ASKARI WENZAKE
Kauli
ya Waziri huyu iturudishe nyuma tu. Wakati anazungumza kwamba polisi
walishindwakumkamata mhalifu kwa sababu eti wananchi wamechochewa muda mrefu na
hivyo kulichukia jeshi la polisi kwa kiwangu cha polisi kushindwa kutekeleza
wajibu wake wa kumkamata mhalifu, wakati ukweli wa mikanda tuliyo nayo
unaonyesha kuwa polisi ndio ambao waliamua kumtorosha mhalifu.
Sio
tu kumtorosha kwa magari, bali kwa matumizi ya bunduki na bastola kuwapiga
risasi wananchi waliokuwa wanafanya ulinzi shirikishi wa kuelekea kumkamata
mhalifu waliyemwona, kwa sababu tu mhalifu huyo amevaa mavazi ya FFU, kwa
sababu tu mhalifu huyo ni mwenzao. Polisi hawa wakatekeleza uhalifu mwingine wa
kupiga raia risasi ili kulinda uhalifu. Jeshi la namna hii haliwezi kutetewa.
d.
WANAOWATUMIA POLISI VIBAYA NDIO WANAWATETEA POLISI.
Watetezi
pekee wa jeshi la namna hii ni watu kama Waziri Lukuvi, ambaye ndani ya jimbo
lake alituhumiwa bungeni kulitumia vibaya jeshi la polisi, kumtumia vibaya
Kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda. Lakini Lukuvi aliposimama akaenda mbele
zaidi, sio tu ndani ya jimbo lake, akafikia hata hatua ya kumkingia kifua
Michael Kamuhanda, ambaye ripoti ya tume ya haki za binadamu na utawala bora
inamhusisha moja kwa moja na kusimamia opereshein iliyosababisha mauaji ya
mwanahabari Daudi Mwangosi.
Kama
ambavyo alimtetea Kamuhanda kwa mauaji ya Daudi Mwangosi kwa kupigwa na bomu
tumboni, ndivyo ambavyo Lukuvi amesimama bungeni kutetea askari aliyeua raia
kwa bomu, askari walioua raia kwa risasi ni mwendelezo wa serikali ya CCM
kutetea mauaji. Ni ishara wazi kwamba mauaji ya namna hii yanayotetewa na
serikali ni wazi yamepangwa na serikali.
e.
SERIKALI, CCM WANAFANYA PROPAGANDA BADALA YA KUTOA NAFASI YA MAOMBOLEZO .
Sote
tuna majonzi, sote tunaomboleza. Ni bahati mbaya kuwa serikali, CCM na bunge,
badala ya kutoa nafasi kwa maombolezo, wakati ambapo hatujawazika wenzetu,
wakati ambapo tuko katika kipindi cha maombolezo, wao badala ya kuomboleza
wanafanya propaganda.
f.
TAMKO HILI LINAKUJA SASA KUKANUSHA UONGO.
Tumelazimika
kuzungumza jambo hili badala ya kuzungumzia majeruhi, ambao wapo hospitali na
tunaendelea kuwahudumia mpaka sasa, badala ya kuzungumzia marehemu, ambao lewa
wanapewa heshima, wengine watapewa heshima kesho, tumelazimika kuyazungumzia
haya kwa sababu UONGO UKIACHIWA, UKASEMWA, UKASEMWA, UKASEMWA, watu wanaweza
kuamini kwamba ni ukweli. Lakini ni wazi, UKWELI UKISEMWA WATU WACHACHE
WANAWEZA KUDANGANYIKA KWA MUDA MFUPI SANA, LAKINI SIO WATU WOTE KWA WAKATI
WOTE.
Watanzania
tusikubali kudanganyika, kwa pamoja tuungane katika kipindi hiki kigumu cha
maombolezo, tuendelee kusimamia UKWELI, kuueleza UKWELI.
g.
WAUAJI WAWAJIBISHWE.
Lakini
baada ya kipindi hiki cha maombolezo kwa mauaji kama haya na mauaji mengine
ambayo yametokea muda mrefu katika taifa letu, ni lazima tufike hatua tuseme
hapa imetosha. Ifike hatua tuseme, waliohusika na mauaji haya, si tu
yaliyotokea Arusha Juni 15 mwaka huu, bali waliohusika na mauaji ya kuanzia
yale ya Arusha Januari 5 2011, na mauaji yaliyofuatia baada ya hapo: mauaji ya
Igunga Mwezi Oktoba 2011 ya Marehemu Mbwana Masoud, aliyekutwa ameuawa na
kutupwa. Mauaji yaliyofuata Arumeru, alipochinjwa kiongozi wa Chadema Marehemu
Mbwambo aliyechinjwa kwa msumeno, na baadaye askari Polisi wakadiriki
kumtorosha mtuhumiwa huyo mahakamani na mpaka leo hajapatikana, na mauaji yote
yaliyotokea baada ya hapo, ifike hatua tuseme sasa imetosha.
Ifike
hatua tuiwajibishe serikali, ambayo baada ya kushindwa kubaki madarakani kwa
kuwatumikia wananchi, baada ya kushindwa kubaki madarakani hata kwa kutumia
ufisadi na rushwa, kutoa rushwa kwenye chaguzi, lakini wananchi bado wanakubali
mabadiliko. Baada ya kushindwa kung'ang'ania madarakani kwa siasa za UONGO, SIASA
CHAFU ZA PROPAGANDA ZA UDINI, UKABILA n.k., sasa wanafikiri kwamba wanaweza
kung'ang'ania madarakani kwa UMWAGAJI WA DAMU.
h.
HAKUNA DOLA ILIYODUMU KWA KUMWAGA DAMU YA RAIA WAKE.
Historia
ya dunia inaonesha kuwa hakuna dola iliyokataliwa na wananchi kwenye sanduku la
kura, kwa nguvu ya umma, ikafanikiwa kubaki madarakani kwa kutumia askari, kwa
kutumia umwagaji damu. Tanzania tunapita njia hiyo. Tusielekee huko.
i.
CHADEMA TUTETEE AMANI HUKU TUKIDAI HAKI.
Sisi
Chadema tunapenda amani ya nchi yetu, tutaendelea kutetea amani ya nchi yetu.
Lakini hatutarudi nyuma katika kudai haki. Haki za sisi tunaoishi, haki za
waliokufa na haki za watakaokufa. Hatutaacha, kwa sababu tukifanya hivyo
itakuwa ni usaliti kwa imani kubwa ambayo wananchi wameipa Chadema.
John Mnyika
No comments:
Post a Comment