Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa
kwa njia mbalimbali za upashanaji habari tangu jana juu ya vitu viwili ambavyo
vyote vinamhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Ndugu Wilfred
Mganyizi Lwakatare.
1. Kwamba atafanya press conference
leo, (watu wale wa upande wa pili wameenda mbali hata wametaja muda eti ni saa
4 asubuhi)
2. Atakuwa kwenye mizunguko ya
mikutano ya kampeni katika chaguzi ndogo za udiwani zinazoendelea katika hatua
ya lala salama maeneo mbalimbali nchini.
Usahihi.
Kwa kuzingatia masuala kadhaa hasa
mikakati ya kitaalam katika mapambano ya kisiasa, hususan katika suala hili,
press conferense iliahirishwa tangu jana mapema asubuhi, baada tu ya baadhi ya
vyombo vya habari kuwa vimetangaza kuwa itafanyika leo, Alhamis. Tuliviarifu
vyombo vya habari hivyo. Imesogezwa mbele na taarifa zitatolewa tena.
Suala la mizunguko kwenye kampeni za
uchaguzi mdogo...hakuna kitu kama hicho kwa sasa.
Pamoja na kwamba kuna watu wenye
mapenzi mema kabisa na vuguvugu la mabadiliko wamekuwa na hamu ya kutaka
kumsikia kamanda mwenzao, ndugu Lwakatare akizungumza majukwaani baada ya miezi
mitatu ya 'ukatili' mkubwa, pia tumebaini kuwa watu wa upande wa pili, wanataka
sana kujua CHADEMA sasa inajua kiasi gani juu ya njama za kuibambikia ugaidi,
utekaji na mauaji.
Hivyo upande huo wa pili, ambao
unaonekana dhahiri kuwa under pressure ya kutojua kiasi gani mipango yao
inajulikana na itaumbuliwa kwa kiwango kipi, umekuwa ukieneza habari za
Lwakatare kufanya mikutano ya hadhara kwenye kampeni za uchaguzi wa madiwani,
kitu ambacho si kweli.
Baada ya hila na uovu wa watawala na
vibaraka wao kushindwa katika jaribio lingine kubwa kabisa wao kuwahi kupanga
dhidi ya wimbi la mabadiliko na kutaka kuzuia kasi ya CHADEMA kuwaondoa
madarakani, tumwache ndugu Lwakatare apumzike na familia, wakati mipango makini
ikifanywa kwa ajili ya matukio yote mawili ambayo Watanzania wanategemea na
kuyasubiri kwa hamu yafanyike; mkutano na press conference.
Kitu kimoja cha uhakika ni kwamba,
watu wa upande wa pili, ambao tayari hofu yao inajulikana, hawataweza
kumchagulia Lwakatare wala kuichagulia CHADEMA kitu gani cha kusema, kama
ambavyo wameanza kufanya kupitia forums mbalimbali. Let tthem cool down,
wasiwasi wa nini! Yote yakayosemwa itakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya
Watanzania, haitakuwa kwa ajili ya kuifurahisha 'status quo'.
Ukweli
haujawahi kushindwa na uongo, wala dhuluma haijawahi kuishinda haki. Vyote
viwili, ukweli na haki, vinaweza kuchelewa tu, lakini hatimaye huwadia. Kwa
sababu Lila na Fila havitangamani.
No comments:
Post a Comment