"Ni kweli alikuwa polisi Dodoma,
alikoitwa kwa madai ya kutoa lugha ya matusi kwa Ndugu Mizengo Pinda, lakini
hajaandikisha maelezo, kwa sababu 3, zifuatazo:
1. Wakili wake, Tundu Lissu,
amewaambia kuwa Polisi hawawezi kumkamata na kumhoji Mbunge Sugu, iwe ukumbini,
maeneo ya bunge, au nje ya maeneo ya bunge, wakati bunge likiendelea,
kutokana na parliamentary immunity aliyonayo hadi polisi watakapofuata taratibu
zinazotakiwa.
2. Neno hilo wanalotuhumu kuwa ni
lugha ya matusi, si tusi kwa sheria za nchi yetu, bali linaweza kutumika kwa
vitu au mtu anayefanya matendo au kusema maneno yanayostahili kuitwa
hivyo.
3. Wakili wake kawauliza, nani
mlalamikaji katika tuhuma hizo, je wamepokea malalamiko ya Ndugu Pinda
mwenyewe? Majibu yamekuwa yenye kigugumizi kingi.
Wameondoka polisi kwa makubaliano ya
kurudi kesho asubuhi.
Tumaini Makene
CHADEMA
Senior Information(Press) Officer
No comments:
Post a Comment